albab
JF-Expert Member
- Jul 6, 2018
- 1,198
- 2,562
Hodi wanajamvi....
Nianze kwa kutoa shukrani za dhati kwa jukwaa hili kwani naanza kukuona mwanga japo Kuna kigiza katika kuisimamisha biashara yangu ndogo..
Nianze kwa kutoa story fupi Kwanza..
Mimi Sina uzoefu katika kufanya biashara yoyote Ila nimekua na mawazo ya kuanzisha biashara na ndipo mwaka huu nikafanikiwa kuanzisha genge dogo kwa ajili ya chips ikiwa ni safari ya kuelekea kufungua Fresh Pub kwa ajili ya juice na maziwa tu hii ndio ndoto yangu kibiashara.
Basi nikapata kijana Analia shida sana kwani siku Kama 34 nyuma Tajirii yake aliyumba hivyo akawa Hana kazi tukapambana tukaanzisha biashara hiyo ya chips ambayo kwake yeye ni mzoefu wa muda mrefu na anajulikana sanaaa kwa Hilo eneo.
Sikutaka kumbana Kama kijana mwenzangu nkampa Uhuru na swali lilikua JE UTANIPA SHILINGI NGAPI KWA SIKU KWA UWEKEZAJI HUU...??
MAJIBU YAKE YAKAWA NI 25,000/- nikamuuliza unauhakika Hapo utapata pesa pia kuendesha maisha yako?? Akajibu NDIO pasi shaka... TUKAANZA KAZI Kama siku 20 nyuma.
Mwanzo ukawa nzuri hela ikaanza kuflow Kila siku sa tatu asubuhi anatuma Ila sasa siku Kama 6 nyuma Mambo yameanza kubadilika hela haiji kwa wakati... Kijana anasumbua Mara mi sipati chochote....
Mara wenzangu wananiloga Mambo mengiii na siku zingine hatumi chochote... Jamaa ni mshikaji Ila ananizingua...
Kwa ufupi kwa siku
Anauza kilo 30 za viazi
Mayai kati ya trei moja na nusu Hadi mbili
Nyama kilo tano
Samaki hapa inategemea na siku
Ndizi za kukaanga
Wajuzi nisaidieni hapa huyu mtu anaingiaza kiasi gani Ila ameshindwa kuzalisha 25k tu.
Leo nimegombana nae sanaaa nawaza kumtimua au la nimpelekee mtu wa mauzo na manunuzi abaki kuwa mkaangaji tu.
Wadau hebu nishaurini nini nikifanye kiukweli eneo Lina mzunguko mkubwa wa pesa na watu pia Ila huyu kiumbe ananikwamisha na mbaya zaidi huku Sina ndugu na Mimi muda wa kusimami sina