Kabla hujaenda alibaba umewahi kwenda maduka ya jumla ya hivyo vitu kwa hapa Tanzaia?
Umejaribu kuuza ?
Unajua changamoto zake ni zipi na zipi?
Chukua ushauri huu acha kuruka hatua.
Tafuta suppliers kwa hapa Tanzania kama ni kariakoo kisha chukua mzigo kidogo, ukaone ugumu na urahisi wa soko, ukiona biashara ina uelekeo mzuri na inakua kwa kasi, ndio uanze kufikiria huko alimama sijui alibaba.
Kingine urahisi wa bei unapumbaza, hivyo vitu unavyoona vya dolar moja inategemea unamuuzia nani, kama unawazuia wanachuo wenzio lawama unatafuta, zile usb cables na chargers wanauza wamachinga nadhani unajua quality zao, na watu wanaowauzia ni wa njiani wapitaji, kikifa mtu kurudisha ni ngumu.