BradFord93
JF-Expert Member
- Oct 11, 2017
- 917
- 2,217
- Thread starter
-
- #61
Maduka rejareja ndio yanayoendesha maisha yangu. Nikiwa kijana bado wa miaka 23. Ila Sasa nataka mwaka huu nifungue biashara tofauti na hii ambayo ninauzoefu nayo mkubwa
Sent using Jamii Forums mobile app
DuPole sana ndugu. Marafiki co watu. Mimi huyu rafiki yangu kuna cku aliniudhi ndo maana nkamkazia, alipita dukani tukasalimiana then akachukua keki akala aksema "hii utalipa wew". Nilikasirika kwakweli, ila nkasema ngojea nimuonyeshe upande wa pili nakuaje. Tangu juz nlpomkazia, hajaja mpaka leo
Sent using Jamii Forums mobile app
Watakupiga kipapaiHahahahhaaaa kwa hapa nilipo kuna maduka ma3, na wao ndo walianza biashara, lakin hakuna anayenizidi kwa mauzo ya siku nzma...!!
Sent using Jamii Forums mobile app
ila biashara ya duka la rejareja ina faida ndogo sana inahitaji uvumilivu na kukusanya hizo ngawira kidogo kidogo mpaka ujaze kibabaBiashara ya duka ni biashara rahisi kufanya ukiwa strict na haina complication wala msimu kama zilivyo biashara nyengine. Shida ni mazoea mabaya watu hufanya na wateja ndio huleta mushkeli. Aheri uonekane bandidu kuliko kuwa na moyo wa huruma halafu unateketea.
Ulizingua.Umenikumbusha wakati nasoma sekondari, miaka ile maduka mengi ya wapemba. Na ule utaratibu wa kununua mahitaji ya nyumbani ya mwezi mzima haukuwepo, mfano sabuni ya kufulia kila siku lazima mtu aende dukani kununua. Vivo hivyo mchele na harage la jioni.
Sasa siku za jumamosi kuna duka jirani na nyumbani muuzaji alikuwa kijana tuu sikumbuki kabila lake ila alikiwa ananipenda balaa. Kila nikienda dukani nikimpa hela naomba sabuni anachukua sabuni ananipa hela hapokei, nikiendelea kusisitiza achukue hela anachukua hela nyingine kwenye droo ananipa. Nikajua huyu ananipenda ila mie sikumpenda hata kidogo nikaona anafanya vile ili niendelee kukaa dukani pale afurahie kunitizama.
Alivoona simuelewi akamwambia dada yangu mmoja tulikuwa tunaishi nae (mtoto wa baba mkubwa) dada akawa nanituma dukani, Kasie nenda dukani kanunue mafuta ila niombee na halfkeki.
Sikumfilisi duka lake Ila nilifaidi hela ambazo hakupokea nikawa naweka akiba.
Kweli biashara ya duka ni ngumu, yataka moyo.
Wateja wengi wamefungua biashara mkuu. Tafuta namna ya kufanya.Mimi wateja wamepungua sana yaani mauzo yapo chini ya elfu 50 kutoka zaidi ya kilo 100 nifanyeje niongeze wateja vitu vinadoda dukani
Sent using Jamii Forums mobile app
Watakupiga kipapai
Mkuu unaendeleaje na biashara yako?Duka unaweza kuanza hata na laki 5....kkubwa n moyo na msimamo wa kulisimamia
Kwanza chunguza unapotaka kuweka biashara
Chunguza bidhaa adim...iweke
Chunguza pia kipato cha wateja wa hyo sehem(hii n kujua aina gan ya bidhaa zitatoka)
Chunguza washindan wako(wauza duka wenzio...mapungufu yao na ikiwezkana muda wanaofunga na kufungua)
Katika kipindi cha mwanzon angalia huduma ambzo zna faida...hii n kwa ajili ya kuleta mzunguko mzuri
Duka likisimama na kukua sasa ndipo utaweka na zile znazochukua mda mrefu kutoka
Just duka co mtaji wa kuanza nao....bali ni wew muuzaji...ht kama ukianza na billion 1 muuzaji ukiwa weak litafirisika ndan ya wiki
Just...
kama n bachelor weka mapenz pemben
Tumia lugha nzuri kwa wateja(usiseme kitu hakipo...sema kimekuishia...ahidi kuwa utaleta...ht km hutaleta)
Jenga mazoea na wateja ila yasizidi(mazoea kwenye biashara hupelekea mikopo)
Pia kaa mbali na wanawke hasa wake za watu(wengi huleta mazoea lkn jitahidi kuwaepuka.....hii ni sababu kuu ya maduka mengi kufa)
Epuka mikopo..(usikopeshe...na kama ukishndwa weka limit kuwa mwsho ni 500....na iwe kwa wateja waaminifu tu)
Huruma weka pemben..(binadam hua wana majaribu usiruhusu huruma ikutawale....hata kama waweza kmsaidia jizuie maan itakuponza)
Iheshim hela ya dukani....(ikitoka nje iwe n kama unarudisha chenji au unanunua bidhaa...usimpe mtu hela ya biashara ht km akisema ataleta baada ya dakika 2...binadam akiwa na shda huongea ahadi nyingi sana)
Mwisho napenda kusema kuwa hakuna biashara nzuri kama ile uloikuuza kwa mtaji mdogo...utaiheshim....utakuwa makini...na pia utaogopa kufirisika maana unajua hali ilivyo ukiwa umefirisika
Hpo gharama hasa ni frem...ila hapo kwenye duka ni wew mwenyew....!!mtaji wa kwanza kabisa ni wew....then hela inafuata....ila ni vema ukianza na mil.1...na tafuta frem ndogo ya wastan
Sent using Jamii Forums mobile app
5. KuhongaChanzo kikuu cha maduka mengi kufilisika ni
1. Kodi kubwa ya fremu
2. Gharama za maisha (maana mwenye duka pia ni binadam na ana familia pia kama amepanga chumba ana kodi ya kulipa)
3. Kodi kubwa ya Serikali (wengi huangushwa na hili)
4. MIKOPO dukani (marafiki, ndugu na majirani)
Schoolboy nawe unauza rejareja?5. Kuhonga
6. Mizinga kutoka kwa ndugu na jamaa
Mimi nanunua rejareja, uko wapi nije ninunue?Schoolboy nawe unauza rejareja?
Hujanijibu!Mimi nanunua rejareja, uko wapi nije ninunue?
Still unafanya hii biashara Ndugu tushauriane?Mimi wateja wamepungua sana yaani mauzo yapo chini ya elfu 50 kutoka zaidi ya kilo 100 nifanyeje niongeze wateja vitu vinadoda dukani
Sent using Jamii Forums mobile app
Hama don't force kuna expire date ume expire kaji update sehemu nyingineMimi wateja wamepungua sana yaani mauzo yapo chini ya elfu 50 kutoka zaidi ya kilo 100 nifanyeje niongeze wateja vitu vinadoda dukani
Sent using Jamii Forums mobile app