Biashara ya hisa na faida zake

Biashara ya hisa na faida zake

Gwaje

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
299
Reaction score
85
Salama waungwana?

Nimenunua share za CRDB miezi sita iliyopita. Naona kama zimepanda kwa Tshs 150 toka niliponunua. Je , biashara ya hisa hufanyikaje kwa faida zaidi? Je, niziuze na kununua nyingine au faida nitapataje sasa?
 
mkuu tofauti kati ya buying price na market price ya sasa ndo capital gain yenyewe hiyo faida yako, market timing iko hivi buy shares when price is low and sell shares when price is low( nunua hisaa bei ikiwa chini afu ziuze bei ikiwa juu)
 
Kuna namna nyingi za kufanya biashara ya hisa inategemea wewe umejielekeza wapi. Suala la biashara hii linahitaji ujuzi na weledi. Wapo wanaonunua hisa kwa kuvizia pindi zinaposhuka bei kwa lengo la kuuza wakati bei itakapoimalika. Chaguzi nyingi katika nchi za Afrika hasa kusini mwa jangwa la Sahara huwa hazitabiriki. Kipindi kuelekea uchaguzi na wakati wa uchaguzi fedha hushuka thamani na masoko ya hisa hudorora. Wapo watu huamua kununua hisa kipindi hiki ili soko likiimalika auze hisa zake. Kuna watu hawavutiwi na riba zinazotolewa na benki kwa watu wanaotunza hela zao hasa kwenye akaunti ya muda Maalum, badala ya kuweza fedha huko huamua kununua hisa ili muda wa kuzihitaji hizo fedha huuza hisa zao. Kuna watu wenye uelewa mpana juu ya mambo ya fedha na hisa wenye uwezo wa kung'amua hali ya soko la hisa mbeleni. Hawa hujielekeza kununua hisa kwenye makampuni ambayo leo yanaonekana ya kawaida au dhaifu Lakini kwa sababu ya menejimenti bora na Uwekezaji mzuri yatafanya vizuri. Pengine ni vyema ukasema wewe katika biashara hii ya hisa umelenga kufanya biashara ya hisa kwa mtazamo upi?
 
Hata mimi nilinunua hisa 1000 CRDB wiki iliyopita,lakini mimi malengo yangu nije niziuze baadae saana maana nimezinunua kwa ajili ya kulipia ada watoto baada ya kuangalia utendaji kazi wa CRDB kwa miaka 3 iliyopita.
mwezi huu nataka ninunue za NMB na DCB.
JE hisa za TCC na TBL ninaweza kuzipata kwa uhakika?
 
Hisa za TBL na TCC unaweza kuzipata kwenye soko la hisa la Dar es salaam kupitia kwa mawakala. Makampuni haya ni miongoni mwa makampuni yaliyojisajili kwenye soko la hisa la Dar es salaam. Kwa kuwa umeamua kuwekeza katika soko la hisa ni vizuri ukajiogezea maarifa juu ya jambo hili kwa kusoma vitabu, majalida na magazeti. Kutembelea tovuti mbalimbali na kuwa karibu na watu walio katika tasnia hiyo. Hata mbuyu ulianza kama mchicha, kila la kheri.
 
Back
Top Bottom