Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

😳😳😳😳 mkuu kumbe huku mjini ilikua nipigwe kinoma yani eti ndoo elf 70 mwisho 65 . Ngoja nijipange niende, vp gharama za usafiri kuanzia mzigo namimi mwenyewe?
Jaribu kufika Happ mwaloni pale wanapandia hizo meli ziendazo visiwani uulize Bei,kwasasa,,haiwezi kuwa kubwa maana na wewe mzigo wako haitakuwa Tani kadhaa,Bali box mbili tatu au mifuko michache.
Ila Kama unataka kuchukulia Happ kwa elfu 40,Kuna jamaa Happ mwaloni alikua nao hao dagaa juzi tu waweza kumcheck
 
Habari ndugu. Hongera sana kuingia katika ujasiriamali. Hakuna tatizo kusoma vitabu sababu unaongeza elimu. Ila ukweli nikuambie kwamba waandishi wa hivyo vitabu wako kimaslahi zaidi. Huyo mwandishi wa hicho kitabu Kiyosaki anaitwa, yeye kampuni yake inayotoa hivyo vitabu ilifilisika na hadi aka-file bankruptcy. Sasa jiulize mtu anayeshauri vizuri anafilisikaje kama sio uongo tu kaandika.

Kiukweli kujua biashara ni kuifanya. Na utakapoifanya ndio utajifunza. Umetaka faida, napenda kukupa habari mbaya kwamba usitegemee faida hadi baadaye sana kwa hio biashara sababu umeshasema hauna soko na haujui pa kuanzia. Manake utafanya makosa mengi kwanza ya kujifunza ambayo yataleta hasara hadi ukipata mfumo mzuri ndio utapata faida. Kwa hio kama lengo ni faida sasa hivi, tafuta biashara unayoijua vizuri sana, na ambayo tayari una wateja ndio uanze nayo hio. Manake tafuta wateja kwanza kabla ya kuanza. Kama ni dar, usinunue bidhaa tafuta wateja wa uhakika kabisa kabis, ndio upeleke bidhaa upate hela yako. Hongera tena. Ujasiriamali ni mzuri sana, lakini mwanzo una changamoto nyingi.
Ahsante sana mkuu kwa ushauri muruaaa. Ngoja niende visiwani kama alivyonishauri mkuu hapo juu ninunue mzigo kiasi ili nije nao dar kama kupata experience hata nikipata hasara Kama ulivyosema itakua imenijenga sana nakujua makosa yangu. Nakubaliana nawewe kabisa hawa waandishi wa vitabu wapo kibiashara tuu hamna lolote nimeamini, ila nimeamua kutake risk nipo tayari kuanguka ata mara kumi sio mbaya but am sure one day nitasimama. Thanks again mkuu kwa ushauri mzuri.
 
Nipe namba yake mkuu, ila ningependa niende mwenyewe kisiwani niweze kujifunza zaidi. Kwasababu naanza na mtaji wangu sio mkubwa kiivyo isitoshe sina soko la uhakika inabidi nipate mzigo kwa bei rahisi ili hata nikija dar niuze kwa bei pungufu nirudishe hela yangu huku nikizidi kukomaa zaidi na zaidi kibiashara. Ngoja nije niende mwaroni nipate abc zote mkuu
 
Nipe namba yake mkuu, ila ningependa niende mwenyewe kisiwani niweze kujifunza zaidi. Kwasababu naanza na mtaji wangu sio mkubwa kiivyo isitoshe sina soko la uhakika inabidi nipate mzigo kwa bei rahisi ili hata nikija dar niuze kwa bei pungufu nirudishe hela yangu huku nikizidi kukomaa zaidi na zaidi kibiashara. Ngoja nije niende mwaroni nipate abc zote mkuu
Haya nakupa screen shot Kama una Twitter account unaweza kubonga nae,ila namba Ni hizo,angalia tu asiku discourage kwenda chimbo mwenyewe ili ununue kwake.
Screenshot_20200513-104115~2.png
 
