Hisa za TBL na TCC unaweza kuzipata kwenye soko la hisa la Dar es salaam kupitia kwa mawakala. Makampuni haya ni miongoni mwa makampuni yaliyojisajili kwenye soko la hisa la Dar es salaam. Kwa kuwa umeamua kuwekeza katika soko la hisa ni vizuri ukajiogezea maarifa juu ya jambo hili kwa kusoma vitabu, majalida na magazeti. Kutembelea tovuti mbalimbali na kuwa karibu na watu walio katika tasnia hiyo. Hata mbuyu ulianza kama mchicha, kila la kheri.