Biashara ya Computers

Biashara ya Computers

Joined
Jan 4, 2015
Posts
6
Reaction score
0
Natumai mmeuanza mwaka kwa amani na matumaini mapya,ninakuja jukwaani kutafuta ushauri,mawazo.Niko mkoa wa Kagera na hivi karibuni nimebarikiwa kupata chumba cha biashara pamoja na kimtaji cha shilingi Mil 4, napenda kufungua biashara ya kuuza Computers pamoja na vifaa vyake yaani (Computers &, accessesories), Pamoja na kuwa na wazo hilo sehemu sahihi ya kupata mzigo pamoja na ni jinsi gani biashara hii inaweza walau ikanipa faida kidogo hapa mjini kwetu:
Nimekuja kwenu wadau kuomba yafuatayo;
1.Je ni biashara sahihi ya kufanya wakati huu?
2. Je naweza kupata mtu wa kunisuply hizo computers kwa walau bei ya chini?
3. Je tofauti na hiyo biashara ipi nyingine inaweza ikanipa faida kidogo tofauti na hiyo?

Nb; Nimeamua kuchagua aina hii ya biashara maana walau nina uelewa wa computers and its accessories.
Natanguliza shukurani kwa ushauri wenu
 
Ninavyo jua biashara yoyote ikifanywa kwa umakini inalipa vizuri..kikubwa ni kufanya Utafiti wa soko. Je Umefanya utafiti na umewajua wateja wako ni akina nani...

KUHUSU MTAJI
Unaweza anza na Computer Accessories Hardware na Software alafu mtaji ukikua utaweka Kompyuta, printa,projector. Ukianza na kuweka kompyuta sasa huo Mtaji hautoshi.
 
biashara nzuri, Fanya utafiti WA soko lake ujiridhishe. kuhysu supply ya computer tuwasiliane, give pm
 
Tumia ushauri wa tired maana hapo kwa mahesabu ya haraka ukisema uanze na computer hautoona faida na itakula kwako..
 
Last edited by a moderator:
Tunahitaji kujiamini haswa kama tu wajasiriamali wadogo ili tukuze biashara zetu/kwani kidogo is /sio haba..
 
Natumai mmeuanza mwaka kwa amani na matumaini mapya,ninakuja jukwaani kutafuta ushauri,mawazo.Niko mkoa wa Kagera na hivi karibuni nimebarikiwa kupata chumba cha biashara pamoja na kimtaji cha shilingi Mil 4, napenda kufungua biashara ya kuuza Computers pamoja na vifaa vyake yaani (Computers &, accessesories), Pamoja na kuwa na wazo hilo sehemu sahihi ya kupata mzigo pamoja na ni jinsi gani biashara hii inaweza walau ikanipa faida kidogo hapa mjini kwetu:
Nimekuja kwenu wadau kuomba yafuatayo;
1.Je ni biashara sahihi ya kufanya wakati huu?
2. Je naweza kupata mtu wa kunisuply hizo computers kwa walau bei ya chini?
3. Je tofauti na hiyo biashara ipi nyingine inaweza ikanipa faida kidogo tofauti na hiyo?

Nb; Nimeamua kuchagua aina hii ya biashara maana walau nina uelewa wa computers and its accessories.
Natanguliza shukurani kwa ushauri wenu

Sijawahi kufika Bukoba. kuna duka lolote wanauza computer na accessories? umelenga zaidi mpya au used?
kama unahitaji ushauri zaidi ni-pm.
 
Biashara ya kompyuta siyo mbaya, tena ipo kwenye soko sana siku hizi. Ila usiegemee kwenye kuzaa tu kompyuta kamili uzaa na vifaa vyake.
 
Mkuu Eddy! Kama Umeridhika na Market Research Yako You can go ahead.Labda Uangalie Pia Upande wa Smart Phone Mana Nazo Sikuizi Zimekuwa na Uhitaji Sana.Waweza Weka vile vitectono vya bei ya kawaifa kwa kuanzia.

Kila la Kheri Mkuu
 
Asante #Bw Daffa ntafatilia ushauri wako
 
Back
Top Bottom