Biashara ya chupa za plastiki

Biashara ya chupa za plastiki

Joined
Mar 31, 2022
Posts
22
Reaction score
42
Mambo vipi wadau, huu mchongo hapa chini naona unasambaa sana kwenye mitandao ya kijamii nikaona niulete humu tuujadili kama una uhalisia wowote, karibuni kwa maoni.

*************************
Kwa majina naitwa Steve Mtundu. Nimfanyabiashara wa spea za magari lkn pia nafanya biashara ya makopo ya plastiki na machupa ya maji.

Leo nimeona nikupe huu mchongo uwashirikishe wadau ikikupendeza, uhenda kuna mtu akatoboa kupitia mchongo huu wakukusanya makopo ya plastiki.

Kamwe tusiwe na roho mbaya za kuficha njia zetu zamafanikio. Tuwashirikishe wenzetu na wao wapige hatua uhenda kupitia mafanikio yao siku moja jamii yako ikanufaika.

Mimi nimefanikiwa kufika hapa nilipo ni kwavile nilikutana na watu waliofanikiwa wakanishika mkono wakanionyesha njia na mimi nikafanikiwa.

Sijawahi kuwa mchoyo ktk kuwapa rafiki zangu michongo ya kimaisha.

Kwanza kabisa tukumbuke hakuna biashara yeyote isiyokua na changamoto. Biashara yeyote ina faida na hasara zake. Hii biashara ya chupa sikuanza tu leo na kesho nikaona faida, ilininichukua muda kidogo kuanza kuingiza faida.

Sasa tuanze kuichanganua.

Unaweza kuanza hii biashara kwa msingi hata laki mbili. Utaanzaje na laki mbili?

Kwanza kabisa wewe utakua unanunua kwa wale waokotaji wamtaani watakuuzia sh 200 mpk 250 kwa kilo.

Sasa kama unayo laki mbili utanunua mzani wakupimia sh.10,000 itabaki laki tisini. Ukinunua mzigo wote wa 190,0000 nisawa na kilo 750. Ukinunua kilo hizo wewe unaenda kwa mchina unamwambia nina mzigo wachupa anakupa gari unakuja unapakia unaenda kumuuzia kilo moja sh.400 mpk 450.

Kwahiyo utauza 400×750=300,000
ukishauza mzigo wako laki tatu utatoa pesa yakununulia mzigo ambay ni 250×750=187, 500 utabakiwa na 112,000.
ukitoa ya mzani sh 10,000 unabakiwa na faida 100,000.

Kwahyo ukiwa na mtaji wowote ule unaweza kuanza hii biashara kinachotakiwa nikupambana tu.

Haya kwa wale wenye mtaji mkubwa kama mimi unatakiwa uwe na mashine yakusaga plastiki. Uwe na eneo kubwa wastan wa viwanja viwili vya miguu ishirini kwa ishirini.

Uwe angalau kiwanda kipo mita ishirini na majirani. Uwe na kibali cha mazingira unapewa na manispaa. Uwe na wafanyakazi watatu, na vibarua kama watano.

Baada ya hapo sasa, unaanza kununua mzigo kutoka kwa muokotaji anayeuza 250 na huyo mkusanyaji hapo juu anayeuza 400 wote unanunua wewe unajaza stoo kwa muda wamiezi mitatu.

Mzigo ukishafikisha tani 30, unawapa vibarua kazi yakutoa vifuniko vya chupa pamoja na lebo nakuchambua chupa za energy hutakiwi kuzichanganya. Ukishazichambua vzr ndiyo unaanza kusaga sasa.

Hapo kila siku utasaga tani 3 kwahyo Tani 30 utasaga siku 10.

Mzigo ukishakamilika wafanyakazi wanajaza kwenye magunia, halafu ukimaliza unapima tena ukiwa umeshasaga unaandika kilo zako za mzigo wote. Ukimaliza kama upo mkoani unatafuta Lori unapakia mzigo wako unaleta kwa mchina.

