Biashara ya 'kiboya' lakini yenye pesa ndefu!

Mr.genius

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2012
Posts
1,374
Reaction score
1,201
Kwenye jiji lenye mzunguko mkubwa wa hela kama Dar-Es-Salaam,biashara ni nyingi sana. Iwe kubwa ama ndogo;kila siku watu hubuni biashara au kazi mpya ambazo kwa namna moja ama nyengine huwaingizia kipato. Kuna wauza maji,kuna Dobi,kuna wakusanya uchafu,kuna wanaotoa huduma za usafi kama kusafisha vyoo nakadhalika. Hizi ni kati ya ajira ndogo ambazo baadhi yetu huzitumia kuendesha maisha yao na familia zao kwa ujumla. Zipo biashara au ajira nyingi ambazo zimeshafanywa na nyengine zitafatia kufanywa zikipata watendaji. Leo nakushirikisha kwenye wazo hili la ajira ambalo labda mimi na wewe tunaojiona watanashati hatuwezi kufanya,ila kuna kijana mtaani itamfaa.

Je,umewahi kufikiria utoaji wa huduma ya uoshaji vyombo na vifaa vitumikavyo jikoni,kula na kupikia;kwa nyumba za wanaume ambao hawajaoa au zisizo na wafanyakazi. Ni wazo moja la 'kiboya' sana ila niamini mimi,likipata mtendaji lina hela nyingi. Mimi ni moja ya vijana ambao naishi mwenyewe tu,sijaowa;napika kila siku ila kuosha vyombo itanichukua wiki moja au zaidi. Na sio mimi tu,labda niseme marafiki zangu wa kiume karibu wote wapo hivyo. Umewahi kuwaza kama kuna watu wanatoa huduma za kufua majumbani,vyuoni au kusafisha vyoo na mazingira kwa kila mwisho wa juma,kwanini ishindikane kutoa huduma ya kufanya usafi wa vyombo. Na bila shaka kazi hii huweza fanywa kila siku kulingana na wingi wa wateja wako. Nitakupa mfano:mtaa kama Sinza una vijana wengi ambao huishi wenyewe,kuna ambao wanapika na ambao hununua vyakula kwenye migahawa ambao bila shaka idadi yao huweza kuwa kubwa kiasi. Ukiwa na uwezo wa kupata vijana 20 (ambapo kwenye nyumba moja huweza kuwa na vijana watatu au zaidi kulingana na walivyopanga) na ukawa unawapa huduma ya kuwaoshea vyombo kila baada ya siku mbili,na tufanye kila kijana mmoja atalipia 1,000 au 1,500 kulingana na wingi wa vyombo;kwa mwezi utakuwa na uhakika wa kukusanya 300,000 mpaka 450,000 au zaidi. Huo ni mfano tu.

Kila biashara huwa na changamoto zake,haimanishi kwamba biashara au ajira hii itaenda sawa sawa kama ilivyoandikwa hapa. Kuna wenye maarifa zaidi yangu huenda wakachukua wazo hili na kuliongezea vitu fulani ikawa kubwa zaidi na ikatoa ajira kubwa zaidi,pia sio mbaya ikiwa hivyo. Kuna ambao wataenda mbali zaidi na kuhudumia kwenye migahawa midogo,ni vizuri zaidi kujiongeza. Na labda kama hatufahamu ni kuwa,kwenye mahoteli makubwa kuna vijana mahususi wa kuosha vyombo tu,kwa nchi zilizoendelea wana vifaa kama ‘dish washer’ ambayo hutumika kuosha vyombo. Kwetu Africa unaweza kuwa ni wewe na ukajiita au ofisi yako ukaiita ‘The Walking Dish Washer’, ‘ Mr Dish Washer’, ‘Utensils Cleaner’ nakadhalika; nimetumia mifano ya kiingereza sababu wengi wetu huamini kutumia lugha hiyo huvutia wateja zaidi au huduma yako ni ya ‘kisomi. Na usifikirie labda utahitaji mtaji mkubwa sana kulifanya hili,kiosheo chako kimoja tu kitatosha kuanzia. Sabuni,maji au mahitaji ya ziada atatoa mhudumiwa.

