Kilanga komo
JF-Expert Member
- Aug 27, 2022
- 337
- 290
Changamoto za biashara ya Delivery Ni zipi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakuu karibuniChangamoto za biashara ya Delivery Ni zipi?
AsanteIpo kwenye kuaminiana kati ya wewe na mteja
Hahah hiyo Ni hatariMteja kuingia mitini...huku wewe ukiwa umesha mfikishia mzigo alipo kuelekeza umpelekee
Ni kweli aiseeeTrust ndo changamoto kubwa
DuhKutapeliwa mzigo ukaenda na pesa usilipwe...
Hahah watu hawana hurumaUsimpe mtu mzigo kabla hajakupa pesa mkononi. Sio eti mtu anakwambia niletee mzigo niko hapa jengo la NSSF ukifika unishtue nije nichukue mzigo. Unafika unampigia anatoka nje, anapokea mzigo halafu anakwambia ngoja niingize huu mzigo nilete na hela. Ndio humuoni. Unajaribu kuulizia unaambiwa hatumjui mtu unayemtafuta....ndio ushaibiwa hivyo
Asante kwa kutujulisha hayo...1. Umefika eneo husika mteja kaingia mitini , inabid urud na mzgo hapo mafuta umechoma
2. Kutapeliwa , mteja anapokea mzgo kabla hajakupa pesa then anaingia ndani , hafu anapotea mazima
3.usalama , Mteja anakuelekeza umletee mzgo eneo ambalo usalama wako ni mdogo anaweza akawaandaa watu wakakupora
4.Umepeleka mzgo amekulipa fresh , baada ya Muda anakupigia simu mzgo labda haufanyi kazi , inabid urud Tena kwenda kuangalia na kuset vizur ,
5. Bidhaa kukataliwa na mteja , ile umepeleka mteja anakuambia bidhaa na picha hazifanani[emoji16] hiyo inakuwa imekula kwa mtu