Wadau naomben mnisaidia nimefungua kasehem kwaajili ya kuuza chipsi na huu ndo mwanzo yaani naelekea kukata tamaa maana kila siku nakula loss na nilikuwa nimeweka mtu nakosa hata pesa ya kumlipa em nisaidieni nifanyeje ili niikuze hiyo biashara? Maana wateja nnao wapata niwachipsi kavu tu hasa hata faida ikija nikidogo au kwakuwa ndo mwanzo au nifanyeje ili nikuze biashara yangu.
Hii biashara ina changamoto sana mkuu!
But kwa experience yangu, niliwahi kuifanya kwa takribani miezi 8 hivi iko hivi..
1. Biashara ya chipsi huwezi ukaona faida kwa kuuza chipsi peke yake, hapo ni lazima uweke products zingine mfano. Mishikaki, ndizi, sausage, samaki, kuku, sambusa, kacholi...etc
2. Chipsi huwa zina hasara kwasababu ya upimaji wa chipsi kavu ni tofauti chipsi mayai hapo inabidi upate sahani zenye plain surface ( isiwe imeingia kwa ndani) pia lazima umbane muuzaje na Mara kwenye viazi mfano Mimi ndoo kubwa nilikua nanunua kwa elfu 15-17 nikiuza mpaka vikiisha napata Faida ya elfu 14-16 (hapo ni chipsi kavu tu nimepigia hesabu)
3. Weka kipimo ambacho hakimfurahishi mteja wala hakimfukuzi mteja ( pima kipimo ambacho ni average kwa kila sahani).
4. Kupunguza gharama usitumie mkaa Mwanzo mwisho unaweza tafuta jiko la maranda au Kuni mkaa tumia kwenye kukaangia chipsi mayai, kuchoma mishikaki, na kupashia chipsi.
Pia viazi nunua gunia kama mtaji unaruhusu, mafuta ya kukaangia nunua walau kindoo cha lita 10 na mayai kama trei tano, then piga kazi hapo utaona mabadiliko na faida utapata.
N.b kumbuka faida ya chipsi ni ngumu kuiona kwa sababu ina gharama nyingi za ziada mfano. Mkaa ( gas), mafuta, tomato, kachumbari, pilipili etc.