KENGE 01
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 1,705
- 4,217
Na kenge,
Hakuna biashara ngeni lakini unaweza kuifanya bila kuwa na mtaji mkubwa na bila taaluma kama IT au ufundi gereji kama wengi wanavyodhani.
UTAFANYAJE?
Wizi wa vyombo ni tatizo kote duniani sasa kama ni Jobless na unatafta pakuanzia unaweza kutafta mtaji wa kuanzia LAKI 5 NA KUENDELEA.Kisha uagize vifaa hivi ni tudude tudogo ukiingia Alibana,Amazon utazikuta zipo aina nyingi vilevile kwa bei tofauti.Lakini kwakuanzia utanunua za kuanzia $35 kushuka chini.
Sasa baada ya kuagiza Fungua ukurasa kwenye Social Media achana na umbea/Udaku anza kutafuta wateja wenye magari,Shawishi watu wenye magari ya usafiri wape elimu namna zinavyofanya kazi na umuhimu wa kufunga GPS hasa magari ya biashara.
UTAWAELEZA
~Kwanza kifaa kinaunganishwa na simu,Laptop n.k ili kupata taarifa ya chombo.
~Inaweza kujua gari lilipo muda wowote(Location)
~Inatoa taarifa ya mafuta,engine temprature n.k
~Nyingine zinauwezo wa kuzima gari hata kama lipo mbali(au limeibiwa)
UTAJIONGEZA!
Sasa watu wengi hudhani GPS ni kwaajili ya magari na pikipiki tu lakini device hizi zinaweza kupachikwa kwenye TV,Laptop, na vifaa vingine vya kieletroniki kwahiyo kazi yako itakua ni kushawishi watu faida za kuweka GpS kwenye vifaa vyao.
CHANGAMOTO
Kama teknilojia inavyokua basi na Wezi wanaongeza mbinu za kivita hivyo baadhi ya Wezi wanatumia kifaa maalumu cha kudetect uwepo wa GPS kisha wanaitoa na kuitupilia mbali na chombo/gari linaibwa na hutolipata
Pia wengi huiweka sehemu moja(Kwenye AC) hii ni kwasababu ya kukosa maarifa kwaio wezi wabobezi wanajua GPS nyingi zinawekwa kwenye AC,ikumbukwe device hii inabidi ifichwe sehemu ambayo ni ngumu kuonekana kwenye gari,pikipiki n.k
MUHIMU!
Mambo ya kuzingatia ni angalau uelewe mambo ya wiring(Umeme wa magari) Pia uwe unajua kutumia smartphone aina zote utakutana na wateja wana iphone nawewe ushazoea Tecno,Infinix, UTAJIBEBA MBONA ,Nisikutishe tamaa ukishapachika GPS, App utazikuta playstore nyingi tu na Appstore vilevile kwaio uhitaji kuwa IT(japo ni muhimu kujua vifaa vinavyofanya kazi)
PLAN INAKUA HIVI
~Unamtaji wa 500k
~Ukiagiza device 10 au 20 za $50-$60
~Device moja utauza 150k na kama mteja atahitaji umfungie utatoza 30k ya ufundi jumla 180k mpaka 200k
~Ukipata wateja 5 mtaji utarudi na faida
NB:Biashara rahisi kuiongelea,ingia uone moto wake (Raha ya ngoma,Ingia uicheze)lakini penye nia,pana njia..
Wako mtiifu,
Balozi wa Jobless
KENGE 01
NAWASILISHA