JR mpya, kwa kuanzia wanaitwa kamba koche (lobster) na sio kambakochi!, katika sea food, huyu ndio the most expensive sea food, akifuatiwa na kamba, (prone).Kwenye bandiko lako, umeleta hoja tatu za msingi, 1. Shauku yako ya siku nyingi kusafirisha kwenda China kwa sababu ndiko kwenye soko kubwa.2. Biashara hii hujawahi kufanya na huna uzoefu nayo.3. Unaomba msaada kwa wanaojua.Kabla sijakusaidia, naomba maelezo yako kidogo hiyo shauku yako ya siku nyingi ilitokana na nini kwa biashara ambayo huijui wala hujawahi kuifanya, kiasi cha kupanga hadi lini biashara inaanza?!. Nilidhani ulipata shauku kutokana na sababu fulani, na hizo sababu ndizo zikakuelekeza China ndio soko kubwa, sasa utaanzaje biashara ambayo huijui, huna uzoefu nayo, nilidhani shauku yako ulipata kwa wenye uzoefu?!.Mimi sijui lolote kuhusu biashara hii zaidi ya kujua kamba wanapatikana kwa wingi delta ya Rufiji.Kiendo cha kuwa na shauku ndio mambo yote, mengine yote yatafuatia, ila ulipaswa kabla hujaamua kuanza biashara fulani, ulipaswa kuanza na homework yako na sio kupanga hadi tarehe ndio unakuja hapa jf kutoa homework!. Kwa maoni yangu, ndugu yangu wewe bado sana ila penye nia pana njia!.Pasco