Biashara ya Kukodisha Mitambo Tanzania

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Wajasiriamali Wenzangu
Naomba msaada wenu, nahitaji kuanza biashara ya kukodisha Mitambo yaani niwe na mitambo yangu niwakodishe watu. Lengo la kuweka uzi huu hapa kwenu nikuomba ushauri wa mitambo ipi hasa mngenishauri ndugu yenu niweze kuifanyia kazi, kwa mfano kuna mitambo kama hii
  • Mitambo ya kuchimbia Visima
  • Mitambo ya Kukorogea Zege
  • Folk Lifts
  • Matrekta
  • Kijiko
  • Grader
  • N.k
Nisaidieni Mawazo. je biashara hii italipa? Je ni mitambo ipi naweza kuitumia??
 
Folk Lifts
Inaitajika kwa sehemu kubwa sana hasa kwenye yard ambazo agents wa bandari wanatumia wakati wa kupakia contena uwa zinapatikana kwa shida na ni gharama pia wakati unaingiza mashine iyo itakupa unafuu wa kodi aina mambo mengi
 
Folk Lifts
Inaitajika kwa sehemu kubwa sana hasa kwenye yard ambazo agents wa bandari wanatumia wakati wa kupakia contena uwa zinapatikana kwa shida na ni gharama pia wakati unaingiza mashine iyo itakupa unafuu wa kodi aina mambo mengi
Asante sana sana
 
Grader
hii sio mbaya inalipa pia ila hapa inabidi ujipendekeze sana na watu wa harimashauri ili upate kazi za kukwangua barabara za mitaani uku inalipa maana kukodi grader kwa saa ni kama milioni ivi
 
Una hela sana wewe? Umepata wapi hayo mabilioni ya kununua hayo ma grader hadi uje huku kuomba ushauri kwa makapuku?

Sent from iphone 7 plus
 
Una hela sana wewe? Umepata wapi hayo mabilioni ya kununua hayo ma grader hadi uje huku kuomba ushauri kwa makapuku?

Sent from iphone 7 plus
Duh, haya asante sana Mkuu nimekuelewa. Asante
 
heavy equipments (grader,loader,excavator) inalipa sana. lakini jitahidi uwe na machine nzima kidogo na kwa kushauri kama una mtaji mzuri anza kwa kuwa na Motor Grader au Excavator. kama uko vizuri pia jaribu kufikiria kuwa na Cusher la kokote nayo ni biashara nzuri pia...Kilimo cha kisasa, kwa maana ya kutotegemea mvua bali uwekezaji mkubwa na ikiwezekana mazao ya chakula kama mahindi na mpunga then unakuwa na godown lako unastock. Idea nyingine mkuu ni uvuvi wa samaki baharini kama unaweza kumiliki boti kubwa ya uvuvi (troller), ukawa na refrigerated carrier na cold room sehemu fulani... Binafsi nakosa mtaji mkubwa nashindwa kufanya chochote hapo lakini nina uhakika hutojuta..
 
Mimi sina mtaji ila najua ukiwa na idea sahihi ni mwanzo sahihi wa kupata kitu sahihi pia
 
Good business ila changamoto yake kubwa ni malipo, ukianza usije kuthubutu kukodisha kwa "mali kauli" mtu akulipe ndio achukue mitambo. Local contractors wengi ni matapeli wa kukodi mitambo na pia sio watunzaji wazuri wa mitambo, sometime wako locally sana, unakuta anaanza project bila contract baadae anakosa malipo ya hiyo kazi au GoT inamcheleweshea malipo kwa muda mrefu.
 
Grader n.k zinalipa sanaa mkuu hasa ukipata mgodini naonaga watu wanaopata tenda mgodini wananzaa may be na Dozer tu afu baada ya mwaka yuko vizuri na anaongeza mshine zingine maradufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…