Ukifika kwa mchina chupa iliyosagwa ananunua sh.950 kwa kilo.kwahyo
950×30=28,500,000ml.
toa manunuzi
400×30=12,000,000ml.
toa usafiri
1,500,000.
toa mishahara ya wafanya kazi 3,600,000
toa malipo ya vibarua
500,000.
toa pesa ya mashine
8,000,000.
toa pesa ya umeme
500,000.
toa pesa ya mifuko
200,000.

Kwahyo mwisho wamahesabu kuanzia manunuzi mpk mzigo unafika kwa mchina umetumia 26,300,000 ml.
kumbuka tulipouza tulipata 28ml na laki tano. 28,500,000–26,300,000=2,200,000.

Hii 2.2ml ndiyo faida yako kwa miezi mitatu ya mwanzo. Miezi mitatu ijayo gharama zote zitakuwepo isipokua ya mashine kwahyo mieizi mitatu ijayo utapata faida milion 10 ktk hiyo Tani 30.

Kwahyo hii biashara wewe itaanza kukulipa baada yamauzo ya pili.. mauzo ya kwanza utarudisha gharama za mashine ambazo ndizo gharama kubwa mauzo ya pili utaanza kula mema ya nchi".
 
Good idea,ila kama wewe umeshafikia level hiyo hebu fikiria pia kuhusu soko la nje,kuna muhindi namkamilishia project yake kwa ku muundia bale pressing machines na ku zi install kwenye truck,yeye ananunua mzigo wa chupa mikoa mingi,mzigo ukishakuwa mkubwa kwenye kituo A lile truck lenye pressing machines linaenda,linabana kisha lorry jingine linasafirisha kwenda bandarini,muhindi anasema mzigo wake anauza UK kwa bei nzuri mno.
 
Mambo vipi wadau, huu mchongo hapa chini naona unasambaa sana kwenye mitandao ya kijamii nikaona niulete humu tuujadili kama una uhalisia wowote, karibuni kwa maoni.

*************************
Kwa majina naitwa Steve Mtundu. Nimfanyabiashara wa spea za magari lkn pia nafanya biashara ya makopo ya plastiki na machupa ya maji.

Leo nimeona nikupe huu mchongo uwashirikishe wadau ikikupendeza, uhenda kuna mtu akatoboa kupitia mchongo huu wakukusanya makopo ya plastiki.

Kamwe tusiwe na roho mbaya za kuficha njia zetu zamafanikio. Tuwashirikishe wenzetu na wao wapige hatua uhenda kupitia mafanikio yao siku moja jamii yako ikanufaika.

Mimi nimefanikiwa kufika hapa nilipo ni kwavile nilikutana na watu waliofanikiwa wakanishika mkono wakanionyesha njia na mimi nikafanikiwa.

Sijawahi kuwa mchoyo ktk kuwapa rafiki zangu michongo ya kimaisha.

Kwanza kabisa tukumbuke hakuna biashara yeyote isiyokua na changamoto. Biashara yeyote ina faida na hasara zake. Hii biashara ya chupa sikuanza tu leo na kesho nikaona faida, ilininichukua muda kidogo kuanza kuingiza faida.

Sasa tuanze kuichanganua.

Unaweza kuanza hii biashara kwa msingi hata laki mbili. Utaanzaje na laki mbili??.

Kwanza kabisa wewe utakua unanunua kwa wale waokotaji wamtaani watakuuzia sh .200 mpk 250 kwa kilo.

Sasa kama unayo laki mbili utanunua mzani wakupimia sh.10,000 itabaki laki tisini. Ukinunua mzigo wote wa 190,0000 nisawa na kilo 750. Ukinunua kilo hizo wewe unaenda kwa mchina unamwambia nina mzigo wachupa anakupa gari unakuja unapakia unaenda kumuuzia kilo moja sh.400 mpk 450.

Kwahiyo utauza 400×750=300,000
ukishauza mzigo wako laki tatu utatoa pesa yakununulia mzigo ambay ni 250×750=187,500
utabakiwa na 112,000.
ukitoa ya mzani sh 10,000 unabakiwa na faida 100,000.

Kwahyo ukiwa na mtaji wowote ule unaweza kuanza hii biashara kinachotakiwa nikupambana tu.

Haya kwa wale wenye mtaji mkubwa kama mimi... unatakiwa uwe na
mashine yakusaga plastiki.
uwe na eneo kubwa wastan wa viwanja viwili vya miguu ishirini kwa ishirini.