Niwakumbushe tu kuwa hili ni wazo,na huenda lisikufae wewe likamfaa kijana wa hapo mtaani kwako ambaye hana ajira yoyote kwa sasa na anaweza kulifanyia kazi. Napokea ushauri na maoni yako kwenye hili,lengo ni kupunguza umaskini.

Shukran.
 
First of all, naomba nitoe credits for somebody known as @classmateTz (on twitter) kuptia mtandao wa Medium aliiweka hii post. Sabab sharing is caring nami nikaona si vibaya nikiileta hii idea hapa kwenu wana jukwaa tutapata nafasi ya kui discuss na kumsaidia yoyote anaetaka kuifanya!

Here we go, ur welcome...

Asante mkuu...!
 
Si salama kabisa, watu wana wivu na chuki zisizo na sababu, unaweza sababisha msiba kwako bila kujua au ukawekewa vitu vya magendo ukajikuta unamalizia maisha yako mahakamani. Binadamu wamejaa chuki na husda zisizo na sababu.
 
Inatakiwa ifanywe na watu ambao ni vetted, verified and background checked people
Si salama kabisa, watu wana wivu na chuki zisizo na sababu, unaweza sababisha msiba kwako bila kujua au ukawekewa vitu vya magendo ukajikuta unamalizia maisha yako mahakamani. Binadamu wamejaa chuki na husda zisizo na sababu.
 
Wazo zuri sana tatizo dunia ya leo uaminifu hakuna.
 
Na wanaume walivyo wavivu kwenye ya sector vyombo.
Mtu haezi ajiri wa kufua na wa vyombo
 
Kama ulivyosema ni biashara ya kiboya. Ni kweli ni biashara ya kiboya,ni kiboya ksbb huwezi kupata hata vijana wa5 tu wa kuwaoshea hivyo vyombo kila siku, utakuwa wewe mwanaume,nakuhakikishia. Sikukutashi tamaa kwa ulichofikiria,lakini utapoteza muda tu. Kwanza vijana wengi hawapiki. Ksbb gharama ya kupika na kula kwa magenge ni karibu sawa au inaweza kuwa gharama kupika. Kwenye migawaha. Huwezi kupata migahawa zaidi ya miwili,nayo watataka wakuone uko hapo hapo kila wakati,wakumiliki. Hili wazo ni bovu sana
 
Mbona hi ipo muda Sana...Hawa wanaopita majumbani kufua wakikuta na vyombo wanaosha na nyumba wanapiga usafi na wewe ukitaka kuogeshwa unaogeshwa pia.
Hata ukitaka na huduma ya ziada wanatoa pia
 
Kama ulivyosema ni biashara ya kiboya. Ni kweli ni biashara ya kiboya,ni kiboya ksbb huwezi kupata hata vijana wa5 tu wa kuwaoshea hivyo vyombo kila siku, utakuwa wewe mwanaume,nakuhakikishia. Sikukutashi tamaa kwa ulichofikiria,lakini utapoteza muda tu. Kwanza vijana wengi hawapiki. Ksbb gharama ya kupika na kula kwa magenge ni karibu sawa au inaweza kuwa gharama kupika. Kwenye migawaha. Huwezi kupata migahawa zaidi ya miwili,nayo watataka wakuone uko hapo hapo kila wakati,wakumiliki. Hili wazo ni bovu sana
Tena wanaume wa Dar mwendo wa Chips Mayaiii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama ulivyosema ni biashara ya kiboya. Ni kweli ni biashara ya kiboya,ni kiboya ksbb huwezi kupata hata vijana wa5 tu wa kuwaoshea hivyo vyombo kila siku, utakuwa wewe mwanaume,nakuhakikishia. Sikukutashi tamaa kwa ulichofikiria,lakini utapoteza muda tu. Kwanza vijana wengi hawapiki. Ksbb gharama ya kupika na kula kwa magenge ni karibu sawa au inaweza kuwa gharama kupika. Kwenye migawaha. Huwezi kupata migahawa zaidi ya miwili,nayo watataka wakuone uko hapo hapo kila wakati,wakumiliki. Hili wazo ni bovu sana
Haiwezekani kabisa kupita pita kwenye nyumba za watu si ataonekana ni mwizi lakini pia ata akipata kazi hayo mapato atakusanyaje mana watu inabidi awafuate
 
Back
Top Bottom