Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Habari wakuu,
Nna idea ya kuweka vijiwe vya chips kama vitatu hivi alafi niweke vijana wapige kazi kwa makubaliano ya kuniletea hesabu kwa siku.
Nauliza kwa wazoefu,kwa siku hesabu ni sh ngapi?Ili kijana naye abaki na ela ya kuendeshea biashara,kulipa eneo na ya kwenda nayo home ?
njoo pm tulonge
 
Mm nime wahi Fanya hii biashara ni moja kati ya biashara ambayo ina hitaji usimamizi wa Hall ya juu kama Mimi wewe umesema una Fanya kazi arafu una taka kufungua biashara hii siku katishi tamaa ila kiukweli utalia na kusaga meno asilimia kubwa ya vijana hawa jitambui andika maumivu una kuta mahitaji yame kwisha arafu hela hakuna stori kibao . ukihitaji vitu kama kabati na jiko la pumba njoo nikuuzie nishaachana na hii biashara kichaa.. Ina hitaji usimamizi wa Hall ya juu
 
Ngoja tuone itavokua
 
Mkuu nakubali mtalamu sana nitakufuta nipete vifaa
Mchanganuo wa biashara ni huu mkuu

Kwanza kabisa vifaa vyake muhimu

1: ile kabati ya kuhifazia chipsi inatakiwa iwe kubwa kiasi ngazi mbili au tatu itapendeza zaidi hapo kiasi ni 150k-250k

2:majiko mawili moja ya kuivishi chipsi nyingine ya kuchomea chipsi mayai mishikai N. K, hapo kila jiko itakost kuanzia 35k--45 kwa hiyo total pigia tu 90K,

3:vifaa vidogo vidogo kuna karai 10k--15k,sahani Dz 1 au 2 fanya 10K,koleo 3k,flampeni 2 5k, beseni dogo na kichujio chake kwa ndani 10K, vitu vidogo vidogo fanya 15K,

4:uje kwenye mazaga yenyewe.
Viazi gunia inategemeana na eneo ila bei kuanzia 45k--60,mafuta ya kula ndoo ndogo 30k,mkaa gunia moja inategemeana na eneo ila approximately ni 25k--40k,mayai tray 3 24K

Kwa kifupi kama hauna kifaa ata kimoja unatakiwa usiwe na chini ya 500k, na hapa ni kibanda tu cha kishkaji.

Faida zake,
Chipsi zina faida sana mkuu kama ukikaa location inayoeleweka inayoweza kumaliza kuanzia nusu gunia la viazi mpaka gunia moja na uwe na msimamizi imara huwezi kosa kuanzia 25k--45k kwa siku kama faida,

Hapo weka vyuku vyuku mishikaki,juice na N.k faida inakuwa mara dufu

Warning.
Usiwe na masihara ya kucheka na mademu, zingatia kipimo chako usisikie ya mteja anasema nini eti chipsi sishibi sijui chache mwambie aongeze hela umjazie.

Kuna kingine mkuu hapo ni kwa haraka haraka tu

CC Zero IQ
 
Nina mtaji wa laki 3 na nusu, wakati natafuta ajira nimeona nijiajiri niuze chips, vipi mtaji unatosha? Any idea ya how to make them in a way it suits me (kisomi)?

Ushauri wenu unahitajika.

--------------------------------------------------------------------------------------------------------
Maswali kutoka kwa wadau wengine kuhusu biashara hii

================================================
Michango ya wadau kuhusu mchanganuo wa biashara hii
================================================

Ushauri mzuri ukipata sehemu ambayo unaweza kuuza viazi kwa debe kwa siku mbona utafurahi maishani kaza mwendo kamanda kazi inalipa sana hiyo.
Mfano: kwa siku unauza kilo 20 za viazi, trei moja ya mayai, na nyama kilo moja kwa uzoefu wako faida hapo haikosekani km shilingi ngap?
 
Nina mtaji wa laki 3 na nusu, wakati natafuta ajira nimeona nijiajiri niuze chips, vipi mtaji unatosha? Any idea ya how to make them in a way it suits me (kisomi)?

Ushauri wenu unahitajika.

--------------------------------------------------------------------------------------------------------
Maswali kutoka kwa wadau wengine kuhusu biashara hii

================================================
Michango ya wadau kuhusu mchanganuo wa biashara hii
================================================

Inatosha kabisa Ila zingatia location
 
Wakuu hivii unapomiliki banda la chipsi na kuuza msosi ni lazima uwe na leseni??
 
Habari wakuu,

Hatimaye nimepata wazo la kufanya na hii milioni 1 yangu.

Ni hivi nimejitokeza kuomba mwongozo wa nini mambo ya muhimu niweze kuanzisha biashara ya chipsi kwa kuwa na banda classic, vifaa na chipsi classic pia yaani ziwe za viwango vya juu na kuwavutia wateja wanaopenda chips bora na katika mazingira bora

Eneo ninalopanga kuanzjsha si kwamba hawauzi chipsi, vibanda vipo lakini si vya viwango vya juu katika utengenezaji na uusaji wa chipsi hivyo njia ya kuwin ni mimi kuwa na huduma nzuri na bora zaidi yao kwa bei ya kuuza kama wao

Wakuu ni vifaa gani vinahitajika kuweza kuwa na bishara hii kwani sina ujuzi nayo, vipi faida ikoje, changamoto zake ni zipi?

Je, milion 1 inatosha kuwa na banda la chips la viwango vya juu kabisa?

Nawasilisha
 
Kama upo Dar es salaam, hiyo pesa ni changamoto kwako labda kama unalenga ufanye hiyo biashara ndani ndani au tayari una eneo! Kwa eneo zuri, hiyo ni pesa ya kulipia eneo tu! Kwa maeneo ya afadhali kidogo, huwezi kupata kwa chini ya 100K kwa mwezi, na kwa ya afadhali zaidi, kodi inafika hadi 200K kwa mwezi!

Sasa ndo hapo tena, mtu anakuambia kodi miezi 6!

Na kama eneo lenyewe ni baraza ya mtu, basi ni ungese mtupu labda mtu mwenyewe asiwe wa kuendekeza njaa! Kupaanzisha unapaanzisha wewe, lakini baadae pakichanganya, basi anza kupiga hesabu zimebaki wiki ngapi kutimuliwa kwa mbinu yoyote! Ukitimuliwa leo J4, rudi Jmosi utakuta mtoto wa dadake na yeye anauza chips! Unabaki kujiuliza "kwani hili eneo walikuwa hawalioni?"
 
Back
Top Bottom