Biashara ya genge ni lazima kuwa na TIN na leseni ya biashara?

liq

Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
61
Reaction score
43
Habari wadau,naomba ushauri kidogo,ukiwa mfano umekodisha frame na ukaamua kufungua au kuweka bidhaa za matunda,spices na mbogamboga,Je ni vibali gani utahitajika uwe navyo?msaada kwa anayejua tafadhali
 
biashara yyte ambayo inalipa kodi lazima iwe na TIN na LESENI.

hizo spices na vegatables kama ni za packages kuna umuhimu wa kuwatembelea TFDA watakupa muongozo.
 
biashara yyte ambayo inalipa kodi lazima iwe na TIN na LESENI.

hizo spices na vegatables kama ni za packages kuna umuhimu wa kuwatembelea TFDA watakupa muongozo.
nimekupata mdau,ila kiufupi ni genge sema linakua kwenye frame na sio kibanda au meza kama wengi wanavyofanya.hapo ndio nastack kidogo kua je nini hasa chahitajika?maana mamlaka zetu wakishaona upo kwenye frame basi lazima ulipe.muongozo tafadhali
 
nimekupata mdau,ila kiufupi ni genge sema linakua kwenye frame na sio kibanda au meza kama wengi wanavyofanya.hapo ndio nastack kidogo kua je nini hasa chahitajika?maana mamlaka zetu wakishaona upo kwenye frame basi lazima ulipe.muongozo tafadhali
hapo lazima TIN na LESENI uwe navyo...maana si unalipia kodi ya frame, hata wale wa magenge wanatakiwa kuwa navyo ila si Tanzania tena unaijua.
 
Habari wadau,naomba ushauri kidogo,ukiwa mfano umekodisha frame na ukaamua kufungua au kuweka bidhaa za matunda,spices na mbogamboga,Je ni vibali gani utahitajika uwe navyo?msaada kwa anayejua tafadhali
1. Suala la TIN
Mkuu kuwa na TIN inatakiwa kwa raia wote pasipo kujali wafanya biashara au laa. Matumizi ya TIN utaona ya biashara na isiyo ya biashara. Kwa mantiki hii bhasi unalazimika kuwa na TIN tena ya biashara

2. Kulipa kodi TRA
Malipo ya kodi inategemea vlvl kutokana na mauzo yako. (Kwa kuzingatia wa kifungu cha 35 cha Sheria ya usimamizi wa kodi ktk utunzaji wa kumbukumbu), mauzo yasiyozidi mil 4 kwa mwaka haustahili kulipa kodi hata kama umepanga ktk fremu hiyo ya biashara

3. Je ntakata leseni ya biashara?
Laa hasha huwezi kukata leseni ya biashara ila utaangukia katika kundi la biashara ndogondogo za kulipa ushuru. Hivyo anapopita mtoza ushuru wa eneo lako tafadhali toa ushirikiano.

Tafadhali
Sijasema hustahili kuwa na TIN, unatakiwa kuwa na TIN tena ya biashara lakini kiwango cha kulipa kodi utakuwa haujafika kama mauzo hayazidi mil 4 kwa mwaka
 
Kwa maelezo haya bila shaka wewe ni afsa huko kwa wakusanya kodi. Asante kwa elimu.
Ila Magenge yaliyo mengi hesabu ya milioni 4 yanafikisha kwa mwaka. Maana ili ufikoshe milion 4 inatakiwa uuze wastani wa sh. 11,000 kwa siku.

