Biashara ya Chips

SamuraiJack

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2017
Posts
225
Reaction score
239
Poleni na majukumu wana JF wenzangu,

Nina kijana mchapakazi na ninayemfahamu vizuri na kumuheshimu, Nina wazo la kufungua kijiwe cha chipsi niweke kila kitu cha kisasa kama vile jiko la umeme na gesi na vifaa vyote vya kuwezesha kazi pamoja na mtaji wa kununulia mazaga kwa ajili ya biashara.

Lengo langu ni kumkabidhi kijana huyu kwa makubaliano kwamba kila siku awe ananikabidhi mimi 20,000/= tu. Nafanya hivyo kwa sababu siwezi kupata muda wa siku nzima kuwepo eneo la biashara.

Kwa wazoefu wa biashara hii, Je? jambo hili litawezekana na kama litawezekena, ni changamoto gani ambazo ni common kwenye hii biashara?

NB: Eneo nimeshapata na lipo eneo la chuo ndani ya jiji la DSM.
 
biashara ya chipsi ina faida kubwa sana,lakini kijana ajitahidi kuwa msafi,usafi wa mazingira ya biashara kwa ujumla,na awe mbunifu katika huduma.
 
Sijaelewa Yani unampa Kila kitu,,Yani Hadi mafuta ya kula ,chumvi, tomato's,pilili na mazaga yote alafu akufungie hesabu la 20,000 per day
 
Kwahiyo inawezekana akaifanya bila mimi kuwepo muda wote na je hicho kiwango atakachokuwa ananipa kwa siku ni sawa? maana binafsi sina experience yoyote ya hii biashara zaidi ya research.
 
Sijaelewa Yani unampa Kila kitu,,Yani Hadi mafuta ya kula ,chumvi, tomato's,pilili na mazaga yote alafu akufungie hesabu la 20,000 per day
I mean nikishampa hiyo starting capital natarajia kuanzia hapo atasimamia kila kitu mwenyewe, mimi nitakuwa tu ninahitaji hesabu ya 20,000/- per day!
 
I mean nikishampa hiyo starting capital natarajia kuanzia hapo atasimamia kila kitu mwenyewe, mimi nitakuwa tu ninahitaji hesabu ya 20,000/- per day!
Jumla ya starting capital ni kiasi gani tuanzie hapo kwaza
 
Vipi kwa upande wangu nitakuwa nimeumia au nitakuwa ninamnyonya dogo?
Inategemea na wingi au uchache wa wateja, km ni sehemu yenye biashara dogo ataneemeka kulilo ww ila km mzunguko mdogo unaeza mnyonya dogo, btw ungetafuta muda ht kwa siku 2 au 3 unakaa hapo kuanzia mchana hadi usiku ili ujue hali ya biashara
 
Sawa mkuu nashukuru kwa ushauri mzuri nitaufanyia kazi.
 
Ni vizuri ukitaka ushauri wa kuvua samaki uende direct kwa wavuvi, vile vile katika biz ya kiepe nenda direct kwa wauzaji. Tengeneza urafiki wa apa na pale jua changamoto na faida za biashara.

Ukifungua kijiwe angalau kaa hapo kila weekend uone mzunguko hii itakua rahisi kujua kama dogo amekukaba au umemkaba.
 
Kwahiyo in 40 days mtaji uliowekeza unakuwa umerudi? Ukizingatia unaenda kuanza kuna muda ajenge soko watu wamfahamu etc . Fanya tathimini ya hiyo biashara kwa wengine. usije ukawa unambana Sana. Mwisho WA siku akapiga chini. Wewe ukabaki na vyombo.
 
Wazo zuri pia # noted
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…