Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili gari silipandi ng'ooooooNchi yetu watu wanaotupenda hatuwajui na watu wanaotuchukia hawatufahamu
Thread in a nutshell[emoji993]
Mwaka 2019 ni mwaka ambao niseme ulikua mwaka wa matatizo mengi sana,ni mwaka ambao nilikua naonekana sio kitu kabisa hapa duniani,ni mwaka ambao nilisalitiwa mpaka na rafiki zangu wakatembea na mke wangu kwa kumlaghai na pesa
Ulikua mwaka wa majito,mwaka wa kuteseka,hakuna rangi ambayo sikuiona na nilikua na miaka 21 tu ndugu zangu waliniona sifai kwa kua sina pesa,nimefilisika hata wale waliokua walinipenda kumbe walikua wananinafkia tu
Siku moja nikiwa namawazo maeneo ya kirumba nikiwa natembea tembea sina kitu mfukuno,mke wangu ameshaondoka kodi zimebaki wiki mbili iishe
Nikaketi chini kalibu na mlango wa kuingilia uwanja wa ccm kirumba nikashika kichwa nisijui nini cha kufanya maisha yamekua magumu akatokea Dada poa mmoja akiwa anahitaji huduma ili nimlipe pesa
Badae kidogo akaniuliza mbona unamawazo sana nika msimulia maisha yangu na changamoto mpaka hapo nlipofika nimekaa
Aisee sitamsahau huyo mdada akatoa noti ya sh 10000 akanipatia huku akiniambia maisha hayataki kulalamika lalamika ila ni kutafuta hela tu
Nikatoka hapo nikaenda kupata chakula sababu nlikua sijala kabisa chakula cha 1000 nikabakiza 9000 wakati naludi nyumbani nikawa nawaza hii 9000 ndio baba ndio mama niifanyie nini ili niweze kuishi
Ndipo likaja wazo la kulangua chenga za mkaa na kuziuza kwenye nyumba za watu
Nikaanza kuokota mifuko ile ya kununulia chakula na nikaanza kununua mkaa wa 5000 kisha naufunga kwenye mifuko nausambaza kwenye nyumba za watu
Aisee mwanzo ulikua mgumu sana lakini baada ya miezi 3 nilikua tayari nimefikisha mtaji wa 50000 nikiwa nimeshafahamika na wateja wengi
Nikawa navuka naenda kamanga nalangua gunia kwa 35000 nakuja nalifunga kwenye mifuko nauza aisee nimefanya hio kazi kwa mwaka mmoja mpaka sasa navyosema nina milikia Mpesa,nina hotel ambayo nimeajili wapishi na grocery ndogo ambapo pia na mtaji wangu pia umekuzwa na biashara ya forex
Kwa hio vijana wwnzangu tusizalau kazi huwezi kujua ni kazi gani itakayokutoa kwenye wimbi la umaskini mpaka uchumi wa katiView attachment 2113158
Dah jf usipokuwa makini unaweza jiona wewe mzembe watu wanatoka kila siku kwa vitu vya kawaida, kumbe ni mastori ya townForex ilivyofilisi maduka yangu mawili ya nguo
Daaaaah "Asie sikia la mkuu huvunjika guu" na "kusikia kwa kenge mpaka masikio yatoke damu" "Ulafi ulimponza mzee fisi"[emoji24][emoji24] Thread in a nutshell[emoji993] ____________________________ OK ngoja tuanze thread [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Nijambo la kufurahisha sana kuona...www.jamiiforums.com
Jamaa muongo kweli halafu hata kumbukumbu hana[emoji16][emoji16][emoji16]
Inabidi sasa mwelewa kuwa jamaa anamiliki biashara za kila aina kwa jina lingine ni conglomerateHahahahaha jamaa alinunua hadi nyoka ila wapi!
Bwana eeenh😆😆😆kwaio mtaji wa buku tano tena chenji ya mama ntilie ndo imekutoa kimaisha???. Ivi wengine tunakwama wapi haibooo..🤣🤣🤣Yani watu wanawekeza mamilioni ya pesa huku wakirejesha well below 10% ROI kwa mwezi afu nyie mnakuja na mapicha picha haya🚮🚮Anyways kila mtu na hustle zake, ila usichukue tu hela za wanyonge kwa kutaka kuwauzia strategy zako nyuma ya pazia.Nchi yetu watu wanaotupenda hatuwajui na watu wanaotuchukia hawatufahamu
Thread in a nutshell[emoji993]
Siyo wabishi mkuu. Ukieleza kitu eleza tu vizuri watu wajifunze na kukuhongeresha siyo unadanganya waziwazi. Hustle za kweli zinajulikana tu mbona? Siyo leo unasema eti Forex imekutajirisha within a year na hukuwa na mtaji halafu uzi wako uliopita umeelezea jinsi Forex hiyo hiyo ilivyokufilisi. Mkanganyiko eeeh!?Ila watu wanabisha bure, hakuna kinachoshindikana mbona hata mm nilianzaga na mtaji wa elfu 5 kuuza makande kwa kuunga unga njia za masoko nazojua mpaka kufikia kupata faida ya 30k Kila siku
Asante kwa taarifaDogo naona wewe bado mpya sana humu Jeiefu....
Hio forex ilikuja humu toka kipindi wewe bado unachapwa viboko shuleni na hadi leo hakuna aliyekuja na Success story zaidi ya Ontario (SirJeff) ambae nae ni tapeli tu kwa baadhi ya watu..
Acha kufanya vijana waone maisha ni rahisi hvo kwa kauli kama za kudownload pesa