jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Barikiwa sana.Msije kuniuliza maswali.
Mie nimecopy huko nimeileta.
"admin naomba nijibu maswali yaliyoulizwa Sana kupitia coment kuhusu hii biashara ya makopo ya plastiki[emoji120].
swali la kwanza:
mashine zinauzwa wapi? nazinauzwa Bei gani??
jibu:[emoji3578]
mashine zinauzwa kwa wachina,au unaweza kuweka oda Sido wakakutengenezea.bei yamashine ya size ya Kati inaanzia 5ml,6ml, mashine kubwa 8ml,na 12ml.[emoji3578]
swali la pili.
wachina wanaonunua haya makopo wanapatikana wap??
jibu: [emoji3578]
wachina wanaonunua haya makopo wanapatikana dar maeneo ya kigamboni kibada,kisemvule pwani,vikindu,tegeta,mwenge itv,mbezi makonde nak...[emoji3578]
swali la tatu:
umesema chupa za energy na Malta hazichanganywi je wachina nikwamba hawazinunui??
jibu:[emoji3578]
chupa za energy na zile na Malta rangi zake nitofauti kabisa nachupa zamaji na juice.kwahyo za eneg pamoja namalta zikusnye peke yake,Bei yake nichini kuliko hiz zamaji na juice.ukichanganya bila kuzichagua mchina atanunua mzigo wako kwa Bei ya chini na utapata hasara kubwa.[emoji3578]
swali la nne:
ni chupa zajuice na maji pekee ndiyo wananunua wachina au niplastiki aina zote??
jibu[emoji3578]
mchina ananunua chupa aina zote,plastik aina zote,mifuko ya nailon kama ile inazungushiwa ktk katon ya maji au juice,ananunua pia mifuko ya sanadarusi,ananunua viti vya plastiki,bakuli,vikombe,na kila kitu Cha plastiki.
unachotakiwa kufanya nikutenganisha aina ya plastik Ili ukifika sokon mzigo wako usilete shida.
mfano chupa zamaji aina zote pmaoja na zile za juice aina zote kusanya pamoja.
chupa za energy pamoja na zile za malita kusanya pamoja.
plastiki aina ya ndoo,viti,bakuli,vikombe,jjag,chupa ya chai,besen,Bomba zamaji,hizi pia kusanya pamoja.
plastiki aina ya madumu yamafuta,madumu ya oil,matank Yale ya maji,mapipa Yale ya gresa kusanya pamoja.
ukichanganya mchin atanunua kwa Bei ya chini maana itabidi alipe watu wakuyachambua upya.[emoji3578]
swali la tano.
Ili uweze kumuuzia mchina unaingia naye ubia au mpk upate connection??
jibu[emoji3578]
kumuuzia mchina siyo mpk uingie naye ubia.ukishakua tyr na mzigo wako,unaenda na sample anangalia alafu atakupa bei kulingana na aina ya mzigo wako,Kisha atakwambia uende ulete.akiona mzigo haujakizi viwango anakwambia usilete.
kwahyo Nashauri nivyema wakati unaanza ukamuajiri mtu anayejua kuchambua aina ya chupa na plastiki Ili usipate shida sokon.[emoji3578]
swali la sita.
umesema hii biashara haina mambo ya lesen Wala tin no.je hicho kibali Chamazingira unakipataje nanibei gani???
jibu:[emoji3578]
kibali Chamazingira kinapatikana nemc nahiki kibali utakitafuta endapo unataka kufanya hii biashara kwakutumia mashine yaan kusaga.kama unakusanya tu nakuuza mazima huitaji kibali chochote kutoka popote pale[emoji3578]
swali la Saba:
kwasisi wamikoan tutauzia wap hizi chupa wakati wachina wote wapo dar???
jibu[emoji3578]
nyie wamikoan ambao hamsagi mnatakiwamtafute mkusanyaji mkuu ambaye nyie mtanunua kwawaokotaji na nyie mtauza kwake,Kisha yeye atayasaga nakuyaleta dar kuuza kwa mchina.
kumbuka haya makopo ukiwa hujayasaga nimepsi sana.ukisema utoe makopo Lori moja Arusha ubadala yakupakia Tani 30 utapakia Tani tano ambayo ukiuza hutopata hata pesa ya nauli.
kwahyo wewe utanunua kwa muokotaji,alafu wewe utauza kwamsagaji,alafu yeye ataleta mjini[emoji3578]
swali la nane
nizipi changamoto za hii biashara??
jibu[emoji3578]
hakuna biashara inakosa Changamoto,ila Ili ukue kibiashara lzm uzivuke changamoto.
changamoto ya kwanza nikwamba unaweza kufikisha mzigo sokon alafu mchina akakagua akakwambia analipa Bei fln ambayo siyo ile mliyokubaliana awali.mfano mm kipindi naanza niliongea nao vzr tu na sample wakaona wakasema watalipa 800 lkn baada yakufikisha mzigo wakaukagua wakasema nimchafu hivyo watalipa 700.ukiangalia nishatoa gari mkoan siwezi Tena kusema siuzi maana Sina pakuweka,ikabidi niuze.nikapoteza 100×28,000=2,800,000 ikapotea.kwahyo hiz ndiyo changamoto zahii kazi.changamoto nyingne nikwamba unaweza kununua mzigo kwa Bei kubwa,alafu ile ushajaza tan kazaa unasikia sokon Bei imeporomoka,huna namna inakubidi uuze urudishe mtaji hakuna faida.changamoto nyingne nikuibiwa mzigo,gari yako yamzigo kuanguka namengineyo[emoji3578]
swali la Tisa.
umesema lzm uwe na eneo kubwa.je! niukubwa waina gani??
jibu[emoji3578]
eneo lolote linatosha nikutegemeana na ukubwa wabiashara yako[emoji3578]
swali la kumi:
mzani wa aina gani unaotumika kupimia??
jibu[emoji3578]
mzani unaotumika kwa mkusanyaji mdogo,nimzani wa kutundika,inauzwa maduka ya pembejeo zakilimo.kwamsagaji atatumia mzani wakulaza ambao utatoshea kulaza gunia lenye kilo 100 juu yake.inaitwa digital scale.[emoji3578]
asanteni nyote mliouliza maswali kutaka kujua.ninaimani kwa uelewa wangu nitakua nimewajibu vzr nammeelewa.
note[emoji3578]yeyote atakayeanza kuifanya hii biashara akipata faida amkumbuke admin maana bila yeye kuruhusu post mngeendelea kusema Steve fremason anajenga majumba kila siku pesa anapata wap[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
kumbuka mwanzo nimgumu changamoto zisikurudishe nyuma.
Mimi nilipofunga mashine hata sijasaga Tani kumi bearingi zikavunjika kuuliza dukan nikambiwa moja inauzwa 2.8ml[emoji1787][emoji1787] nikatamani kuachana nayo lkn rafiki yangu akaniambia nunua funga mashine pesa itarudi hiyo.
haya wapambanaji tupambane."
#MaendeleoHayanaChama