Biashara ya kukaanga mihogo

Chum Chakavu

Member
Joined
Oct 19, 2018
Posts
18
Reaction score
22
Habari wana JamiiForums,

Kwa mud wa miezi karibu mitatu sasa nimekua nikiumiza kichwa kuhusu kufanya biashara. Nimefikiria biashara nyingi sana katika kipindi chote hicho ila biashara pekee ambayo imekuja kutawala sana kichwa changu ni biashara ya Chakula.

Jana usiku majira ya saa tisa hivi nilishtuka usinginzi na fikra zikaendelea ila kuna kipindi kuna wazo lilinijia ambalo ni kufungua banda la kukaanga mihogo ambayo nitaiboresha na kuiuza katima mtindo wa chipsi.

Ila hii ntaiboresha zaidi kwa kufungua kama restaurant ambayo itakua ni special kwa kuuza juice za matunda tofauti na mihogo ya kukaanga ambayo nitaikaanga katika ladha tofauti kama vile vannila, garlic, na ladha ya kawaida pamoja na mishkaki na kuku wa kuchoma maarufu kama sekela. Naombeni kuwasilisha wazo langu.

Kwa yeyote mwenye ushauri swali au jambo lolote litakalosaidia kuboresha wazo langu anakaribishwa.

Asanteni sana
 
Hongera mkuu
Umesha fanikisha hilo jambo??
Pia kuhusu radha ikoje boss naomba utaalam
 
Fanya Kile unacho penda kufanya na kile kitakacho kupatia pia Furaha.

Kinacho mata sana ni kiwango cha mapenzi na hicho unacho taka kufanya.
Mmh!! Inahitaji umakin unaweza kupenda fanya biashara fulani ila kutokana na sabab za kibiashara ikawa ngumu kufanya au utaweza fanya kwa hasara
 
Mmh!! Inahitaji umakin unaweza kupenda fanya biashara fulani ila kutokana na sabab za kibiashara ikawa ngumu kufanya au utaweza fanya kwa hasara
Ugumu unatoka wapi wakati ndo unacho penda?

Ugumu unaanza pale unapo fanya kwa sababu umeambiwa inalipa au uliiga tu

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
'To prosper anything , you must first put on its shoes ' Una idea nzuri sana , ila hapo kwenye kuitia flavour mihongo ndo panaponitatiza ,

Mihogo ni chakula cha asili, kuitia atrificial flavour kukatakufanya ujitenge na walaji asili ambao kimsingi ndo tegemeo lako, na badala yake utahangaika kuwashawishi walaji wapya juu ya hivo vikolombwezo vyako , na chances ya kufanikiwa kwenye hiyo idea yako itakuwa ndogo sana.

We boresha kwenye usafi na namna ya kuandaa hiyo mihogo, ila ipike katika namna ambayo inafahamika huku uswahilini kwetu, kuna watu kibao , nikiwemo mimi , ambao tunapenda mihogo ila kupata sehemu sahihi ya kukaa na kula muhogo ni challenge.
 
Asante sana kwa wazo lako. Nalifanyia kazi ndugu yangu
 
Ugumu unatoka wapi wakati ndo unacho penda?

Ugumu unaanza pale unapo fanya kwa sababu umeambiwa inalipa au uliiga tu

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app


Akuna kitu unapenda mkuu hizo theory tu fanya cheku kukutoa kwa muda huwo hivyo boashara yoyote unafungua kwaajiri inalipa na itakutoa na nisawa kwamba unaipenda.

Mimi kichwani nina malengo ya kufanya biashara kibao inamaana kati ya hizo yepi naypipenda
1)Restaurant
2)Uwakala
3)Juice bar
4)Car wash
6)Kilimo
7)Ufugaji
8)Duka la nguo nk

kwahiyo hapo napenda kipi minangalia chochote kitachonitoa, kwahiyo unaamini wanaofanya kazi ya kupakuwa mavi wanapenda, nina mtaji wa 700K itanilimiti kufungua biashara ya pesa hiyo kama kiduka cha CD, nina 6M nitataka Carwash au Restairant nk, nina 1Billion nitafanya Real Estate nk kwahivyo mtaji utakupangia na watu wanaangalia faida mzee, sikweli kwamba muuza duka la rejareja anapenda kuwa kama mfungwa saa 12 asubui hadi 5 usiku ila pesa ndio influencial factor mkuu.
 
Umeongea kitu cha maana boss
Kikubwa ni kuangalia aina ya biashara na eneo unalotaka kufanya biashara pamoja na nguvu ya mtaji
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…