GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,651
- 14,337
Ni siku ya jumamosi asubuhi napigiwa simu na jamaa yangu mmoja akitaka kujua ratiba zangu kwa siku hiyo.namwelekeza. ananambia kama sitojali jioni anipitie niende kumsalimia mjomba wake mgonjwa anayeishi kimara.
Well,sikuwa na pingamizi ukichukulia sikuwa na ratiba ya kubana na pia ni siku nyingi sijaonana na omar.anakuja home mida ya saa tisa alasiri...tunaongea mambo kadhaa akitaniana na shemeji yake na baadaye anaomba niruhusiwe kutoka naye kwenda kwa mjomba wake kimara.kawaida ya nyumbani kwangu kama kuna mtu anatoka nami wife hupenda aombwe hasa siku za weekend ili aridhie mimi kutoka na wakati mwingine hukataa kutoa ruhusa.basi huwa sina namna nabaki.
Omar na jamaa zangu nlishawaambia utaratibu huo.anyway najua wakiwa wanakunywa huko hunisema nimewekewa limbwata,namsikiliza mwanamke n.k i dont care.mi ndiye nliyeoa. Nao wanajua wanaendesha vipi nyumba zao.
Tunaondoka na omar akiwa amehidi kunirudisha kabla ya saa tatu.tunafika kimara huko ndani kidogo mbali na barabara.baada ya kupanda milima na kushuka na kona kona kadhaa tunafika mbele ya nyumba moja kubwa mjengo wa zamani.kma sikoi ni ule wa kutoka uganda.
Ni nyumba kubwa sana maana inaonesha kuna familia nyingi pale ndani.sebule na kibaraza vipo wazi barabarani ila upande mwingine kumezungushiwa ukuta na pia kuna geti.
Mimi navua sandals zangu nyeus na omar anavua viatu kibarazani tunaingia ndani kumsalimia mjomba.amelala kibarazani...kutuona anainuka na kutukaribisha akitupa mkono.tunasalimiana naye na baada ya mawili matatu anaita watoto wake.wanakuja mabinti wawili mmoja anavutia sana kwa kweli namtizama na kumeza fundo la mate...halafu natizama kwenye simu yangu screen saver nmemsave mke wangu.naukunyata moyo."mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba"
Basi mjomba anasema tutoke nje tukakae kwenye kibaraza tukipata upepo.mle ndani kuna kelele wengine wakisiliza music na wengine wakiangalia mpira wa miguu kupitia dstv.
Tunaongea maneno kadhaa na mwishowe omar ananitambulisha vizuri kwa mjomba.mjomba amelala kwenye kiti uvivu...huku tukinywa maziwa na karanga za kukaanga anaanza kutusimulia ugonjwa wake.
Anasema miaka kadhaa (akitaja mwaka husika) akiishi ilala alikuwa ni mtu wa dini sana.kwa mujibu wa maneno yake.alipenda sana kusoma...hii ilimfanya asome na mwishowe awe mdadisi sana kwa mambo ya imani.
Anasema alipenda kusoma vitabu mbalimbali mpaka alifikia hatua ya kuwa na maswali mengi sana kwa viongozi wake wa kiimani.alijifunza mengi ikiwepo elimu ya majini.alijifunza na alipenda kujifunza sana.pale ilala kuna sehemu ambayo aliweza pata elimu hiyo na mwishowe alianza hata kusafiri nje ya nchi akianzia na lamu,mombasa na libya.
Alikuwa na bidii sana kila hatua aliyofika alikuwa vizur.alifundishwa pia sanaa za mapigano na kuiva vizuri.anasema alifundishwa namna ya kusoma kitabu kuita jini.na alipofanikiwa siku ya kwanza hakuamini akiwa chumbani peke yake amejifungia.jini lilikuja likaongea naye na kumwondoa hofu kabisa.
Aliendelea na elimu hiyo hata kufikia hatua ya kuoa jini.alipendana sana na hili jini ambalo alikuwa akiliita au likimjia usiku na kufanya naye mapenzi waki enjoy sana. Ingawa alikuwa na mke. Walikubaliana kuwa awe na siku kadhaa za kufanya na mke na pia siku za kufanya nalo yeye .
Maana alishaambiwa mara nyingine huwa majini yanaachanisha ndoa. Wao walikubaliana isingekuwa vyema akae bila mke.anasema aliendelea hivi hadi kufikia hatua ya kuoa mwanaume mwenzie naye awe anafanya naye mapenzi.
Lile jini lilikuwa linampa nguvu ya ajabu ya kufanya mapenzi.akaoa mwanaume mwenzio...shoga na kumpangishia nyumba mitaa flani.alimpenda sana naye akimpa mapenzi kama mwanamke.
Anasema katika hilo alifanikiwa pia kuwa na majini kadhaa ambayo yalikuwa na kazi mbalimbali.ya kudhuru,kuleta pesa n.k. bado aliendelea kupata elimu ya majini.na siku moja akiwa katika mashindano ya kutumia majini na wataalamu wengine aliweza ikausha nazi iliyokuwa bado mbichi kama dafu.akajifunza namna ya kumsomea ngamia kisomo mpaka akalala kuchinjwa bila mushkeli.
Anasema mjomba alii enjoy sana nguvu ya mambo yale.alikuwa na uwezo wa kuua mtu halafu akaliweka jini likazikwe kumbe mhusika mwenyewe amechukuliwa msukule.hivyo anahesabiwa kama amekufa kumbe pale pamelazwa gogo,mgomba au mzoga ambao umevalishwa sura ya jini husika.
Anasema majini yanakunywa damu...na mara nyingi yanapata kwenye ajali.wakati mwingine yanapanda mabasi kama abiria na kumwingia dereva aendeshe hovyo ili kusababisha ajali.abiria wanaweza wakawa wanapiga kelele kumbe yenyewe ndo yanamchochea dereva kuendesha kwa hasira...kuwakomoa abiria wanaoonekana kumfundisha kazi.
Lengo itokee ajali yapate damu.anasema hata barabarani yanaweza weka kituo sehemu ikawa haupiti muda ajali inatokea watu wanamwaga damu.yanakunywa.
Mjomba aliendelea kusimulia visa vyake hivi kwa masikitiko na wakati mwingine majivuno akionesha umwamba aliokuwa nao.aliweza kutabiri aliweza wapatia watu majini ya bahati,kupendwa,mafanikio n.k
Anasema yeye hakuwa akifanya kazi...kwa kufuga majini alikuwa tu anaweza shinda vijiweni na wazee au kuzunguka zunguka tu lakini jioni akaletewa pesa na majini afanye anachotaka. Anasema hili pia alijifunza kwa watu wengi ambao walikuwa wanacheza bao karibia siku nzima pamoja.lakini unakuta mzee huyu anavyoweza kula na kulisha familia yenye watoto wengi na wake kadhaa.
Mjomba ake omar anasema ili pia watu wasiwe na maswali basi akanunua daladala ambayo hiyo ndo ingeonekana kuwa inampatia pesa....
ITAENDELEA.
TAHADHARI:
1. Jina halisi la mhusika nmelificha ila details nyingine kwa watu waliokaa ilala miaka ya nyuma wanaweza wakawa wanazifahamu.sitazitaja.
HADITHI HAIHUSIANI NA DINI YOYOTE HIVYO EPUKA KUSHAMBULIA DINI YANGU AU YA MTU MWINGINE.