Yani kwanza dagaa kununua kwa hiyo bei ni kubwa sana kama unaanza biashara, kama upo mwanza nenda Igombe, mwaloni,bwiru jiwe kuu ukanunue dagaa kutoka kwa wavuvi moja kwa moja ndio uzikaange mwenyewe. kwenye kuuza jiulize unataka kuuza jumla au rejareja hii itakupa muongozo wa kufanya biashara yako. Pia usiache kutumia mitandao ya kijamii hasahasa facebook kule kuna wateja wa kila aina. All the best
 
Kitu kingine kwenye dagaa hasa hasa huku mwanza angalia sana ni dagaa gani wa kukaanga unanunua, kuna wanaokaangwa wakiwa wabichi kabisa hawa soko lake lipo juu, kuna wengine wanaanikwa kidogo juani then wanakaangwa, na wengine wanapigwa jua kabisa halafu wanakaangwa haya makundi mawili ya mwisho kama biashara ni ngeni kwako mzigo unaweza kukufia maana afta sometime dagaa huanza kuwa wachungu.
 
Kitu kingine kwenye dagaa hasa hasa huku mwanza angalia sana ni dagaa gani wa kukaanga unanunua, kuna wanaokaangwa wakiwa wabichi kabisa hawa soko lake lipo juu, kuna wengine wanaanikwa kidogo juani then wanakaangwa, na wengine wanapigwa jua kabisa halafu wanakaangwa haya makundi mawili ya mwisho kama biashara ni ngeni kwako mzigo unaweza kukufia maana afta sometime dagaa huanza kuwa wachungu.
Duh nilikua siijui hii mkuu. Shukran sana asee
 
Yani kwanza dagaa kununua kwa hiyo bei ni kubwa sana kama unaanza biashara, kama upo mwanza nenda Igombe, mwaloni,bwiru jiwe kuu ukanunue dagaa kutoka kwa wavuvi moja kwa moja ndio uzikaange mwenyewe. kwenye kuuza jiulize unataka kuuza jumla au rejareja hii itakupa muongozo wa kufanya biashara yako. Pia usiache kutumia mitandao ya kijamii hasahasa facebook kule kuna wateja wa kila aina. All the best
Shukran sana mkuu
 
Kama uko na mawazo ya kufanya biashara ni bora ukaifanya wala mtu asikuogopeshe na ww ukaacha kufanya mjasiliamali hatakiwi kuogopa kufanya kitu cha kufanya ni kuangalia hizo risks alizozisema mdau hapo juu kuna kipindi kama mwezi umepita,nilitembelea Kilosa nikataka kwenda porini hivyo ikanipasa kununua baadhi ya vyakula pale mjin,nilistaajabu kukuta bei ya kilo moja ya dagaa iko sawa na kilo moja ya nyama kwa Dar kwa huko nyama iko chini kidogo zaidi ya dagaa hao wa Mwz hivyo inaonekana soko lake ni zuri sehemu hizo ingawa sikufanya utafiti wa kutosha sana ila nilizunguka sokoni na nikakuta bei iko juu zaidi ya nyama hivyo kama kweli uko tayari unaweza ukafanya utafiti wako katika hiyo biashara ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko maeneo hayo sio kila bidhaa lazima iende k/koo mdau hata maeneo mengine kuna masoko mazuri tu cha msingi ni ujasiri na kutokata tamaa
Daaaah ume ongea mpaka nimeanza kuvutiwa na mm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za asubuhi wakuu?

Naomba kufahamishwa aina ya hii ya dagaa kutoka kigoma inafanyikae kwa upande wa huko?

Hali ya soko lake iko kwa sasa? Bei yake kwa kuanzia ngazi ya gunia moja kwa huko kigoma na mpaka kuja kuuza miji mikubwa kama dar es salaam, mwanza, tanga na mikoa mingine, bei zake zikoje na hali ya soko kiujumla ikoje wadau?

Ahsanteni!
Mkuu wadau waki kujibu uni tag

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Mkuu,
Kwakuwa wazo lako ni biashara ya dagaa, nadhani hata biashara ya samaki wengine itakufaa!

