Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

Habari wakuu.

Wenyeji wa mkoa wa Shinyanga na Simiyu biashara ya dagaa soko lake.

Hii biashara ya Dagaa naikubali sana japo sijaanza kuifanya lakini nahisi ipo vizuri.

Na vipi kuhusu pesa ya kuanzia kwa wazoefu wa hii biashara ya Dagaa ni shilingi ngapi. Nisaidieni kimawazo wakuu.
 
Ni biashara nzuri mkuu hasa kipindi hiki cha hali ngumu ya maisha. Tunalazimika kununua dagaa. Nyama ni anasa.
 
Nipo Bukoba kama utahitaji dagaa wa uku ni pm tuyajenge
 
MM NAOMBA NAMBA YAKO , MKUU , NAITAJIKUFANYA HII BIASHARA . 0767216191
 
Kitu kinachorudisha nyuma ni soko, kama soko likipatikana la uhakika mtu unafanya kazi vizuri
 
Heri ya mwaka mpya 2021.
LAKE FOOD PRODUCT SUPPLIER

Wauzaji na wasafirishaj wa samaki na dagaa waliokaangwa mikoani.
Jipatie dagaa safi wa mwanza waliokaangwa
Vizur na watamu Hawana michanga.
Kula dagaa kwa Bei
nafuu kabisa kwa matumiz ya nyumbani na
biashara package zipo za 200,500,1000,2000, na 5000
Sado 20000
Ndoo ndogo 35000
Ndoo kubwa 55000

Tunapatikana wilaya ya karatu iliyoko mkoa wa Arusha. kwa mawasiliano
zaidi 0717200471 na 0625406328 nyote
mnakaribishwa sana.karibu weka dukan,supermarket au sokon.

Tunauza jumla na rejareja. jumla pia tunauza kuanzia packt 50.

Mikoani tunasafirisha kwa gharama za mteja.

Tufollow page yetu Facebook na Instagram. Lake Food Product

https://www.facebook.com/
Instagram:
 
Mimi ni kijana niliyeamua kuongeza kipato kwa njia nyingine bila ya kutegemea ajira.

Wazo lililokuja kichwani mwangu ni kuuza dagaa wabichi waliokaangwa kutoka mwanza. Maana huku niliko(Mbeya) zinapatikana kwa uchache sana.

Nahitaji msaada wenu kwenye mambo haya;


1. Dagaa hawa kwa pale mwanza wanapatikana wapi?

2. Bei yake kwa vipimo mbalimbali kama sado na ndoo ni shilingi ngapi?

3. Naweza kupata mtu wa moja kwa moja kutoka hapo ziwani bila kufanyiwa udalali wowote?

NB: Nina mtaji wa shilingi laki moja na nusu tu nina imani itatosha.

Naombeni mnisaidie mawazo yenu sana sana kwenye hayo maswali matatu hapo juu.

Ahsante.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Habari za majukum wakuu,

Nimeamua kuanzisha uzi huu ili kupeana changamoto, motisha, ujanja , locationa ambazo dagaa wanapatikana kwa wingi na rahisi zaid, uandaaji ili zikae na shape nzuri kwa muda, pamoja na idea nyingine zinazohusiana na biashara hii.

Binafsi nimeamua kuanza kufanya hii biashara na nimejikita kwenye kuuza dagaa wa mafuta(sio dagaa mchele) kutoka Mwanza. Ninauza kwa jumla na rejareja japo mwanzo nilijipanga kuuza jumla tu lakini changamoto za wateja wa jumla kupenda kulalia wafanya biashara wapya ilinifanya niamue kuuza reja reja pia kuliko kuwategemea wao.

Changamoto mpya kwa sasa naona ni bei ya mafuta ilivyo panda, wateja wengi wanafahamu ilo lakin wanataka kubaki kupokea mizigo saizi zile zile kwa garama za zamani pia.

Natamani kujua bei za sehemu mbalimbali kwa wauzaji, mnauza kwenye Range ipi, na wanunuaji pia mnaweza tupea uzoefu mnanunuaje

Kwa mikoa ya kaskazini bei ina Range kutoka 32k -42k (inaweza pungua zaid au kuzid) kwa debe.

Kwa wanao hitaji Dagaa pia ni Dm nikupe mawasiliano

Karibuni wadau
 
Niko Musoma nataka nianze kufanya hii biashara though sijui a,b,c zake.
 
Mimi nipo Dar nipo interested na hii biashara naomba mwongozo wake
Kwa Dar upande wa masoko sijui kupo vipi ila upande wa ziwani unaweza kuwa na mtu ama wew mwenyew; unanunua dagaa wabichi kwenye mtumbwi, unalipia sehemu za kuanika, unanunua mafuta, kuni, n.k dagaa zikikauka kuna wakaangaj unawalipa wanakukaangia, mna pack kwenye viroba mnalipia ushuru na kibali kama hutaki usumbufu laikni, then unasafirisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…