Hivi nyie mmekuja Dar lini?
Hakuna kitu hapo mtaibiwa mjini.
Hata Samaki ukivmua unamuonyesha kwanza chambo kabla ya kumvua.
Namna ya kumpika anajua mpishi mwenyewe
Nyie mngekuwa mnataka maelezo zaidi ya biashara hizi,wasiliana na KENICE POOL Company.
Watakupeni kila kitu,sio kila kitu kuangalia kwenye upande ambao mtu ana personal interest zake.
Halafu heading eti Tajirika,we umeona nani duniani katajirika na Pool table zaidi ya kupata pesa ya kula na kuendesha familia kwa kiwango cha chini.
Na declare interest kwamba mie ninayo hapa mtaani,na unapata pesa ya kawaida tu ya kupunguza ukali wa maisha.
Na pia kuwa makini maana wapo vijana wanatabia ya kucheza kamari kwa kuwekeana pesa katika mchezo huo,mwisho wa siku ni laana kwa mwenyepool table na wachezaji.
Inalipa zaidi ikiwa nje ya Bar,siku hizi vijana wengi bar wanaenda kuangalia tu bar gani inamadem wazuri basi.Na ukiangalia vijana wengie wanaishia kwenye viroba juu kwa juu,na wenye nazo muda wa kupindisha viuno kwenye pool table sio kivile wengi kama vile wameisha uchoka.
Ilikuwa zamani wakati mchezo unaingia na hakuna pa kuchezea zaidi ya bara ndio maana watu wakaona kwamba lazima uweke bar.
Ila ukweli ni kwamba hata mazingira ya kawaida unalipa vizuri sana.We muuliza mtu wa Bar akuambie mapato ya miaka ya 2004 hadi 2007 na sasa ni tofauti baada ya mchozo kuzagaa hadi mitaani.
Muhim ni kuangalia sehem yenye utulivu.
Na bora zaidi kuweka sehem ya wazi,mie nilikodi kiwanja cha mtu kwa mkataba kwamba akitaka kujenga naodoka.
Sasa niliweka sakafu chini na bati juu,kisha chini nikaweka tiles za vipande,halafu nikafanya kuigeuza iwe kijiwe cha biashara.
Yaani nauza chipsi,juices,supu,maji bites kibao na mambo mengine.Ili niwe naokota mia mia.
Ila mwanzo ni gharama kidogo ila inalipa kiasi kwa kushirikisha biashara zaidi ya moja.
Naamini sie wote wengi kila mmoja mtaani kuna kiwanja cha mtu hakijajengwa au sehem ya mtu ipo wazi.
Sasa unaweza kumuomba uibadilishe iwe kibiashara zaidi,sio kuweka turubali juu kama uwanja wa fisi.
Sasa ukimuomba mwenye uwanja na ukamuambia dhamira yako basi hakukatalii kabisa,muhim heshim ya mchezo huu ni jinsi unavyoiweka na kuiandaa kwa ujumla.ukiweka kihuni basi wateja wako watakuwa wahuni na ukiiweka kiheshima kidogo basi hata wale wahuni watakuwa wapole na kufuata utaratibu kutokana na mazingira.