Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Dar maeneo mengi biashara ya chips inalipa ila zaidi angalia sehemu ambapo wanawake ni wengi yani population ya wanawakr ni kubwa hapo utapiga pesa na laki 7 inatosha sana
 
Nahitaji kujua bei ya vitu vifuatavyo kwa nyakati hizi, kabati la kioo cha kuuzia chips cha wastani, gunia la viazi za chips, jiko la kukaangia chips la umeme, jiko la kukaangia chips la mkaa, gunia la mkaa, mafuta ya kupikia ndoo lita 20,
Asanteni
 
Kabati linaanzia 150,000 mpaka 200000.jiko la Mkaa 25,000 mpk 30000.Viazi inategemeana na msimu sasa ivi viko juu inaeza ikawa 100000 mpk 120000 .
 
Kwa wenye uzoefu, ukiajiri mtu inatakiwa uchukue kiasi gani per day? Or process nzima ya operation ipoje?
 
Kwa wenye uzoefu, ukiajiri mtu inatakiwa uchukue kiasi gani per day? Or process nzima ya operation ipoje?
kwa dar huwa wanalipwa on daily basis ..mara nyingi wanakuwa wawili au watatu.....kiongozi around 10,000 ,msaidizi 5,000
 
Daah aisee na mimi ningeomba nialikwe nije kuchukua ujuzi, nina imani sijachelewa
 
Habarini wana-jf.

Nahitaji kufanya biashara ya chips ya kisasa hapa Dar, lakini nahitaji mtu wa kuungana naye ili tuunganishe akili na mitaji maana umoja ni nguvu.

Vigezo; Awe mwaminifu, aliye tayari kuchapakazi mzoefu wa biashara hii hasa kukaanga, awe anajua maeneo ambayo biashara yetu inaweza kufanya vizuri na hatimaye tukaitanua na kufungua frem zingine.

Asilimia 90 ya vifaa nimekwishanunua. Mpaka sasa nilichobaki ni kupata frem, kuilipia na pesa za kuanzia yaaani kununulia vitu, meza, viazi, Mafuta, kuku, samaki na vitu vidogovidogo. Aliye tayari tuwasiliane kwa namba 0655-535593
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…