Uwe angalau kiwanda kipo mita ishirini na majirani.
uwe na kibali cha mazingira unapewa na manispaa
uwe na wafanyakazi watatu, na vibarua kama watano.

kumbuka tulipouza tulipata 28ml na laki tano.
28,500,000–26,300,000=2,200,000.

hakika wewe ni mtu mwema, natumaini kuna watu watalifanyia kazi hili wazo......
 
Mchina ananunua mzigo wote? Maana taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa ni kiasi kidogo tu cha plastic kinachokuwa recycled.
 
Good idea,ila kama wewe umeshafikia level hiyo hebu fikiria pia kuhusu soko la nje,kuna muhindi namkamilishia project yake kwa ku muundia bale pressing machines na ku zi install kwenye truck,yeye ananunua mzigo wa chupa mikoa mingi,mzigo ukishakuwa mkubwa kwenye kituo A lile truck lenye pressing machines linaenda,linabana kisha lorry jingine linasafirisha kwenda bandarini,muhindi anasema mzigo wake anauza UK kwa bei nzuri mno.
Imekaa poa sana hii mkuu, nadhani wadau wanaweza ku-compare bei ya mchina na huyo mhindi kuona unafuu uko wapi
 
Mchina ananunua mzigo wote? Maana taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa ni kiasi kidogo tu cha plastic kinachokuwa recycled.
Huyu mchina wanasema ana magodown sehemu mbalimbali mfano kigamboni, makumbusho, tegeta nk so nadhani kiwango cha plastic anachochukua kitakuwa kikubwa. Hizo taarifa zako ni kutoka kiwandani au wapi?
 
Mambo vipi wadau, huu mchongo hapa chini naona unasambaa sana kwenye mitandao ya kijamii nikaona niulete humu tuujadili kama una uhalisia wowote, karibuni kwa maoni.

*************************
Kwa majina naitwa Steve Mtundu. Nimfanyabiashara wa spea za magari lkn pia nafanya biashara ya makopo ya plastiki na machupa ya maji.

Leo nimeona nikupe huu mchongo uwashirikishe wadau ikikupendeza, uhenda kuna mtu akatoboa kupitia mchongo huu wakukusanya makopo ya plastiki.

Kamwe tusiwe na roho mbaya za kuficha njia zetu zamafanikio. Tuwashirikishe wenzetu na wao wapige hatua uhenda kupitia mafanikio yao siku moja jamii yako ikanufaika.

Mimi nimefanikiwa kufika hapa nilipo ni kwavile nilikutana na watu waliofanikiwa wakanishika mkono wakanionyesha njia na mimi nikafanikiwa.

Sijawahi kuwa mchoyo ktk kuwapa rafiki zangu michongo ya kimaisha.

Kwanza kabisa tukumbuke hakuna biashara yeyote isiyokua na changamoto. Biashara yeyote ina faida na hasara zake. Hii biashara ya chupa sikuanza tu leo na kesho nikaona faida, ilininichukua muda kidogo kuanza kuingiza faida.

Sasa tuanze kuichanganua.

Unaweza kuanza hii biashara kwa msingi hata laki mbili. Utaanzaje na laki mbili??.

Kwanza kabisa wewe utakua unanunua kwa wale waokotaji wamtaani watakuuzia sh .200 mpk 250 kwa kilo.

Sasa kama unayo laki mbili utanunua mzani wakupimia sh.10,000 itabaki laki tisini. Ukinunua mzigo wote wa 190,0000 nisawa na kilo 750. Ukinunua kilo hizo wewe unaenda kwa mchina unamwambia nina mzigo wachupa anakupa gari unakuja unapakia unaenda kumuuzia kilo moja sh.400 mpk 450.

Kwahiyo utauza 400×750=300,000
ukishauza mzigo wako laki tatu utatoa pesa yakununulia mzigo ambay ni 250×750=187,500
utabakiwa na 112,000.
ukitoa ya mzani sh 10,000 unabakiwa na faida 100,000.

Kwahyo ukiwa na mtaji wowote ule unaweza kuanza hii biashara kinachotakiwa nikupambana tu.

