Valar Morghulis
Member
- Mar 31, 2022
- 22
- 42
Mambo vipi wadau, huu mchongo hapa chini naona unasambaa sana kwenye mitandao ya kijamii nikaona niulete humu tuujadili kama una uhalisia wowote, karibuni kwa maoni.
*************************
Kwa majina naitwa Steve Mtundu. Nimfanyabiashara wa spea za magari lkn pia nafanya biashara ya makopo ya plastiki na machupa ya maji.
Leo nimeona nikupe huu mchongo uwashirikishe wadau ikikupendeza, uhenda kuna mtu akatoboa kupitia mchongo huu wakukusanya makopo ya plastiki.
Kamwe tusiwe na roho mbaya za kuficha njia zetu zamafanikio. Tuwashirikishe wenzetu na wao wapige hatua uhenda kupitia mafanikio yao siku moja jamii yako ikanufaika.
Mimi nimefanikiwa kufika hapa nilipo ni kwavile nilikutana na watu waliofanikiwa wakanishika mkono wakanionyesha njia na mimi nikafanikiwa.
Sijawahi kuwa mchoyo ktk kuwapa rafiki zangu michongo ya kimaisha.
Kwanza kabisa tukumbuke hakuna biashara yeyote isiyokua na changamoto. Biashara yeyote ina faida na hasara zake. Hii biashara ya chupa sikuanza tu leo na kesho nikaona faida, ilininichukua muda kidogo kuanza kuingiza faida.
Sasa tuanze kuichanganua.
Unaweza kuanza hii biashara kwa msingi hata laki mbili. Utaanzaje na laki mbili?
Kwanza kabisa wewe utakua unanunua kwa wale waokotaji wamtaani watakuuzia sh 200 mpk 250 kwa kilo.
Sasa kama unayo laki mbili utanunua mzani wakupimia sh.10,000 itabaki laki tisini. Ukinunua mzigo wote wa 190,0000 nisawa na kilo 750. Ukinunua kilo hizo wewe unaenda kwa mchina unamwambia nina mzigo wachupa anakupa gari unakuja unapakia unaenda kumuuzia kilo moja sh.400 mpk 450.
Kwahiyo utauza 400×750=300,000
ukishauza mzigo wako laki tatu utatoa pesa yakununulia mzigo ambay ni 250×750=187, 500 utabakiwa na 112,000.
ukitoa ya mzani sh 10,000 unabakiwa na faida 100,000.
Kwahyo ukiwa na mtaji wowote ule unaweza kuanza hii biashara kinachotakiwa nikupambana tu.
Haya kwa wale wenye mtaji mkubwa kama mimi unatakiwa uwe na mashine yakusaga plastiki. Uwe na eneo kubwa wastan wa viwanja viwili vya miguu ishirini kwa ishirini.
Uwe angalau kiwanda kipo mita ishirini na majirani. Uwe na kibali cha mazingira unapewa na manispaa. Uwe na wafanyakazi watatu, na vibarua kama watano.
Baada ya hapo sasa, unaanza kununua mzigo kutoka kwa muokotaji anayeuza 250 na huyo mkusanyaji hapo juu anayeuza 400 wote unanunua wewe unajaza stoo kwa muda wamiezi mitatu.
Mzigo ukishafikisha tani 30, unawapa vibarua kazi yakutoa vifuniko vya chupa pamoja na lebo nakuchambua chupa za energy hutakiwi kuzichanganya. Ukishazichambua vzr ndiyo unaanza kusaga sasa.
Hapo kila siku utasaga tani 3 kwahyo Tani 30 utasaga siku 10.
Mzigo ukishakamilika wafanyakazi wanajaza kwenye magunia, halafu ukimaliza unapima tena ukiwa umeshasaga unaandika kilo zako za mzigo wote. Ukimaliza kama upo mkoani unatafuta Lori unapakia mzigo wako unaleta kwa mchina.
Ukifika kwa mchina chupa iliyosagwa ananunua sh.950 kwa kilo.kwahyo
950×30=28,500,000ml.
toa manunuzi
400×30=12,000,000ml.
toa usafiri
1,500,000.
toa mishahara ya wafanya kazi 3,600,000
toa malipo ya vibarua
500,000.
toa pesa ya mashine
8,000,000.
toa pesa ya umeme
500,000.
toa pesa ya mifuko
200,000.
Kwahyo mwisho wamahesabu kuanzia manunuzi mpk mzigo unafika kwa mchina umetumia 26,300,000 ml.
kumbuka tulipouza tulipata 28ml na laki tano. 28,500,000–26,300,000=2,200,000.
Hii 2.2ml ndiyo faida yako kwa miezi mitatu ya mwanzo. Miezi mitatu ijayo gharama zote zitakuwepo isipokua ya mashine kwahyo mieizi mitatu ijayo utapata faida milion 10 ktk hiyo Tani 30.
Kwahyo hii biashara wewe itaanza kukulipa baada yamauzo ya pili.. mauzo ya kwanza utarudisha gharama za mashine ambazo ndizo gharama kubwa mauzo ya pili utaanza kula mema ya nchi".