Biashara ya dagaa nje ya nchi

Biashara ya dagaa nje ya nchi

changaule

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
6,039
Reaction score
10,151
Habari ndugu wana JF

Nataka nianze biashara ya uuzaji wa dagaa lakini kwa kuwasafirisha nje ya nchi nikilenga Congo na Comoro.

Hivyo kama kuna watu humu wazoefu wa biashara hizi naomba msaada wa kujua utaratibu ulivyo juu ya biashara hii. Ikiwa pamoja na usafirishaji, ushuru na mengineyo.
 
Anzisha point ambazo zitapokelewa. Huko congo/ Comoro mpokeaji ni nani?
 
Ukifanya kazi na wacomoro kuwa makini,wana kaubabaifu fulani!
 
Comoro wanahitaji dagaa? Au unakusudia kutoa Comoro kupeleka Congo?
 
Dagaa ukipeleka Congo ni deal sana kwani kuna ndugu yangu huwa anapeleka Congo na Kenya,na nafanya nae kazi.
Yaani kule Congo dagaa inasaminiwa sanaa kuliko kawaida ni sawa na chipsi kwa wadada Bongo kule mpaka unga wa dagaa upo wanatengenezea uji.
Kwa ufupi dagaa inaliwa kwa haraka sana na faida ni kubwa kwa mfano gunia iliyo nunuliwa kwa 200000/= kule inaweza kuuzwa kuanzia 600000/= na kuendelea.
VIBARI NA UTARATIBU .
1.uwe na TIN NAMBA NA LESENI YA BIASHARA KUTOKA TRA.
2.INJE NA HIYO LESENI YA TRA UWE NA LESENI YA KUSAFIRISHIA DAGAA NDANI YA TANZANIA AMBAYO KWA SASA NI ELFU 30 KWA SASA.
3.UWE NA KIBALI KUTOKA WIZARA HUSIKA YA MALI ASILI AMBACHO UKIFUATILIA HUWA VINATOKA DODOMA KWENYE WIZARA HUSIKA.

Ukifanikiwa hivyo wewe nikupiga hela tu dagaa ni biashara ya uhakika mkuu.

Mambo mengine sio lazima tuweke hapa .sometimes biashara ni sili.
 
NAHITAJI MSAADA ZAIDI NDG, NJOO PM KAMA HUTAJALI
 
Unataka upeleke Congo eneo gani, wengi wanafanya biashara ya kupeleka Lubumbashi kupitia Tunduma. Wengine wanapeleka Bukavu na Goma wanapitia Kigoma.

Kama utafanikisha kupeleka Kisangani kule utapiga pesa zaidi ingawa changamoto ni umbali mkubwa.Kisangani vyakula bei ni kubwa sana na uhitaji ni mkubwa
 
Peleka uko uko Congo,comoro achana napo,hakuna huitaji wadagaa kule.peleke ng'ombe,mbuzi,magimbi,vitunguu,n.k
 
Dagaa chafu au safi?tuanzie hapo kwanza.Machimbo ya kuyapata unayajua?
 
Habari ndugu wana JF

Nataka nianze biashara ya uuzaji wa dagaa lakini kwa kuwasafirisha nje ya nchi nikilenga Congo na Comoro.

Hivyo kama kuna watu humu wazoefu wa biashara hizi naomba msaada wa kujua utaratibu ulivyo juu ya biashara hii. Ikiwa pamoja na usafirishaji, ushuru na mengineyo.
Kwa ushauri TU nenda kafanye utafiti kwanza wa soko , nenda na sample tu kidogo, kabla ya kununua mzigo mkubwa
 
Kuna wale dagaa wa mafia wana soko sana Congo... nina rafiki yangu mkongo ndo biashara yake kuu hiyo. dagaa wa mafia wakiwa adimu huwa anafuata wa zenji.. ila wa mafia ndo wazuri na wana bei kubwa pia
 
Dagaa nyama, Mafia tayari wakusanyaji wengi bei ya kununua ipo juu. Angeenda Pangani Maeneo ya Mkwaja na Kipumbwi napo zinapatikana hizo dagaa
 
Kuna wale dagaa wa mafia wana soko sana Congo... nina rafiki yangu mkongo ndo biashara yake kuu hiyo. dagaa wa mafia wakiwa adimu huwa anafuata wa zenji.. ila wa mafia ndo wazuri na wana bei kubwa pia

Mi mwenyewe nawahitaji

Masokoni wamekuwa adimu sana
 
Back
Top Bottom