Haya kwa wale wenye mtaji mkubwa kama mimi... unatakiwa uwe na
mashine yakusaga plastiki.
uwe na eneo kubwa wastan wa viwanja viwili vya miguu ishirini kwa ishirini.

Uwe angalau kiwanda kipo mita ishirini na majirani.
uwe na kibali cha mazingira unapewa na manispaa
uwe na wafanyakazi watatu, na vibarua kama watano.

Baada ya hapo sasa, unaanza kununua mzigo kutoka kwa muokotaji anayeuza 250 na huyo mkusanyaji hapo juu anayeuza 400 wote unanunua wewe unajaza stoo kwa muda wamiezi mitatu.

Mzigo ukishafikisha tani 30, unawapa vibarua kazi yakutoa vifuniko vya chupa pamoja na lebo nakuchambua chupa za energy hutakiwi kuzichanganya. Ukishazichambua vzr ndiyo unaanza kusaga sasa.

Hapo kila siku utasaga tani 3 kwahyo Tani 30 utasaga siku 10.

Mzigo ukishakamilika wafanyakazi wanajaza kwenye magunia, halafu ukimaliza unapima tena ukiwa umeshasaga unaandika kilo zako za mzigo wote. Ukimaliza kama upo mkoani unatafuta Lori unapakia mzigo wako unaleta kwa mchina.

Ukifika kwa mchina chupa iliyosagwa ananunua sh.950 kwa kilo.kwahyo
950×30=28,500,000ml.
toa manunuzi
400×30=12,000,000ml.
toa usafiri
1,500,000.
toa mishahara ya wafanya kazi 3,600,000
toa malipo ya vibarua
500,000.
toa pesa ya mashine
8,000,000.
toa pesa ya umeme
500,000.
toa pesa ya mifuko
200,000.

Kwahyo mwisho wamahesabu kuanzia manunuzi mpk mzigo unafika kwa mchina umetumia 26,300,000 ml.
kumbuka tulipouza tulipata 28ml na laki tano.
28,500,000–26,300,000=2,200,000.

Hii 2.2ml ndiyo faida yako kwa miezi mitatu ya mwanzo. Miezi mitatu ijayo gharama zote zitakuwepo isipokua ya mashine kwahyo mieizi mitatu ijayo utapata faida milion 10 ktk hiyo Tani 30.

Kwahyo hii biashara wewe itaanza kukulipa baada yamauzo ya pili.. mauzo ya kwanza utarudisha gharama za mashine ambazo ndizo gharama kubwa mauzo ya pili utaanza kula mema ya nchi".
Vipi ukiwa mikoa kama mbeya, njombe una mzigo tayari je mchina atakuja pia ?
 
Huyu mchina wanasema ana magodown sehemu mbalimbali mfano kigamboni, makumbusho, tegeta nk so nadhani kiwango cha plastic anachochukua kitakuwa kikubwa. Hizo taarifa zako ni kutoka kiwandani au wapi?
Tunaomba basi uende hatua moja mbele. Maana umechagua kutuletea huu mchongo.

Tupe anuani kamili ya huyo Mchina. Na kama huna, basi unaweza ukatuelekeza "Tegeta sehemu gani, Makumbusho sehemu gani, na huko Kigamboni anapatikana eneo gani! Maana wengine tuko Mikoani huku.

Naomba kuwasilisha✍️
 
Mkuu si kwa ubaya. Ungetoa credit pia kwa dj tee wa pale twita kwa huu uzi.

Yaani ni biashara nzuri ila uzito ni kwamba binadamu wengi hatuwezi himili hasara au uvumilivu wa kupata hasara tukingoja faida.

Yeye hapo pia alifanya iyo biashara kwa kuongozwa na watu waliamua kufanikiwa pamoja nae. Na ugumu ndio huko hapa kupata mtu wa kukuongoza kwenye fursa.
 
Naomba kuwasilisha[emoji3578]

Habari katoa Twitter ni ngumu kukujibia ili swali.
 
Wazo la kwanza nimekubali, lakini la pili hapana. Yaani Unawekeza mtaji mkubwa sana hapo halafu faida million mbili tu halafu unaipata kwa mizi mitatu.
 
