Mtaji wa laki saba unatosha sana mkuu, kuna jamaa yangu yeye huwa anaanza na laki mbili tu, anachofanya anatafuta vijana wanaoaminika wa kitaa ambao hawana kazi, anatafuta location nzuri na kuilipia ,anawanunulia jiko na vikoro koro kibao, na mtaji wa kuanzia anawakabidhi kwa maandishi kwa sharti la kila siku wanamletea Tshs 10,000 tu.
Jamaa anapiga sana hela, na bahati nzuri hawa vijana nao huwa wanafurahia kazi maana jamaa huwa hawabani wala nini,na wanakula hapo hapo, wengi chipsi hizo hizo ndio msosi wao wa mchana, jioni ndio wanahangaika kula magetoni kwao, yeye anachotaka ni Tshs 10,000 yake daily na kazi isife, ukipata hata millioni kwa siku yeye hana habari ilimradi umpe mwekundu wake.
Ukiwa na nia nzuri tafuta location hasa maeneo ya vyuo au sehemu zenye muingiliano wa kibiashara au gesti nzuri ambayo kuna wazinzi wengi, utapiga sana hela.
Kwa uswahilini maneno ya Sinza, Mabibo NIT sokoni, Manzese barabara ya kutokea tiptop kuelekea Mabibo jeshini, Kigamboni chuo cha mwalimu Nyerere, Mabibo Hostel, Tabata yote, Kawe Ukwamani, Temeke sokoni, Kinondoni mwajuni, Kinondoni studio, Mikocheni maeneo ya Kisiwani pale yana biashara kubwa sana ya chipsi.
Nimeona pia watu wanaingia mpaka kwenye shule za msingi na sekondary wanatengeneza chipsi kavu kidogo za 200 wanazifunga, watoto wanakula sana, na kwa kuwa wanaofanya hivi wanaongezeka kila siku inaonekana mfumo huu wa mashuleni unalipa sana.