Biashara ya Kuchakata na Kufungasha Unga wa Mahindi (Sembe na Dona)

Hello JF,
Nina wazo hilo la biashara, nataka nimwezeshe mdogo wangu afanye;

Pendekezo liwe Unga Wa Dona ukichanywa na aidha Unga Wa mtama au Ngano halisi. Kisha nitafunga au pack ktk ujazo Wa kuanzia kg 1 hadi 15kg.

Masoko tarajiwa ni Supermarkets, mini markets, maduka kawaida, migahawa, hotelini na mashuleni nk.

Hili ni wazo tu, naomba ushauri wako Wa nyongeza ktk hili. Na pia unayependa wazo hili Jaribu, Tanzania bado kubwa.

Karibu.
 
Mmmmhhh...Mr consultant, Upo kwenye data collection process nini? Hahahaa...napita tu.
 
Kamanda wa ukweli, rudi hapa kabla hujafika mbali.
 

Mkuu tunaomba mrejesho umefikia wapi na hii mega project
 
This is the best idea,,,for those who are expert in this business could you give us the challenges and how to overcome them
 
Ndugu. Kila biashara ina siri zake. Wàsagaji wa nafaka wamewahi kuibuka wakiwa na mashine nzuri na miundombini bora ya usambazaji, lakini wengi hoi au wamefilisika. Kampuni ya Bhakhresa, Scandnavia na moja iko Kibaha zote hoi kwenye usagaji wa mahindi.

Nyumba ya pazia la kila buashara inayokua kwa spidi kuna siri kubwa.
 
Hongera kwa hatua uliyofikia mkuu, hivi kwa wajuzi gunia la kilo 100 la mahindi kwa wastani huwa linatoa unga wa sembe kilo ngapi na pumba kilo ngapi?
 
Hongera kwa hatua uliyofikia mkuu, hivi kwa wajuzi gunia la kilo 100 la mahindi kwa wastani huwa linatoa unga wa sembe kilo ngapi na pumba kilo ngapi??
Kutegemeana na mahindi, unaweza pata uwiano wa Unga 50 % mpaka 70% inayobaki pumba. Yani unga kilo 50 mpaka 70 na pumba kilo 30 mpaka 50. Mahindi ya ubora wa wastani yanatakiwa kukupa at least 65kg na pumba 30 kg.
 
Mdau GreenCity nimevutiwa na mchango wako juu ya biashara hii. Je kwa mfumo huo bado vibali vya TBS na TFDA vinahitajika? Na leseni ya biashara ya aina hii inaweza kuchukua muda gani kuipata? Umeongea pia juu ya nembo ya mtu mwingine unadhani nahitajika kuongea na mhusika juu ya kutumia nembo yake?

Mm nina mashine tayari ya kusanga na kukoboa .ila naona kuna changamoto ya kupata vibali vya ruhusa ya uzalishaji toka kwa TBS na TFDA . Ndio maana nimeona ww una weza nipa nwanga zaidi kwa plan B ya kutumia mashine za kulupia.
 
Mm ninaifanya hii kitu kwa muda kidogo sasa ngoja niwape ujanja kidogo ingawa bado nakuza mtaji maana ndo kwanza nimetoka chuo

Ninatafuta mahindi vijijini then nayaleta mjini nikifika hapo kuna wafanyabiashara wakubwa ambao tayar wapo kwe soko la unga kwa muda mrefu na wana mashine zao ninachokifanya mm nikifika na mahindi yanga ninayasimamia yanasagwa na kufungwa kwe mifuko ya ujazo wa kg 25 then ninaiuzwa kwa jumla kwa mmiliki wa mashine then naiuza na pumba then narud vijini kusaka mahindi

Ni biashara nzur tena sana since nimeianza sijui kitu kinachoitwa hasara

Kwa wenye mitaji mikubwa unaweza tafuta soko lako mwenyewe la unga na hata kufungua mashine zako na ikakulipa zaidi

Nadhani nimetoa ABC kidogo kwa maelezo zaid 0659902425

Changamoto kubwa kwe kwe hii biashara ni variations ya bei za mahindi
 
Labda ufanye kama huyu kuepuka usumbufu wa TBS na TFDA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…