Mr.genius
JF-Expert Member
- Feb 20, 2012
- 1,374
- 1,201
Kwenye jiji lenye mzunguko mkubwa wa hela kama Dar-Es-Salaam,biashara ni nyingi sana. Iwe kubwa ama ndogo;kila siku watu hubuni biashara au kazi mpya ambazo kwa namna moja ama nyengine huwaingizia kipato. Kuna wauza maji,kuna Dobi,kuna wakusanya uchafu,kuna wanaotoa huduma za usafi kama kusafisha vyoo nakadhalika. Hizi ni kati ya ajira ndogo ambazo baadhi yetu huzitumia kuendesha maisha yao na familia zao kwa ujumla. Zipo biashara au ajira nyingi ambazo zimeshafanywa na nyengine zitafatia kufanywa zikipata watendaji. Leo nakushirikisha kwenye wazo hili la ajira ambalo labda mimi na wewe tunaojiona watanashati hatuwezi kufanya,ila kuna kijana mtaani itamfaa.
Je,umewahi kufikiria utoaji wa huduma ya uoshaji vyombo na vifaa vitumikavyo jikoni,kula na kupikia;kwa nyumba za wanaume ambao hawajaoa au zisizo na wafanyakazi. Ni wazo moja la 'kiboya' sana ila niamini mimi,likipata mtendaji lina hela nyingi. Mimi ni moja ya vijana ambao naishi mwenyewe tu,sijaowa;napika kila siku ila kuosha vyombo itanichukua wiki moja au zaidi. Na sio mimi tu,labda niseme marafiki zangu wa kiume karibu wote wapo hivyo. Umewahi kuwaza kama kuna watu wanatoa huduma za kufua majumbani,vyuoni au kusafisha vyoo na mazingira kwa kila mwisho wa juma,kwanini ishindikane kutoa huduma ya kufanya usafi wa vyombo. Na bila shaka kazi hii huweza fanywa kila siku kulingana na wingi wa wateja wako. Nitakupa mfano:mtaa kama Sinza una vijana wengi ambao huishi wenyewe,kuna ambao wanapika na ambao hununua vyakula kwenye migahawa ambao bila shaka idadi yao huweza kuwa kubwa kiasi. Ukiwa na uwezo wa kupata vijana 20 (ambapo kwenye nyumba moja huweza kuwa na vijana watatu au zaidi kulingana na walivyopanga) na ukawa unawapa huduma ya kuwaoshea vyombo kila baada ya siku mbili,na tufanye kila kijana mmoja atalipia 1,000 au 1,500 kulingana na wingi wa vyombo;kwa mwezi utakuwa na uhakika wa kukusanya 300,000 mpaka 450,000 au zaidi. Huo ni mfano tu.
Kila biashara huwa na changamoto zake,haimanishi kwamba biashara au ajira hii itaenda sawa sawa kama ilivyoandikwa hapa. Kuna wenye maarifa zaidi yangu huenda wakachukua wazo hili na kuliongezea vitu fulani ikawa kubwa zaidi na ikatoa ajira kubwa zaidi,pia sio mbaya ikiwa hivyo. Kuna ambao wataenda mbali zaidi na kuhudumia kwenye migahawa midogo,ni vizuri zaidi kujiongeza. Na labda kama hatufahamu ni kuwa,kwenye mahoteli makubwa kuna vijana mahususi wa kuosha vyombo tu,kwa nchi zilizoendelea wana vifaa kama ‘dish washer’ ambayo hutumika kuosha vyombo. Kwetu Africa unaweza kuwa ni wewe na ukajiita au ofisi yako ukaiita ‘The Walking Dish Washer’, ‘ Mr Dish Washer’, ‘Utensils Cleaner’ nakadhalika; nimetumia mifano ya kiingereza sababu wengi wetu huamini kutumia lugha hiyo huvutia wateja zaidi au huduma yako ni ya ‘kisomi. Na usifikirie labda utahitaji mtaji mkubwa sana kulifanya hili,kiosheo chako kimoja tu kitatosha kuanzia. Sabuni,maji au mahitaji ya ziada atatoa mhudumiwa.
Niwakumbushe tu kuwa hili ni wazo,na huenda lisikufae wewe likamfaa kijana wa hapo mtaani kwako ambaye hana ajira yoyote kwa sasa na anaweza kulifanyia kazi. Napokea ushauri na maoni yako kwenye hili,lengo ni kupunguza umaskini.
Shukran.