Sababu samaki na dagaa naona ni kama kitu kile kile.
Kwakuwa wewe uko hapo dar, na naona umeandika kuwa wewe ni mwenyeji (kama sijakosea).

Basi tafuta soko la samaki (sehemu utakapo uza samaki)
Mimi niko nje kidogo ya dar (kilomita 160 hivi) nafanya hili na lile.
Hapa nilipo kuna samaki wengi sana, ninaposema wengi elewa ni wengi.
Hali jinsi ilivyo, unakuja mpaka eneo husika, hapa kuna samaki wanauzwa kwa kipimo cha ndoo kubwa.

Ndoo ni wastani wa 20k - 25k hapo ni mwisho!
Kwa bei hiyo, ukinunua samaki wa 200k, ni mzigo wa kuzidi sana, mwingi. unaweza wakaanga au ukawabanika.

Hao ni samaki wa magamba. Ukija kwenye kambale na jamii zake pia hao ni wengi mara dufu zaidi!Samaki wapo, wananuzi hawatoshi.

Swala la usafiri huku ni boda boda, ila mvua ikinyesha njia ni mziki kidogo.
Mtandao pia huku inakupasa upande japo kisiki ndiyo uwe hewani (niko juu ya mti hapa ninapotype).
Keybord imejaa!
Maeneo gani ulipo?
 
Unacho taka kufanya nazani kinafanywa na watu wengi sana, so kinacho takiwa aisee ni kuumiza akili sana ki chekecha wanaita.

Kwa sasa kwa sababu ya Ushindani anaye umiza akili sana ndo anaye toka,

Lazima uwe mbunifu, kama gharama ni kubwa unafanyaje? Hakuna njia bandala?

Jaribu kuumiza sana kichwa, make wenzako wanao uza utakuta wana njia zao ambazo hawawezi kamwe kukuambia so ni juu yako na wewe kuja na zako na kuziwekea password.

Mimi ni kijana wa miaka 26, baada ya kumaliza kusoma kitabu cha “rich dad poor dad” nakumbuka nilikuja na uzi wa kuahidi kuyafanyia kazi yale yote niliyojifunza kutoka kwenye kitabu kile.

Basi nilianza kufanya saving za hapa na pale mpaka sasa nina laki 4 na elfu 32, wazo la biashara nililokuwa nalo toka muda niliplan kufanya biashara ya dagaa wa kukaangwa kutoka mwanza kwenda Dar so jana nilipata nafasi ya kwenda pale ferry kuuliza bei na vitu kama hivyo.

Ndoo ya dagaa wa kukaangwa ni elfu 65, boksi la package ni elfu 1500, kutoka pale ferry mpaka nata kwenye mabasi ya zuberi ni elfu 1000 kwa boda boda, kusafirisha mzigo kuanzia debe moja ni elf 10000 hadi 15 elfu. Sasa hapa najiuliza mimi uko Dar nitauzaje hao dagaa ili kufidia hizo gharama na nipate faida?

Dar es salaam bado sijafanya utafiti wa soko lenyewe hapa si naenda kuangukia pua wakuu? Nimetoka kusoma ule uzi wa hasara gani umepata kwenye maisha yako ndo nimeishiwa nguvu kabisa.

Naomba mtu mwenye uzoefu wa hii biashara aniambie kwa mchanganuo huo wa gharama naweza vipi kupata faida nikija kuuza Dar au kama nitaangukia pua mniambie mapema, kitabu Kimenifunza kutake risk lakini mmmh.

Nb. Mimi makazi yangu yapo Dar so ni mwenyeji sema Mwanza nipo kwa muda huu.
 
Kule ulikuwa unadanganya kwanini?
Hahaha,we umejichanganya,,naration ya watu wawili tofauti,,

Haya mrejesho vipi wakuu,huu mwaka wa nne sasa,tumetengeza bilionea wangapi hapa?
 
Back
Top Bottom