Tunaomba basi uende hatua moja mbele. Maana umechagua kutuletea huu mchongo.

Tupe anuani kamili ya huyo Mchina. Na kama huna, basi unaweza ukatuelekeza "Tegeta sehemu gani, Makumbusho sehemu gani, na huko Kigamboni anapatikana eneo gani! Maana wengine tuko Mikoani huku.

Naomba kuwasilisha[emoji3578]
Mkuu kama nilivyosema hapo juu hili andiko sio langu ila nikizipata namba za mwandishi au huyo mchina nitawawekea hapa
 
Mkuu si kwa ubaya. Ungetoa credit pia kwa dj tee wa pale twita kwa huu uzi.

Yaani ni biashara nzuri ila uzito ni kwamba binadamu wengi hatuwezi himili hasara au uvumilivu wa kupata hasara tukingoja faida.

Yeye hapo pia alifanya iyo biashara kwa kuongozwa na watu waliamua kufanikiwa pamoja nae. Na ugumu ndio huko hapa kupata mtu wa kukuongoza kwenye fursa.
Mimi nimelitoa fb kwenye page fulani hv mkuu, inaonekana amepost sehemu mbalimbali
 
Msije kuniuliza maswali.
Mie nimecopy huko nimeileta.

"admin naomba nijibu maswali yaliyoulizwa Sana kupitia coment kuhusu hii biashara ya makopo ya plastiki🙏.

swali la kwanza:
mashine zinauzwa wapi? nazinauzwa Bei gani??

jibu:✍️
mashine zinauzwa kwa wachina,au unaweza kuweka oda Sido wakakutengenezea.bei yamashine ya size ya Kati inaanzia 5ml,6ml, mashine kubwa 8ml,na 12ml.✍️
swali la pili.
wachina wanaonunua haya makopo wanapatikana wap??
jibu: ✍️
wachina wanaonunua haya makopo wanapatikana dar maeneo ya kigamboni kibada,kisemvule pwani,vikindu,tegeta,mwenge itv,mbezi makonde nak...✍️

swali la tatu:
umesema chupa za energy na Malta hazichanganywi je wachina nikwamba hawazinunui??

jibu:✍️
chupa za energy na zile na Malta rangi zake nitofauti kabisa nachupa zamaji na juice.kwahyo za eneg pamoja namalta zikusnye peke yake,Bei yake nichini kuliko hiz zamaji na juice.ukichanganya bila kuzichagua mchina atanunua mzigo wako kwa Bei ya chini na utapata hasara kubwa.✍️

swali la nne:
ni chupa zajuice na maji pekee ndiyo wananunua wachina au niplastiki aina zote??

jibu✍️
mchina ananunua chupa aina zote,plastik aina zote,mifuko ya nailon kama ile inazungushiwa ktk katon ya maji au juice,ananunua pia mifuko ya sanadarusi,ananunua viti vya plastiki,bakuli,vikombe,na kila kitu Cha plastiki.
unachotakiwa kufanya nikutenganisha aina ya plastik Ili ukifika sokon mzigo wako usilete shida.
mfano chupa zamaji aina zote pmaoja na zile za juice aina zote kusanya pamoja.
chupa za energy pamoja na zile za malita kusanya pamoja.
plastiki aina ya ndoo,viti,bakuli,vikombe,jjag,chupa ya chai,besen,Bomba zamaji,hizi pia kusanya pamoja.
plastiki aina ya madumu yamafuta,madumu ya oil,matank Yale ya maji,mapipa Yale ya gresa kusanya pamoja.

ukichanganya mchin atanunua kwa Bei ya chini maana itabidi alipe watu wakuyachambua upya.✍️

swali la tano.
Ili uweze kumuuzia mchina unaingia naye ubia au mpk upate connection??