Hivyo jamaa kama ni muaminifu itabidi alipe kodi tu na leseni awe nayo. Nasema kama ni muaminifu kwa sababu tunapokuja TRA kukadiliwa kodi huwa mnauliza unauza sh. ngapi kwa siku, hivyo kama anauza elf 50 na akadanganya anauza elf 8 tayar kashasalimika kwenye kulipa kodi.
 
mkuu kumbuka kiasi utakachoenda kadiriwa na hao TRA ni mtaji wako mara mbili
tujifunze kukwepa kodi ili tuwe na maeendel, huwezi endelea Kwa kulipa kodi bali utaendaleza taifa tu
 
Ni kweli Mkuu
Kama mauzo yanazidi mil 4 kwa mwaka na hana kumbukumbu za mauzo, basi ataangukia katika mauzo kati ya mil 4 hadi 7.5 ambapo kodi yake atatakiwa kulipa kiasi cha shilingi 150,000 kwa mwaka. Yaani atalipa ktk awamu nne za Machi, Juni, Septemba na Disemba. Ila angekywa muwazi zaidi kusema mtaji wake.
Mara nyingine mtaji huweza kusaidia kumweka katika kundi lipi la malipo ya kodi
 
mkuu kumbuka kiasi utakachoenda kadiriwa na hao TRA ni mtaji wako mara mbili
tujifunze kukwepa kodi ili tuwe na maeendel, huwezi endelea Kwa kulipa kodi bali utaendaleza taifa tu
Mkuu hili sio kweli
Kodi inatozwa kwa asilimia 30 kutokana na faida ghafi (mapato) unayoipata baada ya kufanya hesabu za mwaka mzima. Na haichajiwi kutokana na mtaji
 
mkuu kumbuka kiasi utakachoenda kadiriwa na hao TRA ni mtaji wako mara mbili
tujifunze kukwepa kodi ili tuwe na maeendel, huwezi endelea Kwa kulipa kodi bali utaendaleza taifa tu
Kwa Maelezo yake... it's very likely that,,,majadirio ya biashara yake yata-base kwenye mauzo badala ya mtaji!!!
 
Kwa Maelezo yake... it's very likely that,,,majadirio ya biashara yake yata-base kwenye mauzo badala ya mtaji!!!
Ni kweli hili lina sura hii. Lkn kwa sasa suala la TIN na malipo ya kodi lipo hivi. Jamaa akaombe TIN ya biashara na atapewa TAX CLEARANCE CERTIFICATE, ambapo ndani ya siku 90 atatkiwa kwenda kulipa kodi. Sasa anachofanya ataandika barua kuwa mauzo yake ni madogo.
Haya mambo unajua kama sisi Watz tungekuwa na mazoea ya kuwatumia washauri wa kodi ingekuwa changamoto kama hizi hazitupi taabu. Mara nyingine TRA huwa wanakuwa na semina za mambo ya kodi kwa wafanyabiashara, lkn walengwa wagumu kutokea hadi basi. Hadi unatafakari namna gani asaidiwe kutokana na changamoto hizi
 
Tufanyie kazi hii kitu kama tuna madeni ya miaka ya nyuma au haujaepeleka makadirio ya miezi ya Machi na Juni 2018
 
wote nimewaelewa kabisa na asanteni kwa mchango wenu,swala ni hivi,kinachosemekana ni kua Unaenda serikali za mitaa unatoa taarifa ili wakutambue,kisha pale kuna watu wa TFDA itabidi uzungumze nao kwa kua unaenda kuuza chakula then kuna form unajaza na kwenda kulipia bank around 50,000/- then hapo hapo serikali za mtaa utahitajika kuchukua form na kujaza kwa ajili ya kwenda kufanya medical check up na tsh 5000/- then unaenda TRA na TIN yako kama unayo na kupata tax clearance certfct then unaenda manispaa kuomba leseni ya biashara ambayo kwa mujibu wanasema 70,000/-.sasa hayo ndio mambo niliyokutana nayo kwa wadau.je kuna ukweli wowote?hapo sijajua ila nimeona bora kushare na wadau hapa mtujuze zaidi.
 
kwa maana hiyo mdau ninachotakiwa kuwa nacho ni Tin tu,then ushuru watakuja kupitia wenyewe wanapopita?je suala la anayeuza kama nimemuweka kijana lazima apime afya?also swala la kuongea na watu wa TFDA na kulipia 50,000/-limekaaje?pole maswali mengi kidogo ila ndio kutaka kuelewa,asante
 
