Biashara ya genge inalipa sana kinachokwamisha watu ni kuwekeza mtaji mdogo sana

Naja naja

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
747
Reaction score
1,454
Biashara kuuza genge ni biashara moja nzuri sana. Kinachofanya watu wengi wasifanikiwe ni ile kuwekeza mtaji mdogo sana.

Imagine mtu anaanzisha biashara ya genge kwa mtaji wa elfu 80 sasa mtu kama huyu kutoboa kwenye hii biashara ni ngumu.

Biashara yoyote ukitaka upate mafanikio usiifanye kwa kubahatisha wala kuogopa kupata hasara, kuogopa kupata hasara ndiyo hasara yenyewe hiyo.

Biashara ukiiweka katika muonekano wa kuvutia macho ya wateja ni rahisi sana kufanikiwa.

Ukiliweka genge lako kwa muonekano wa hali duni basi tegemea kupata wateja wa hali duni, ila ukiliweka kwa muonekano classic tegemea kupata wateja classic - wateja ambao kwa mara moja wanaweza hata kununua vitu vya elfu 50 kwa mkupuo.

Sasa cha msingi wekeza angalau mtaji wa laki 5, jenga genge katika muonekano wa kisasa; usijenga kakibanda tu ili mradi bidhaa zako zipate mahala pa kuhifadhiwa.

01deb9d5472925f7b18c2ffebd52a087.jpeg
 
Hapo kwenye banda unaweza ukaongeza huduma nyingine ndogo ndogo kama vile kuuza vocha, au Tigo pesa/Mpesa.
 
Naelewa mkuu mimi mwenyewe nimetokea hukohuko.

Alafu raha ya genge unakula chakula chenye mlo kamili kwa bei sawa na bure kila iitwapo leo.
 
Ila ukae ukijua genge lina changamoto yake tena kubwa kama hujawahi kuifanya hiyo biashala utaona ni rahisi sana kutoboa ila kwa sie tuliosota na hiyo biashala mpk tumetoboa, tunajua ugumu wake.
 
Ugumu upo wapi chief?
Unajua biashala ya genge kuna msimu huwa vitu vinapnda kwa mfano msimu huu ni wa vitunguu kupanda bei na kuna msimu nyanya huwa zinapanda bei kiasi kwamba hata ukinunua haikupi faida lazima iwe inakula kiasi flani ulichoingiza kwenye nyanya na nyanya ndio kila kitu kwenye genge ila yote kwa yote ukijituma genge linakutoa kama nitapata mda nitatoa story fupi kuhusu mimi mana mi nilianza kuuza genge nina miaka 13 baada ya kumaliza la saba
 
mliofanya tunaomba changamoto ili tuweze kwenda sawa

Mkuu changamoto hazifanani kt ya mtu na mtu na njia za utatuzi hazifanani kikubwa kuwa na nia na kuwa mbunifu ktk utatuzi wa changamoto.
Hiyo biashara inalipa kama utapata sehemu sahihi na ukauza bidhaa sahihi kwa walengwa.
 
"Uduni wa genge ndio wingi wa wateja" hiyo ndio siri Watanzania wengi wa uswahilini wanapenda kupata huduma katika sehemu duni huwa wanahofia kuwa sehemu classic basi na gharama ni juu, kuna mtu alishawahi kuleta uzi humu kuwa wakati hajaboresha hoteli yake alikuwa anapata wateja wengi,aliporogwa kurekebisha na kuboresha hiyo hotel wateja wote walikimbia,AKILI KUMKICHWA!
 
Unajua biashala ya genge kuna msimu huwa vitu vinapnda kwa mfano msimu huu ni wa vitunguu kupanda bei na kuna msimu nyanya huwa zinapanda bei kiasi kwamba hata ukinunua haikupi faida lazima iwe inakula kiasi flani ulichoingiza kwenye nyanya na nyanya ndio kila kitu kwenye genge ila yote kwa yote ukijituma genge linakutoa kama nitapata mda nitatoa story fupi kuhusu mimi mana mi nilianza kuuza genge nina miaka 13 baada ya kumaliza la saba
Chief mwezi wa ngapi nyanya huwa zinapanda bei?
 
"Uduni wa genge ndio wingi wa wateja" hiyo ndio siri Watanzania wengi wa uswahilini wanapenda kupata huduma katika sehemu duni huwa wanahofia kuwa sehemu classic basi na gharama ni juu, kuna mtu alishawahi kuleta uzi humu kuwa wakati hajaboresha hoteli yake alikuwa anapata wateja wengi,aliporogwa kurekebisha na kuboresha hiyo hotel wateja wote walikimbia,AKILI KUMKICHWA!
Hii kama ikitokea ni kwa muda mfupi tu kiongozi, overtime watu watafahamu kwamba gharama hazijapanda na watarudi.Pia unapoboresha ni vyema ukaweka matangazo ya huduma unayotoa au bidhaa unayouza na bei yake ili wateja wajue kama kuna mabadiliko au la.
 
Nangoja apa mzee ushuhuda

Back
Top Bottom