jibu✍️
kumuuzia mchina siyo mpk uingie naye ubia.ukishakua tyr na mzigo wako,unaenda na sample anangalia alafu atakupa bei kulingana na aina ya mzigo wako,Kisha atakwambia uende ulete.akiona mzigo haujakizi viwango anakwambia usilete.
kwahyo Nashauri nivyema wakati unaanza ukamuajiri mtu anayejua kuchambua aina ya chupa na plastiki Ili usipate shida sokon.✍️

swali la sita.
umesema hii biashara haina mambo ya lesen Wala tin no.je hicho kibali Chamazingira unakipataje nanibei gani???
jibu:✍️
kibali Chamazingira kinapatikana nemc nahiki kibali utakitafuta endapo unataka kufanya hii biashara kwakutumia mashine yaan kusaga.kama unakusanya tu nakuuza mazima huitaji kibali chochote kutoka popote pale✍️

swali la Saba:
kwasisi wamikoan tutauzia wap hizi chupa wakati wachina wote wapo dar???

jibu✍️
nyie wamikoan ambao hamsagi mnatakiwamtafute mkusanyaji mkuu ambaye nyie mtanunua kwawaokotaji na nyie mtauza kwake,Kisha yeye atayasaga nakuyaleta dar kuuza kwa mchina.
kumbuka haya makopo ukiwa hujayasaga nimepsi sana.ukisema utoe makopo Lori moja Arusha ubadala yakupakia Tani 30 utapakia Tani tano ambayo ukiuza hutopata hata pesa ya nauli.
kwahyo wewe utanunua kwa muokotaji,alafu wewe utauza kwamsagaji,alafu yeye ataleta mjini✍️

swali la nane
nizipi changamoto za hii biashara??

jibu✍️
hakuna biashara inakosa Changamoto,ila Ili ukue kibiashara lzm uzivuke changamoto.
changamoto ya kwanza nikwamba unaweza kufikisha mzigo sokon alafu mchina akakagua akakwambia analipa Bei fln ambayo siyo ile mliyokubaliana awali.mfano mm kipindi naanza niliongea nao vzr tu na sample wakaona wakasema watalipa 800 lkn baada yakufikisha mzigo wakaukagua wakasema nimchafu hivyo watalipa 700.ukiangalia nishatoa gari mkoan siwezi Tena kusema siuzi maana Sina pakuweka,ikabidi niuze.nikapoteza 100×28,000=2,800,000 ikapotea.kwahyo hiz ndiyo changamoto zahii kazi.changamoto nyingne nikwamba unaweza kununua mzigo kwa Bei kubwa,alafu ile ushajaza tan kazaa unasikia sokon Bei imeporomoka,huna namna inakubidi uuze urudishe mtaji hakuna faida.changamoto nyingne nikuibiwa mzigo,gari yako yamzigo kuanguka namengineyo✍️
swali la Tisa.
umesema lzm uwe na eneo kubwa.je! niukubwa waina gani??

jibu✍️
eneo lolote linatosha nikutegemeana na ukubwa wabiashara yako✍️
swali la kumi:
mzani wa aina gani unaotumika kupimia??

jibu✍️
mzani unaotumika kwa mkusanyaji mdogo,nimzani wa kutundika,inauzwa maduka ya pembejeo zakilimo.kwamsagaji atatumia mzani wakulaza ambao utatoshea kulaza gunia lenye kilo 100 juu yake.inaitwa digital scale.✍️

asanteni nyote mliouliza maswali kutaka kujua.ninaimani kwa uelewa wangu nitakua nimewajibu vzr nammeelewa.
note✍️yeyote atakayeanza kuifanya hii biashara akipata faida amkumbuke admin maana bila yeye kuruhusu post mngeendelea kusema Steve fremason anajenga majumba kila siku pesa anapata wap🤣🤣🤣
kumbuka mwanzo nimgumu changamoto zisikurudishe nyuma.

Mimi nilipofunga mashine hata sijasaga Tani kumi bearingi zikavunjika kuuliza dukan nikambiwa moja inauzwa 2.8ml🤣🤣 nikatamani kuachana nayo lkn rafiki yangu akaniambia nunua funga mashine pesa itarudi hiyo.

haya wapambanaji tupambane."
 
Swali mimi nipo Mwanza nataka nianze hii biashara ila sio kwa kusaga,nataka ninunue kwa wauzaji wadogo nikauze kwa mchina bila kusaga machupa,je Kwa hapa mwanza mchina anapatikana wapi??nipo mwanza mjini mitaa ya kirumba
 
Back
Top Bottom