1. Suala la TFDA
Labda ungeweka sawa suala la bidhaa unazouza. Je ni "processed food" au ni "fresh food" kikiwa katika hali unayonunua kutoka sokoni? Kama ni chakula ambacho unakifanyia mabadiliko ikiwa pamoja na kufanya "packaging" hapo TFDA watahusika. Lakini kama ni chakula cha kawaida unachonunua na kuuza kikiwa katika mfumo uleule hakuna haja
2. Suala la afya
Ukiangalia hata ktk fomu ya maombi ya leseni kipengele cha 11(ii) kinaweka wazi suala la afya kuwa lazima eneo likaguliwe usafi na kuhakikiwa na Afisa Afya wa eneo husika. Ambapo hutoa maoni yake. Lakini halizingatiwi sana kupata leseni ila tu maafisa afya hupita kuhakiki usafi wa maeneo ya biashara. Hakuna sehemu yenye uhitaji wa TFDA kwa biashara za genge, foodshop. Ingekuwa unauza nyama hii ni lazima ungetakiwa kuwa na kibali cha TFDA
3. Kulipa kodi
Kwa biashara yako utalazimika kulipa kodi japo kwa kuzingatia mfumo wa makisio ya kodi ya kipato (income per year) na sio mauzo (turnover). Huwezi ukaachwa usilipe kodi. Ina maana utalipa kodi ktk mfumo kama mtu binafsi. Kwa mfano ukasema mapato yako ni 540,000 kodi itakuwa 17,100+20% ya mapato yanayozidi 360,000 =53,100 kwa mwaka. (ukiwa TRA utaona kwa haraka zaidi atumia tax table na kukwambia).
4. Leseni ya biashara
Leseni ya biashara nakumbuka ndogo ilianzia sh 81,000 kwa biashara ndogo kabisa. Sasa sijajua kwa eneo lipi, hii kwa kumbukumbu ilikuwa hapa Dar na biashara ilikuwa ya kuuza ktk vizimba vyakula kama clips et al
 
Usijali Mkuu maswali yako ni kheri kwa sote katika kupeana elimu
Naomba unijibu haya maswali kwa upande wa kodi
1. Mtaji wako kiasi gani?
2. Mauzo yako kiasi gani?
3. Mapato unavyoona kwa mwaka unaweza kupata kiasi gani?

Suala la afya
Kama nilivyojibu pale juu, ushauri mzuri utapata kutoka kwa Afisa afya wa eneo husika ambapo ataangalia suala la kiafya likihusiana na vyakula unavyouza na mazingira. Kwa genge la kawaida hushauriwa kusumamia usafi lkn kama bidhaa za nyama ndiyo LAZIMA UTAAMBIWA TFDA wanahusika

Vlvl kutokana na mtaji kuwa mdogo sana wa wengi wanaofanya biashara za genge ndiyo maana huwa wanauchuna tu hafuatilii TIN wala leseni zaidi hulipa ushuru na vlvl kupewa mwongozo wa Afisa Afya "mtaani maarufu sana kama bibi afya" kwa zamani kutokana na wengi wao walikuwa wanawake
 
Ukishakuwa na ofisi (frame) lazima uwe na leseni na leseni haitolewi bila kuwa na TIN ambayo ndani yake ina Tax Clearance! Baada ya hapo watapita tena watu wa MSM kwa ajili ya ushuru, kisha TFDA - usalama wa chakula na uhifadhi, WMA lazima wakague vipimo na hao wote wanadai ada/tozo!

TRA pamoja ya kodi ya mapato utalipia pia kodi ya zuio kwa ile kodi ya nyumba.
 
Leseni inakulazimu pale unataka kutanua biashara yako kwa mkopo wa benki! Hupewi mkopo wa biashara bila up-to-date license! Mind you bila TIN na TC hupewi leseni
 
Leseni inakulazimu pale unataka kutanua biashara yako kwa mkopo wa benki! Hupewi mkopo wa biashara bila up-to-date license! Mind you bila TIN na TC hupewi leseni
Hii uliyosema wewe tayari ni condition nyingine sio inayojadiliwa hapa. Nadhami hii ungeanzisha uzi wa Mahitaji ya taasisi za fedha katika kutoa mikopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…