Biashara ya Dhahabu

Licenced dealers wapo masoko ya dhahabu nenda huko, na wewe pia lazima utambulike na mamlaka.
 
Usituchoshe...Mbona rahisi,..kama una mteja tayari si muulize yuko tayari kununua kwa shs ngapi? Then angalia bei ya huku ni shs ngapi..? Angalia operation costs then utajua kama kuna faida au la.
 
We jamaa mbona mbabaishaji sasa??

Kama umepata mteja si ina maana mmeshakubaliana na bei na specifications za hiyo dhahabu au?? Kama mmekubaliana bei hao delears wewe huwajui? Watafute wewe hao dealers nao ujue bei zao, ukimaliza nenda TRA ujue mambo ya kodi, ukimaliza angalia utaratibu mwingine wa kusafirisha au kusafiri nazo, piga hizo gharama zote then linganisha na hiyo bei uliyopewa na mteja wako.

Mambo mengine mnataka kutapeliwa tu huku mitandaoni.
 
Nyuzi za kitapeli tapeli hizi mkuu. Yaani mtu mteja anaye sasa anachosumbua watu hapa ni nini?? Au ndio unasukwa mtego wa kutapeli watu
Usituchoshe...Mbona rahisi,..kama una mteja tayari si muulize yuko tayari kununua kwa shs ngapi? Then angalia bei ya huku ni shs ngapi..? Angalia operation costs then utajua kama kuna faida au la.
 
Usituchoshe...Mbona rahisi,..kama una mteja tayari si muulize yuko tayari kununua kwa shs ngapi? Then angalia bei ya huku ni shs ngapi..? Angalia operation costs then utajua kama kuna faida au la.
asante,
ila nadhani watu hawakunielewa!
swala langu la msingi lilikuwa nataka kujua, bei huwa zinakuwa kiasi gani kulikana na bei ya soko.
Nilikuwa nataka kusikia kwa watu “experienced” kuhusu asilimia za discount ni kiasi gani.
 
Njoo Kahama, nitafute tukaweke kikao Chillers kwanza, kabla hatujaenda machimboni Mwime, Nyangalata, Mwabomba tukalangue mzigo kwa wachimbaji wa dogo. Muhimu tuwe na mizani na machine ya kuchekia purity.
 
"Ukiitwa kwenye fursa ujue wewe ndio fursa"

Kuna ndoano imerushwa hapa ajichanganye mtu akalie kimya kimya.
Nashukuru,
ila watu hawajanielewa swali langu la msingi.

“ mimi nilikuwa nataka kujua asilimia ngapi naweza kupata ya discount kwenye soko kwa sababu bei huo ni sawa duniani kote”
 
Nyuzi za kitapeli tapeli hizi mkuu. Yaani mtu mteja anaye sasa anachosumbua watu hapa ni nini?? Au ndio unasukwa mtego wa kutapeli watu
nadhani haukunielewa swali langu,

nilikuwa nasema, kama bei ya dhahabu ni sawa duniani kote, nawezaje pata faida? sasa nilitaka kusikia toka kwa “experienced dealers “ kuhusu asilimia za discount inaweza kuwa kiasi gani. hili ndio swali la msingi.
 
Nashukuru,
ila watu hawajanielewa swali langu la msingi.

“ mimi nilikuwa nataka kujua asilimia ngapi naweza kupata ya discount kwenye soko kwa sababu bei huo ni sawa duniani kote”
Aanha, nimekuelewa sasa,
Pia swali lako lina make sense tusubiri wataalam waje wakujuze,

Ushauri wangu unge edit post yako na kuliweka hili swali ili kwa mchangiaji mpya asipate tabu ya kuelewa kama sisi
 
sawa nashukuru, ngoja ni edit upya.
 
Wala sijakataa mpango wako ni mzuri, lakini madini yana ushetani mwingi waweza nunua kitu original leo kesho kiwe fake.ndo maana unatakiwa kuwa mshirikina sana au umshikilie Mungu sana.

Mara ya kwanza utapata pesa wakuvutie ktk soko , mara ya pili utapigwaa mpaka utauza nyumba ya urithi.
Oh kumbe wewe ni msafiri na hauko tz bas biashara pekee inayo kufaa ni real estate, nunua viwanja wekeza kwenye ardhi utakuja nikumbuka baadae.
Narudia tena na tena kama pesa ipo jenga apartments, nunua viwanja baada ya mwaka unaanza kuuza kwa bei kubwa.

Achana na madini wale umbwa wakishajua life stail yako watakupiga tukio hutoamin.

Hao licensed dealers ndo wahuni wenyewe mjini.
Mtu ambae alifanikiwa kwenye madini lazima kwanza apigwe afirisike akili imkae sawa. Akirudi sokoni nae anarudi ashakomaa akili uchawi wote wa dunia hii anaujua basi hapo ndo anarudi sokoni.

Kama nakudanganya hiyo pesa iweke kwenye madini mwaka mmoja nakusubiri hapa jf ukisaga meno. All the best
 
unaweza kuwa ushauri mzuri,ila sio ushauri anaotaka mtoa mada..
 
Nashukuru sana kwa mda wako na ushauri,nimekuelewa vizuri sana.
 
unaweza kuwa ushauri mzuri,ila sio ushauri anaotaka mtoa mada..
Nampa tu taadhali maana kuna baba hapa kapigwa huyo busy anauza bus zake ahaaa kabakiza moja , ila alishawahi pata kupitia hayo madini sasa hivi wahuni wamemuingiza mjini hana namna tofautu na juuza bus zake.
Ahaaaa ni mzoefu kweriiiii kweri ila kapigwa tena
 
Biashara ya dhahabu ina chain yake, hata hao super dealer wanapata mali kupitia kwa broker wao na wachimbaji wadogo na pia Wana connection za maporini halafu eti dealers achukue mali akuuzie wewe kirahisi tu kweli?
 
Kama sio sehenu sahihi kwanini uulize swali?
Akili zako bado zinakukumbusha kuchezea matope
 
Nimejifunza hata Mimi
 
Kama sio sehenu sahihi kwanini uulize swali?
Akili zako bado zinakukumbusha kuchezea matope
kaka,
Nadhani watu hawakuelewa swali, ikiwemo wewe pia!

Lengo ilikuwa sio kununua dhahabu, bali kutaka kupata maelezo tu.

Nashukuru kwa mchangonwako.
Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…