Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Mkuu naomba msaada. Hivi gharama za kutengeneza banda la kawaida tu yaani si local wala classic lipo kati inagharimu kiasi gani
Tayari mkuu

Mchanganuo wa biashara ni huu mkuu

Kwanza kabisa vifaa vyake muhimu

1: ile kabati ya kuhifazia chipsi inatakiwa iwe kubwa kiasi ngazi mbili au tatu itapendeza zaidi hapo kiasi ni 150k-250k

2:majiko mawili moja ya kuivishi chipsi nyingine ya kuchomea chipsi mayai mishikai N. K, hapo kila jiko itakost kuanzia 35k--45 kwa hiyo total pigia tu 90K,

3:vifaa vidogo vidogo kuna karai 10k--15k,sahani Dz 1 au 2 fanya 10K,koleo 3k,flampeni 2 5k, beseni dogo na kichujio chake kwa ndani 10K, vitu vidogo vidogo fanya 15K,

4:uje kwenye mazaga yenyewe.
Viazi gunia inategemeana na eneo ila bei kuanzia 45k--60,mafuta ya kula ndoo ndogo 30k,mkaa gunia moja inategemeana na eneo ila approximately ni 25k--40k,mayai tray 3 24K

Kwa kifupi kama hauna kifaa ata kimoja unatakiwa usiwe na chini ya 500k, na hapa ni kibanda tu cha kishkaji.

Faida zake,
Chipsi zina faida sana mkuu kama ukikaa location inayoeleweka inayoweza kumaliza kuanzia nusu gunia la viazi mpaka gunia moja na uwe na msimamizi imara huwezi kosa kuanzia 25k--45k kwa siku kama faida,

Hapo weka vyuku vyuku mishikaki,juice na N.k faida inakuwa mara dufu

Warning.
Usiwe na masihara ya kucheka na mademu, zingatia kipimo chako usisikie ya mteja anasema nini eti chipsi sishibi sijui chache mwambie aongeze hela umjazie.

Kuna kingine mkuu hapo ni kwa haraka haraka tu

CC Zero IQ
 
Mzee laki tano hapo inatumika pamoja na kulipa mafundi, mi nimejenga banda la kawaida tu bati tano, nguzo nne, na kuzungushia turubai imenitoka 500, hamna ujenzi mrahisi mzee nimeamini
Mkuu naomba msaada. Hivi gharama za kutengeneza banda la kawaida tu yaani si local wala classic lipo kati inagharimu kiasi gani
 
Hela haitoshi kwa classic chips,zile chips zinahitaji kwa haraka haraka deepfryer,showcase ambayo inakuwa na warmer ama uwe na microwave, unahitaji deepfreezer, most chips joint huwa wanazifroze chips na kuhifadhi katika deepfreezer na mteja anapokuja frozen chips ndo huwekwa kwenye deepfryer, hii ni kutaka mteja ale chips quality ambazo hazijapoa na chips ambazo zinakuwa frozen zikiwa fryed zinakuwa na quality nzuri kama za macdonald, juu zinakuwa na crisp,sio hizi chips za mitaani ukiishika mkononi inajikunja kama uume ambao haujasimama. Chips ikishikwa mkononi inatakiwa kuwa wima,na na inakuwa na rangi fulani hivi golden.
 
asante mkuu
mzee laki tano hapo inatumika pamoja na kulipa mafundi, mi nimejenga banda la kawaida tu bati tano, nguzo nne, na kuzungushia turubai imenitoka 500, hamna ujenzi mrahisi mzee nimeamini
 
mkuu wachana na huyo mleta uzi

mimi nataka ya kawaida yenye mazingira ya usafi isiwe local wala classic yaani iwe ya kati
Hela haitoshi kwa classic chips,zile chips zinahitaji kwa haraka haraka deepfryer,showcase ambayo inakuwa na warmer ama uwe na microwave,
unahitaji deepfreezer,most chips joint huwa wanazifroze chips na kuhifadhi katika deepfreezer na mteja anapokuja frozen chips ndo huwekwa kwenye deepfryer,hii ni kutaka mteja ale chips quality ambazo hazijapoa na chips ambazo zinakuwa frozen zikiwa fryed zinakuwa na quality nzuri kama za macdonald,juu zinakuwa na crisp,sio hizi chips za mitaani ukiishika mkononi inajikunja kama uume ambao haujasimama,
chips ikishikwa mkononi inatakiwa kuwa wima,na na inakuwa na rangi fulani hivi golden
 
Mchanganuo wa biashara ni huu

Kwanza kabisa vifaa vyake muhimu

1: ile kabati ya kuhifazia chipsi inatakiwa iwe kubwa kiasi ngazi mbili au tatu itapendeza zaidi hapo kiasi ni 150k-250k

