Asante Kwa ku share utaalam katika biashara la dagaa
Naomba ushauri kuhusu mtaji ni kiasi Gani?, masoko yapo mikoa Gani, gharama za usafirishaji? Risk za hii biashara ni zipi? Bei ya hapo ipoje n.k
Swali lako ni pana sana japo nitakujibu kwa kifupi ili na wengine waone na kuongezea.
MTAJI.
mtaji wa dagaa nikiasi chochote ulicho nacho maana huku tunapima kuanzia Dumu 1 yenye kilo 4.lakini kwa ushauri zaidi kuanzia gunia na kuendelea ni nzuri zaidi na kuongeza faida.
BEI YAKE.
kwa huku hamna bei maalumu ya dagaa inafuatana na jinsi dagaa watakavo toka ziwani, quality ya dagaa(muonekano wake),aina ya dagaa wa mchanga na wasio na mchanga bei tofauti.
RISK ZAKE.
bei kupanda ghafura huku ziwani na kusababisha wateja wako kuona umewaongezea bei kupelekea wateja kupungua.
jinsi ya kukwepa hakikisha unajuwa muda na msimu mzuri wa kuchukua mzigo ili isije kusumbua sokoni.
USAFIRISHAJI.
dagaa unaweza safirisha kwa gari ya Abiria yaani bus au LORI.
Usafiri wa bus ni gharama kwa mikoani kuanzia Tsh 15,000/= -20,000/= kwa guniq moja.
LORI gunia moja linaanzia Tsh 10,000/= -14,000/= mkoani hiyo pamoja ushuru kwa kila gunia.
SOKO.
kwa upande dagaa ni chakula kwa asilimia kubwa Tanzania maana yake soko ni wewe mwenyewe utakapo ona ni rahisi kufanya kazi.
Dagaa wanaliwa kila kona ya Tanzania