gwijimimi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2011
- 7,344
- 3,610
Biashara ya Trekta nami naifanya pia. Ila Mimi hii biashara nimebugi sehemu mbili anbazo ukiifanya nawe uwe makini usibugi kama Mimi.
Kwanza Trekta nililinunua Jipya kabisa, tena Massey Ferguson ila halikua la Original from UK, Bali under license from Pakistan, yanauzwa Sinza Mori kama waelekea Meeda Bar upande wa kushoto. Ni heri ningenunua Used but original from UK kuliko Mpya but under licensed.
Pili location ya biashara. Mimi nalima Ufuta Lindi, hivyo nalo nililipeleka Lindi. Kule kilimo ni Ufuta tu Mwishoni mwa Mwaka hivyo sehemu kubwa ya mwaka linakaa idle, mzunguko wa hela unakua mdogo. Linabebaga korosho sometimes but kwa trailer ya kukodisha. Hivyo ili uione faida nakushauri uliweke sehemu ambapo wanalima mwaka Mzima. Faida ingine ya eneo hili ni kua ardhi sio ngumu sana hivyo trekta haiumii.
Lakini kwa ushauri zaidi sio lazima utumie zote 47mil ziishe sasa, waweza pia kufuga kama alivyosema mdau hapo juu, kilimo cha mboga mboga na pia kuwekeza Nyingine kidogo hata kwenye kilimo cha miti.
Ila daladala, SIKUSHAURI aisee from vivid experience niliyo nayo sasa!!
Mkuu nahtaj Msaada wako kuhusu kilimo cha Ufuta mkuu