2:majiko mawili moja ya kuivishi chipsi nyingine ya kuchomea chipsi mayai mishikai N. K, hapo kila jiko itakost kuanzia 35k--45 kwa hiyo total pigia tu 90K,

3:vifaa vidogo vidogo kuna karai 10k--15k,sahani Dz 1 au 2 fanya 10K,koleo 3k,flampeni 2 5k, beseni dogo na kichujio chake kwa ndani 10K, vitu vidogo vidogo fanya 15K,

4:uje kwenye mazaga yenyewe.
Viazi gunia inategemeana na eneo ila bei kuanzia 45k--60,mafuta ya kula ndoo ndogo 30k,mkaa gunia moja inategemeana na eneo ila approximately ni 25k--40k,mayai tray 3 24K

Kwa kifupi kama hauna kifaa ata kimoja unatakiwa usiwe na chini ya 500k, na hapa ni kibanda tu cha kishkaji.

Faida zake,
Chipsi zina faida sana mkuu kama ukikaa location inayoeleweka inayoweza kumaliza kuanzia nusu gunia la viazi mpaka gunia moja na uwe na msimamizi imara huwezi kosa kuanzia 25k--45k kwa siku kama faida,

Hapo weka vyuku vyuku mishikaki,juice na N.k faida inakuwa mara dufu

Warning.
Usiwe na masihara ya kucheka na mademu, zingatia kipimo chako usisikie ya mteja anasema nini eti chipsi sishibi sijui chache mwambie aongeze hela umjazie.

Kuna kingine mkuu hapo ni kwa haraka haraka tu

CC Zero IQ

Safiii
Hujaongezea banda gharama zake
 
Habari za asubuhi wadau wa JF.

Mimi ni kijana niliewekeza kwenye biashara ya chips hapa chuoni Mipango Mwanza. Kiukweli biashara ipo nzuri tu maana kwa siku nauza kilo 50 mpaka 55 za viazi, mishikaki ya ngombe kilo 2, na kuku 2 mpaka 3. Yaani gunia la viazi la kilo 100 linaisha ndani ya siku 2.

Shida ninayokumbana nayo ni namna ya kutenganisha faida na mtaji baada ya mauzo yote maana nikitoa matumizi naona kama sibaki na kitu mfuko wakati kila kitu kimeisha, na msimamizi ni mimi kwenye hiyo biashara.

Tafadhali wenye uzoefu wa biashara za namna hii nahitaji shule kutoka kwenu.
 
Pole sana dogo, inaonekana una matumizi makubwa kama gharama za uendeshaji. Au unakosea kati ya hivi vifuatavyo
1. Unahonga watoto wa kike chipsy
2. Unazidisha chenji
3. Unapima chipsy nyingi kuliko kipimo (no 2 na 3 ni sababu sababu kuu ya wateja kuwa wengi)
Angalia sana upunguze gharama za uendeshaji mfano acha kutumia mkaa, tumia majiko ya pumba yale yanapunguza sana gharama. Acha kuhonga, watoto wa chuo ni wapenzi sana wa chipsy hata kama una sura kama marehemu ongala utaitwa handsome tu
 
MZAWA JF,
Umenichekesha pia kwenye kuonga japo Simo.....sema gharama za uendeshaji ni kubwa kuanzia mafuta,mkaa,chachandu na nk....nawaza niamie kwenye gas labda
 
Saha
Designated Savaiva,
Sahani moja kama ni chips mayai ni tsh 2000,chips kavu ni tsh 1500.....wanachuo wanapenda sana chips kavu na iliyojaa sn,nimegundua ili eneo linanitia hasara pia
 
Habari za asubuhi wadau wa JF.

Mimi ni kijana niliewekeza kwenye biashara ya chips hapa chuoni Mipango Mwanza. Kiukweli biashara ipo nzuri tu maana kwa siku nauza kilo 50 mpaka 55 za viazi, mishikaki ya ngombe kilo 2, na kuku 2 mpaka 3. Yaani gunia la viazi la kilo 100 linaisha ndani ya siku 2.

Shida ninayokumbana nayo ni namna ya kutenganisha faida na mtaji baada ya mauzo yote maana nikitoa matumizi naona kama sibaki na kitu mfuko wakati kila kitu kimeisha, na msimamizi ni mimi kwenye hiyo biashara.

Tafadhali wenye uzoefu wa biashara za namna hii nahitaji shule kutoka kwenu.
Chuma ulete,hiyo hali iliwahi kunitokea
 
Back
Top Bottom