Ni biashara inayotegemea mambo mengi ili kufanikiwa. Kubwa ni wingi wa wateja. Chips kama chips zinategemea msimu. Kuna msimu gunia linauzwa 75,000. Na na kuna msimu 40,000. Faida utapata bei inaposhuka. Msimu wa 75,000 kitakachokupa faida nia vitu mbadala kama mayai, kuku n.k.
Kama nilivyosema hakuna faida kubwa kiasi kwamba anayetakiwa kufanya awe ndio mwendeshaji wa banda lenyewe. Sio biashara ya kuweka mfanyakazi. Mfano ukishawanunulia bidhaa chips, mayai, kuku, mafuta n.k. hata ungekaa hapo hapo wanakuibia usipokuwa mwangalifu. Ukiwaachia ndio kabisaa. Wanakunywa viroba. Jioni hela kiduchu.
Hata ungempa mtaji muuzaji akuletee kiasi maalumu kwa siku. Atamaliza mtaji bila kuleta tija yoyote.
Biashara ya chips inatakiwa kuendeshwa na mwenye mtaji mwenyewe sio kuachia watu. Utabaki na majiko tu.
Hapa nazunhumzia biashara ya maeneo ya kawaida Dar. Sio yanayouza sahani shs 5,000.