Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Hodi wanajamvi....
Nianze kwa kutoa shukrani za dhati kwa jukwaa hili kwani naanza kukuona mwanga japo Kuna kigiza katika kuisimamisha biashara yangu ndogo..
Nianze kwa kutoa story fupi Kwanza..

Mimi Sina uzoefu katika kufanya biashara yoyote Ila nimekua na mawazo ya kuanzisha biashara na ndipo mwaka huu nikafanikiwa kuanzisha genge dogo kwa ajili ya chips ikiwa ni safari ya kuelekea kufungua Fresh Pub kwa ajili ya juice na maziwa tu hii ndio ndoto yangu kibiashara.

Basi nikapata kijana Analia shida sana kwani siku Kama 34 nyuma Tajirii yake aliyumba hivyo akawa Hana kazi tukapambana tukaanzisha biashara hiyo ya chips ambayo kwake yeye ni mzoefu wa muda mrefu na anajulikana sanaaa kwa Hilo eneo.

Sikutaka kumbana Kama kijana mwenzangu nkampa Uhuru na swali lilikua JE UTANIPA SHILINGI NGAPI KWA SIKU KWA UWEKEZAJI HUU...??
MAJIBU YAKE YAKAWA NI 25,000/- nikamuuliza unauhakika Hapo utapata pesa pia kuendesha maisha yako?? Akajibu NDIO pasi shaka... TUKAANZA KAZI Kama siku 20 nyuma.

Mwanzo ukawa nzuri hela ikaanza kuflow Kila siku sa tatu asubuhi anatuma Ila sasa siku Kama 6 nyuma Mambo yameanza kubadilika hela haiji kwa wakati... Kijana anasumbua Mara mi sipati chochote....
Mara wenzangu wananiloga Mambo mengiii na siku zingine hatumi chochote... Jamaa ni mshikaji Ila ananizingua...

Kwa ufupi kwa siku
Anauza kilo 30 za viazi
Mayai kati ya trei moja na nusu Hadi mbili
Nyama kilo tano
Samaki hapa inategemea na siku
Ndizi za kukaanga

Wajuzi nisaidieni hapa huyu mtu anaingiaza kiasi gani Ila ameshindwa kuzalisha 25k tu.

Leo nimegombana nae sanaaa nawaza kumtimua au la nimpelekee mtu wa mauzo na manunuzi abaki kuwa mkaangaji tu.

Wadau hebu nishaurini nini nikifanye kiukweli eneo Lina mzunguko mkubwa wa pesa na watu pia Ila huyu kiumbe ananikwamisha na mbaya zaidi huku Sina ndugu na Mimi muda wa kusimami sina
 
Hilo nalo la kuomba ushauri? Fukuza haraka sana
 
Anaonekana yupo vizuri so Mpeleke mtu wa kukusanya pesa kama utawezaa...!! Maana ashaonesha pesa anaipataa tatizo sasa ukipigwa hela hapo utashindwa kujua ni mkusanya pesa au muuzaji labda upate mkusanya pesa ndugu yako hivii otherwise utaongeza Tatizo mkuu
 
Ushauri kidogo maana nishamaliza kujenga na bandaa na kuanza tu

Ushaur wa viungi
Kachunbari iweje
Viazi gani

Na mengneyo

Karbuni
 
msaada wa jiko la kutumia pumba waungwana hasa pumba za mpunga mkaa unantafuna vibaya sana... mazingira niliyopo hakuna haya majiko na mtengenezaji bado sijamuona... naomba kujua bei yake kwa DAR kama kuna uwezekano nilisafirishe.
lakini pia kama kuna maujanja ya ziada katika kupunguza gharama tusaidiane hapa ila kuongeza faida
 
kwa uzoefu wangu wa mwezi mmoja na nusu viazi vizuri ni vya ARUSHA
1) havitumii mafuta mengi
2)vina mvuto kwa kabati (vinang'aa) na si rahisi kuonesha kuungua
Bei ni kati ya tsh 80000-90000 kwa gunia. tsh 800/kg kwa mazingira niliyopo
Asante sana! Kamanda
 
Mkuu kuna majiko ya mkaa yanaundwa wanayafanyia modifications yanakuwa yanatumia umeme na mkaa

Yaani unachomeka waya kwenye socket na unaweka mkaa kidogo. Ni mazuri saan mkaa gunia unatumia mpaka unachoka mwenyewe

Nadhani haya yatakufaa zaidi kuliko hayo ya pumba
 

Hayo majiko yanapatikana wapi?
 
Mawasiliano itapendeza mkuuu au Kama utapata yanapopatikana
 
Wakuuu nimeingiliwa nikiwa naanza kusimama nakuuona mwanga Kuna mwamba alikua na kibanda Kama mita 30 kutoka nilipo mimi kafungua kingine nilipo Mimi tunatenganishwa na ndoo ya maji ya kunawa tu.... Huyu mwamba kaniumizaa vibaya mnooo na madhara nayaona waziwazi....

Nimfanyeje huyu bwana Mana najua hii ni strategy ya kunitoa relini.
 
Hizo ni changamoto za kawaida sana wewe ongeza ubora wa bidhaa zako na ujuzi usije anza kuleta uchawi uchawi badal ya kutumia akili

Hivi huwa huoni maduka kumi yapo sehemu moja afu yote yanauza bidhaa moja?
 
Hizo ni changamoto za kawaida sana wewe ongeza ubora wa bidhaa zako na ujuzi usije anza kuleta uchawi uchawi badal ya kutumia akili

Hivi huwa huoni maduka kumi yapo sehemu moja afu yote yanauza bidhaa moja?
Thanks brooo sanaaaa ssnaaaa
 
Simamia mwenyewe huyo wa kukusanya pesa pia atakupiga tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…