jrmpya
Member
- Dec 3, 2014
- 74
- 58
Habari za asubuhi ndugu zangu.
Hongereni kwa kazi na majukumu ya kila siku, Moja ya shauku yangu ya siku nyingi sana ni kusafirisha samaki aina ya kambakochi kwenda China maana ndio soko na uhitaji mkubwa wa kamba kochi ulipo.
Hivyo basi kwa neema ya Mungu natarajia kuanza kupeleka samaki hao mwezi wa nne mwaka huu, na nimeanza kufanya utafiti wa upatikanaji wake pamoja na bei zake pale Feri, na nimefahamu kuwa kilo moja ya kamba aliye hai ni elfu tisini na aliyekufa ni elfu thelathini.
Biashara hii mimi sijawahi fanya wala sina uzoefu nayo. Hivyo kukiwa kuna yeyote anaifanya biashara hii au anaufahamu wa namna moja au nyingine kuhusiana na biashara hii ya kambakochi, naomba mchango wenu katika hili kupitia habari hii ili wengi wanufaike ili nao wapate kuona fursa na kuchukua hatua ya mafanikio.
Asanteni sana, karibuni sana.