Biashara ya fedheha iliyonitoa kwenye umasikini

Biashara ya fedheha iliyonitoa kwenye umasikini

Huyu tangu atangaze anatafuta mtaalamu wa kompyuta ili watengeneze blockchain platform na atamlipa 350,000 kwa mwenzi ndio nikajua uelewa wako ni mdogo. Watu kama nyie JF inabidi isiwe sehemu ya amani kwenu mbaki ukouko IG.

Huyu hana hela lakini tambo kibao. Ningekuwa nina roho ya kitapeli nisingekuwa mjinga hivi. Kila uzi anakuwa anafanya kazi tofauti, leo kasema hoteli na magunia ila nyuzi nyingine anasema vitu tofauti labda kitu cha Fx ndio kinabaki. Wazazi wako kama wapo ni wa kulaumiwa, hawakulea mtu katika maadili wamekuza tapeli na inaonekana elimu yako ni ndogo.
 
Nchi yetu watu wanaotupenda hatuwajui na watu wanaotuchukia hawatufahamu

Thread in a nutshell[emoji993]

Mwaka 2019 ni mwaka ambao niseme ulikua mwaka wa matatizo mengi sana,ni mwaka ambao nilikua naonekana sio kitu kabisa hapa duniani,ni mwaka ambao nilisalitiwa mpaka na rafiki zangu wakatembea na mke wangu kwa kumlaghai na pesa

Ulikua mwaka wa majito,mwaka wa kuteseka,hakuna rangi ambayo sikuiona na nilikua na miaka 21 tu ndugu zangu waliniona sifai kwa kua sina pesa,nimefilisika hata wale waliokua walinipenda kumbe walikua wananinafkia tu

Siku moja nikiwa namawazo maeneo ya kirumba nikiwa natembea tembea sina kitu mfukuno,mke wangu ameshaondoka kodi zimebaki wiki mbili iishe

Nikaketi chini kalibu na mlango wa kuingilia uwanja wa ccm kirumba nikashika kichwa nisijui nini cha kufanya maisha yamekua magumu akatokea Dada poa mmoja akiwa anahitaji huduma ili nimlipe pesa

Badae kidogo akaniuliza mbona unamawazo sana nika msimulia maisha yangu na changamoto mpaka hapo nlipofika nimekaa

Aisee sitamsahau huyo mdada akatoa noti ya sh 10000 akanipatia huku akiniambia maisha hayataki kulalamika lalamika ila ni kutafuta hela tu

Nikatoka hapo nikaenda kupata chakula sababu nlikua sijala kabisa chakula cha 1000 nikabakiza 9000 wakati naludi nyumbani nikawa nawaza hii 9000 ndio baba ndio mama niifanyie nini ili niweze kuishi

Ndipo likaja wazo la kulangua chenga za mkaa na kuziuza kwenye nyumba za watu
Nikaanza kuokota mifuko ile ya kununulia chakula na nikaanza kununua mkaa wa 5000 kisha naufunga kwenye mifuko nausambaza kwenye nyumba za watu

Aisee mwanzo ulikua mgumu sana lakini baada ya miezi 3 nilikua tayari nimefikisha mtaji wa 50000 nikiwa nimeshafahamika na wateja wengi

Nikawa navuka naenda kamanga nalangua gunia kwa 35000 nakuja nalifunga kwenye mifuko nauza aisee nimefanya hio kazi kwa mwaka mmoja mpaka sasa navyosema nina milikia Mpesa,nina hotel ambayo nimeajili wapishi na grocery ndogo ambapo pia na mtaji wangu pia umekuzwa na biashara ya forex

Kwa hio vijana wwnzangu tusizalau kazi huwezi kujua ni kazi gani itakayokutoa kwenye wimbi la umaskini mpaka uchumi wa katiView attachment 2113158
Mkuu umekosa hata picha ya hotel yako, weka hata ya baa tuone maids tuje kukuungisha.... si unajua kivutio Cha baa ni wauzaji!
 
Nitumie basi buku 10 nifate njia za jamaa hapo nami ndani ya mwaka nije nimiliki hoteli jaman😂😂😂
Aki nakuahidi utakua unakula bure kila ukija
Yani buku 10 utegemee ikutoe😅 hio bora ukanunulie pedi tu na chupi mpya!

Chenga za mkaa zitakufanya uishie kuliwa kimasihara kwenye mageto ya wajuba!
 
Motivesheno spika huyo alishakuja na ngonjera za bitcoin akadai Forex haiamini leo hii anadai imemtoa kimaso maso
Hata kwenye umotivesheno spika bado hajakomaa. Huwezi tu ukakurupuka from nowhere eti Forex imekutajirisha. Anaijua Forex huyu? Mwaka wa tatu huu nahangaika nayo na nimesoma mavitabu ya kila aina na kuchukua madarasa ya wataalamu kabisa tena wa nje ya nchi lakini bado nikizubaa tu nakula za uso. Huyu jamaa tapeli!
 
Motivesheno spika huyo alishakuja na ngonjera za bitcoin akadai Forex haiamini leo hii anadai imemtoa kimaso maso


Jamaa muongo kweli halafu hata kumbukumbu hana[emoji16][emoji16][emoji16]
 
View attachment 2113239

We jamaa bana.

Kwa mwaka mmoja tu umeweza kujenga hoteli kwa biashara hiyo? Au unamaanisha mkahawa?

Forex umejifunza lini na kwa muda gani mpaka ukaimudu vizuri na kuifanya kuwa sehemu muhimu ya kukuingizia kipato?

Hata kama lengo lako ni kututia moyo sisi vijana tunaohangaika na ajira lakini njia uliyopita wewe ni ya ghafla mno. Labda kuna mambo umetuficha. Yote kwa yote hongera sana kwa kutajirika [emoji122][emoji122][emoji122]
Ushaniwakilisha kuhoji.

Ahsante mh mjumbe!
 
Huyu ni ontorio aliyechangamka amezaliwa upya[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom