T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Mkuu umekosa hata picha ya hotel yako, weka hata ya baa tuone maids tuje kukuungisha.... si unajua kivutio Cha baa ni wauzaji!Nchi yetu watu wanaotupenda hatuwajui na watu wanaotuchukia hawatufahamu
Thread in a nutshell[emoji993]
Mwaka 2019 ni mwaka ambao niseme ulikua mwaka wa matatizo mengi sana,ni mwaka ambao nilikua naonekana sio kitu kabisa hapa duniani,ni mwaka ambao nilisalitiwa mpaka na rafiki zangu wakatembea na mke wangu kwa kumlaghai na pesa
Ulikua mwaka wa majito,mwaka wa kuteseka,hakuna rangi ambayo sikuiona na nilikua na miaka 21 tu ndugu zangu waliniona sifai kwa kua sina pesa,nimefilisika hata wale waliokua walinipenda kumbe walikua wananinafkia tu
Siku moja nikiwa namawazo maeneo ya kirumba nikiwa natembea tembea sina kitu mfukuno,mke wangu ameshaondoka kodi zimebaki wiki mbili iishe
Nikaketi chini kalibu na mlango wa kuingilia uwanja wa ccm kirumba nikashika kichwa nisijui nini cha kufanya maisha yamekua magumu akatokea Dada poa mmoja akiwa anahitaji huduma ili nimlipe pesa
Badae kidogo akaniuliza mbona unamawazo sana nika msimulia maisha yangu na changamoto mpaka hapo nlipofika nimekaa
Aisee sitamsahau huyo mdada akatoa noti ya sh 10000 akanipatia huku akiniambia maisha hayataki kulalamika lalamika ila ni kutafuta hela tu
Nikatoka hapo nikaenda kupata chakula sababu nlikua sijala kabisa chakula cha 1000 nikabakiza 9000 wakati naludi nyumbani nikawa nawaza hii 9000 ndio baba ndio mama niifanyie nini ili niweze kuishi
Ndipo likaja wazo la kulangua chenga za mkaa na kuziuza kwenye nyumba za watu
Nikaanza kuokota mifuko ile ya kununulia chakula na nikaanza kununua mkaa wa 5000 kisha naufunga kwenye mifuko nausambaza kwenye nyumba za watu
Aisee mwanzo ulikua mgumu sana lakini baada ya miezi 3 nilikua tayari nimefikisha mtaji wa 50000 nikiwa nimeshafahamika na wateja wengi
Nikawa navuka naenda kamanga nalangua gunia kwa 35000 nakuja nalifunga kwenye mifuko nauza aisee nimefanya hio kazi kwa mwaka mmoja mpaka sasa navyosema nina milikia Mpesa,nina hotel ambayo nimeajili wapishi na grocery ndogo ambapo pia na mtaji wangu pia umekuzwa na biashara ya forex
Kwa hio vijana wwnzangu tusizalau kazi huwezi kujua ni kazi gani itakayokutoa kwenye wimbi la umaskini mpaka uchumi wa katiView attachment 2113158
Nitumie basi buku 10 nifate njia za jamaa hapo nami ndani ya mwaka nije nimiliki hoteli jaman😂😂😂😂😂😂😂😂😂 hio noma kweli maana sukar haifui dafu
Yani buku 10 utegemee ikutoe😅 hio bora ukanunulie pedi tu na chupi mpya!Nitumie basi buku 10 nifate njia za jamaa hapo nami ndani ya mwaka nije nimiliki hoteli jaman😂😂😂
Aki nakuahidi utakua unakula bure kila ukija
Acha kunikatisha tamaa bana😂😂Yani buku 10 utegemee ikutoe😅 hio bora ukanunulie pedi tu na chupi mpya!
Chenga za mkaa zitakufanya uishie kuliwa kimasihara kwenye mageto ya wajuba!
Motivesheno spika huyo alishakuja na ngonjera za bitcoin akadai Forex haiamini leo hii anadai imemtoa kimaso masoAcha kunikatisha tamaa bana😂😂
Mbona motiveshno spika kafanikiwa au kwavile ye ni ME
Mjini hapa broMotivesheno spika huyo alishakuja na ngonjera za bitcoin akadai Forex haiamini leo hii anadai imemtoa kimaso maso
Mkuu sas mbona unamuharbia jamaa biashara yake...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]Mnaotaka kujifunza biashara ya Forex njooni huku kuna kijana aliyebobea atawafundisha na kuwapa mbinu bure! [emoji16][emoji16][emoji16]
Amini kwamba😅 wacha tuone!Mjini hapa bro
Hata kwenye umotivesheno spika bado hajakomaa. Huwezi tu ukakurupuka from nowhere eti Forex imekutajirisha. Anaijua Forex huyu? Mwaka wa tatu huu nahangaika nayo na nimesoma mavitabu ya kila aina na kuchukua madarasa ya wataalamu kabisa tena wa nje ya nchi lakini bado nikizubaa tu nakula za uso. Huyu jamaa tapeli!Motivesheno spika huyo alishakuja na ngonjera za bitcoin akadai Forex haiamini leo hii anadai imemtoa kimaso maso
Motivesheno spika huyo alishakuja na ngonjera za bitcoin akadai Forex haiamini leo hii anadai imemtoa kimaso maso
Ushaniwakilisha kuhoji.View attachment 2113239
We jamaa bana.
Kwa mwaka mmoja tu umeweza kujenga hoteli kwa biashara hiyo? Au unamaanisha mkahawa?
Forex umejifunza lini na kwa muda gani mpaka ukaimudu vizuri na kuifanya kuwa sehemu muhimu ya kukuingizia kipato?
Hata kama lengo lako ni kututia moyo sisi vijana tunaohangaika na ajira lakini njia uliyopita wewe ni ya ghafla mno. Labda kuna mambo umetuficha. Yote kwa yote hongera sana kwa kutajirika [emoji122][emoji122][emoji122]
Umesahau alikuja na uzi wa kununua nyoka koboko[emoji23]Motivesheno spika huyo alishakuja na ngonjera za bitcoin akadai Forex haiamini leo hii anadai imemtoa kimaso maso
Hahahahaha jamaa alinunua hadi nyoka ila wapi!Umesahau alikuja na uzi wa kununua nyoka koboko[emoji23]