Biashara ya Fresh Foods

Biashara ya Fresh Foods

mapiki

Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
20
Reaction score
3
Nina mpango wa kuanzisha biashara ya fresh foods (samaki wabichi kama sato, sangara, migebuka na sea foods, kuku, nyama ya ng'ombe na mbuzi) Morogoro. Nataka iwe modern. Naomba wazoefu wa biashara hii wanipe mawazo, ujuzi, n.k. jinsi ya kufanya biashara hii. Asanteni wadau.
 
mbona naona umevichanganya kwa ujumla sio kila kimoja kinauzwa kivyake,kwa mfano bucha ya nyama,duka la samaki wabichi etc,wacha tusubiri wajuvi watatujuza
 
  • Kwanini unataka kufanya hii biashara na sio nyingine (ni nini cha nyongeza kwako kutofautiana na competition)?
  • Je kuna soko uliloshaliona huko ulipo lenye mahitaji haya na kama lipo bei zake zikoje?
  • Je unajua sehemu ya kupata hizo bidhaa kwa bei nzuri ili uweze kuuza kwa bei kama za hapo ulipo au chini ya hapo na wewe kupata faida ?
Ukijibu maswali hayo hapo juu kinachofuata ni mtelemko, na hata kama competition ipo kubwa wewe unaweza ukatoa offer ya kuwakatia watu kabisa nyama na kuwatengenezea samaki ili kuwavutia wateja.

Pia unaweza kwenda vijijini na kununua kuku kwa bei rahisi na kuwachinja na kuwasambaza kwenye migahawa na mama ntilie, au samaki kununua kwa wavuvi kuwatengeneza na kuwalangua kwa wanunuzi. Pia kumbuka hii ni biashara ya vitu vya kuharibika kwahio customer base inayoeleweka ni muhimu
 
Back
Top Bottom