Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Dar maeneo mengi biashara ya chips inalipa ila zaidi angalia sehemu ambapo wanawake ni wengi yani population ya wanawakr ni kubwa hapo utapiga pesa na laki 7 inatosha sana
 
Nahitaji kujua bei ya vitu vifuatavyo kwa nyakati hizi, kabati la kioo cha kuuzia chips cha wastani, gunia la viazi za chips, jiko la kukaangia chips la umeme, jiko la kukaangia chips la mkaa, gunia la mkaa, mafuta ya kupikia ndoo lita 20,
Asanteni
 
Kabati linaanzia 150,000 mpaka 200000.jiko la Mkaa 25,000 mpk 30000.Viazi inategemeana na msimu sasa ivi viko juu inaeza ikawa 100000 mpk 120000 .
 
Kwa wenye uzoefu, ukiajiri mtu inatakiwa uchukue kiasi gani per day? Or process nzima ya operation ipoje?
 
Kwa wenye uzoefu, ukiajiri mtu inatakiwa uchukue kiasi gani per day? Or process nzima ya operation ipoje?
kwa dar huwa wanalipwa on daily basis ..mara nyingi wanakuwa wawili au watatu.....kiongozi around 10,000 ,msaidizi 5,000
 
hahaahh kweli The Boss kuna watu wanaoenda kachumbari kuliko chips
yaa jumamosi nitakuwepo mara chache kuangalia biashara inavyokwenda

yaaa viazi vya kilimanjaro sio vizuri kwa chips vinanyonya maji sana hivyo hutumia mafuta mengi mpaka kukauka si unajua kilimanjaro ardhi yake ina maji vya mikoa mingine ndo vizur na pia kimi nikiviangalia kwa macho navijua vipi ni vipi......,nishalimaga sana
usafi wa dogo ni changamoto kubw sana si unajua ukidili na viazi plus mafuta plus moto

thanx nitakwambia mahala nipo one weekend uje na marafiki zako
Daah aisee na mimi ningeomba nialikwe nije kuchukua ujuzi, nina imani sijachelewa
 
Habarini wana-jf.

Nahitaji kufanya biashara ya chips ya kisasa hapa Dar, lakini nahitaji mtu wa kuungana naye ili tuunganishe akili na mitaji maana umoja ni nguvu.

Vigezo; Awe mwaminifu, aliye tayari kuchapakazi mzoefu wa biashara hii hasa kukaanga, awe anajua maeneo ambayo biashara yetu inaweza kufanya vizuri na hatimaye tukaitanua na kufungua frem zingine.

Asilimia 90 ya vifaa nimekwishanunua. Mpaka sasa nilichobaki ni kupata frem, kuilipia na pesa za kuanzia yaaani kununulia vitu, meza, viazi, Mafuta, kuku, samaki na vitu vidogovidogo. Aliye tayari tuwasiliane kwa namba 0655-535593
 
Back
Top Bottom