Biashara ya kambakochi, China

jrmpya

Member
Joined
Dec 3, 2014
Posts
74
Reaction score
58
Habari za asubuhi ndugu zangu.

Hongereni kwa kazi na majukumu ya kila siku, Moja ya shauku yangu ya siku nyingi sana ni kusafirisha samaki aina ya kambakochi kwenda China maana ndio soko na uhitaji mkubwa wa kamba kochi ulipo.

Hivyo basi kwa neema ya Mungu natarajia kuanza kupeleka samaki hao mwezi wa nne mwaka huu, na nimeanza kufanya utafiti wa upatikanaji wake pamoja na bei zake pale Feri, na nimefahamu kuwa kilo moja ya kamba aliye hai ni elfu tisini na aliyekufa ni elfu thelathini.

Biashara hii mimi sijawahi fanya wala sina uzoefu nayo. Hivyo kukiwa kuna yeyote anaifanya biashara hii au anaufahamu wa namna moja au nyingine kuhusiana na biashara hii ya kambakochi, naomba mchango wenu katika hili kupitia habari hii ili wengi wanufaike ili nao wapate kuona fursa na kuchukua hatua ya mafanikio.

Asanteni sana, karibuni sana.
 
Ndio aina gani ya samaki? na je wanatumika kama malighafi ya kutengenezea nini? Ikiwezekana tupe scientific/english name
 
English name: Lobster, ni kwa ajiri ya kula!!!
 

Attachments

  • 1423072739221.jpg
    71.9 KB · Views: 746
Kamba kochi biashara inayohitaji umakini ktk kuhakikisha hawafi lazima uwe na kisima chako na mashine ya kuzungusha hayo Maji ya kisima na ukitaka kwa wingi nenda Mtwara na Msumbiji
 
wanapatikana kwa kiwango cha mpaka kuexport kweli?...mi naona hawatoshelezi hata mahitaji ya ndani, kama unajua pa kuwapata kwa wingi unaweza kuchukua tender hata mahotelini tu ukapata faida nzuri, biashara ikishasimama na ukawa na uzoefu nayo inakuwa rahisi zaidi kwako kuexport.
 
Hii biashara bwana..kuna jamaa alinipigia simu ya kutaka kunitapeli eti tufanye hii biashara..akanipa namba ya mzee anayevua hao samaki niongee nae kuhusu kupata mzigo,nikampigia kwa namba tofauti akajichanganya mwenyewe..nikamwambia tafuta njia nyingine ya kupata hela hii imebaunsi Bro..
 
Asante sana chinga boy, ushauri nitaufanyia kazi!!!!
 

Kupatikana wanapatikana tena kwa wingi!!! Wazo lako la kusupply kwenye mahotel ya hapahapa kwanza nalo ni zuri nitalifanyia kazi!! Asante sana Rene Jr!!!!
 
hao wanakujua walikuwa wanakutengeneza wakupige tu, kama una shida na aina zote za kamba na samaki wengine si unaanzia ferry? na soko si unatafuta kwa walaji wakubwa? na unalipa pesa unapewa samaki unaondoka zako?
 
Mbona bei kubwa sana hiyo...fuata kwenye chanzo upate faida kubwa..mimi nadeal na crabs ...

Kwenye chanzo ni wap!!? Na bei unayoifahamu wewe ni ipi!!? Vipi kuhusu hao crabs!!! Wanapatikana vipi na soko lake likoje!!!?
 

Hiyo bei ya kununulia itakutia hasara, china huyo samaki anauzwa kwa bei ya chini zaidi,
 
Kwanini uliachana nayo? , naomba unipe uzoefu wako wa hii biashara A to Z!!!

Changamoto gani zaidi ya upatikanaji, packaging,bei, na realiable customers mkuu. na zaidi managing your expenses.
 
Kwanini uliachana nayo? , naomba unipe uzoefu wako wa hii biashara A to Z!!!

I left kwa sababu sikuwa na control nayo, I just invested alafu zikaanza longo longo za kibongo, I quit.
 
English name: Lobster, ni kwa ajiri ya kula!!!

Alafu niisha changanya na Kaa, hawa bei yake iko juu kidogo, lakini ukinunua kwa tisini itakupa shida sana kwenye faida. iko juu ila haivuki $50
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…