Biashara ya Kukodisha Mitambo Tanzania

Biashara ya Kukodisha Mitambo Tanzania

Wajasiriamali Wenzangu
Naomba msaada wenu, nahitaji kuanza biashara ya kukodisha Mitambo yaani niwe na mitambo yangu niwakodishe watu. Lengo la kuweka uzi huu hapa kwenu nikuomba ushauri wa mitambo ipi hasa mngenishauri ndugu yenu niweze kuifanyia kazi, kwa mfano kuna mitambo kama hii
  • Mitambo ya kuchimbia Visima
  • Mitambo ya Kukorogea Zege
  • Folk Lifts
  • Matrekta
  • Kijiko
  • Grader
  • N.k
Nisaidieni Mawazo. je biashara hii italipa? Je ni mitambo ipi naweza kuitumia??
Njoo pm mzee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una hela sana wewe? Umepata wapi hayo mabilioni ya kununua hayo ma grader hadi uje huku kuomba ushauri kwa makapuku?

Sent from iphone 7 plus
Acha hivo huku hakuna makapuku .makapuku wote wapo MAKAPUKU FORUM ndo mana ilianzishwa kama we upo huku alafu ni kapuku unapoteza muda wako bure wai Makapuku forum kwenye mipasho na vijembe vya kila aina huku ni biashara tuu
 
Wajasiriamali Wenzangu
Naomba msaada wenu, nahitaji kuanza biashara ya kukodisha Mitambo yaani niwe na mitambo yangu niwakodishe watu. Lengo la kuweka uzi huu hapa kwenu nikuomba ushauri wa mitambo ipi hasa mngenishauri ndugu yenu niweze kuifanyia kazi, kwa mfano kuna mitambo kama hii
  • Mitambo ya kuchimbia Visima
  • Mitambo ya Kukorogea Zege
  • Folk Lifts
  • Matrekta
  • Kijiko
  • Grader
  • N.k
Nisaidieni Mawazo. je biashara hii italipa? Je ni mitambo ipi naweza kuitumia??
Fungua kampuni ya kukodisha mitambo km vile crane za ukubwa tofauti pamoja na folk lifts, inalipa vizur na kwa vijijini kukodisha matrekta inalipa pia ila hiyo ni biashara ya msimu
 
Seniors hivi ni mashine gani inatumika kulainisha au kusaga kifusi kama kile akichotumia strabag kwny ujenz wa udart?, ile nayo ni mzuri ukiwa unachimba kifusi na kukisaga en unawauzia contractors wa barabara au hata wateja wadogo wanaojenga nyumba za makazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
matrekta vijijini kwa mjini leta tipper truck 15 cubic metres hujulikana kama mende, kama una mda was kutosha wa kusimamia jaribu kukodi mashamba makubwa utumie matrekta yako kulimia kukodisha hakulipi sana labda kama unalimia watu unalipwa mazao kidogo unaweza songa. Vipi mkubwa una aina gani za trekta
 
Grader
hii sio mbaya inalipa pia ila hapa inabidi ujipendekeze sana na watu wa harimashauri ili upate kazi za kukwangua barabara za mitaani uku inalipa maana kukodi grader kwa saa ni kama milioni ivi
Duhh [emoji15] [emoji15] Kwahiyo kwa masaa 12 ni Milioni 12, acha kuzungumza usiyo yajua. Ingekuwa hivyo kila mfanyabiashara mkubwa angefanya hiyo biashara kwasababu motor grader second hand zipo hapo mantrac ni reconditioned zipo kama mpya. Hiyo bei uliyotaja ni ya siku kwa saa 8.

SIKU LAZIMISHI KUAMINI BAKI NA UBISHI WAKO
 
Wajasiriamali Wenzangu
Naomba msaada wenu, nahitaji kuanza biashara ya kukodisha Mitambo yaani niwe na mitambo yangu niwakodishe watu. Lengo la kuweka uzi huu hapa kwenu nikuomba ushauri wa mitambo ipi hasa mngenishauri ndugu yenu niweze kuifanyia kazi, kwa mfano kuna mitambo kama hii
  • Mitambo ya kuchimbia Visima
  • Mitambo ya Kukorogea Zege
  • Folk Lifts
  • Matrekta
  • Kijiko
  • Grader
  • N.k
Am the civil engineer,kama una mitambo tuabzishe kampuni.pays more
 
SIKU LAZIMISHI KUAMINI BAKI NA UBISHI WAKO
Kweli mwenda wazimu yaani bila aibu unaongea kitu usicho kijua tena kwa kubisha!!...Ipo hivi hakuna Motor Grader,Excavator wala set ya mtambo wa barabara unao kodishwa kwa saa milioni moja.

Motor Grader kiwango cha juu kabisa ni 1.2mil VAT inclusive per day (8hrs) na mitambo mingine ni hivyo hivyo na huwa inashuka mpaka laki 7 kwa Dar (8hrs) kukodi Grader na Excavator.

Jamani kwa tusicho kijua tukubali kuwa wasikilizaji sio kudanganya uma eti kukodi Grader kwa saa milioni 1!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa sasa usifanue biashara ya graders wala excavators sbb hali ya uchumi ni ngumu walio nazo hawana kazi km unaweza nunua forklift au loader truck inayoweza kujibebesha container yenyewe hizo ndio mashine zinapiga kazi sana sasa hv.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pata LOADER (kwa ajiri ya kupakilia magogo au nguzo) peleka Mufindi! Hutajuta!
 
heavy equipments (grader,loader,excavator) inalipa sana. lakini jitahidi uwe na machine nzima kidogo na kwa kushauri kama una mtaji mzuri anza kwa kuwa na Motor Grader au Excavator. kama uko vizuri pia jaribu kufikiria kuwa na Cusher la kokote nayo ni biashara nzuri pia...Kilimo cha kisasa, kwa maana ya kutotegemea mvua bali uwekezaji mkubwa na ikiwezekana mazao ya chakula kama mahindi na mpunga then unakuwa na godown lako unastock. Idea nyingine mkuu ni uvuvi wa samaki baharini kama unaweza kumiliki boti kubwa ya uvuvi (troller), ukawa na refrigerated carrier na cold room sehemu fulani... Binafsi nakosa mtaji mkubwa nashindwa kufanya chochote hapo lakini nina uhakika hutojuta..
Nakuunga Mkono Mkuu samurai hizo Heavy Equipment zinalipa. Uwe na Grader, Excavator ( za Chain pamoja na za Tairi), Trucks za kubebea hiyo Mitambo na Tippers. Hakika utatoka tu!

Sent from my LG-D855 using JamiiForums mobile app
 
Kweli mwenda wazimu yaani bila aibu unaongea kitu usicho kijua tena kwa kubisha!!...Ipo hivi hakuna Motor Grader,Excavator wala set ya mtambo wa barabara unao kodishwa kwa saa milioni moja.

Motor Grader kiwango cha juu kabisa ni 1.2mil VAT inclusive per day (8hrs) na mitambo mingine ni hivyo hivyo na huwa inashuka mpaka laki 7 kwa Dar (8hrs) kukodi Grader na Excavator.

Jamani kwa tusicho kijua tukubali kuwa wasikilizaji sio kudanganya uma eti kukodi Grader kwa saa milioni 1!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua sikuelewi tunabishana nini me na wewe,biashara kila mtu anaifanya anavyo jua mimi nimekwambia ninacho jua nilicho wahi kufanya unalazimishi kiwe uongo una akili kweli ungekuwa una busara ungeniuliza wapi inafanyika sio kubishana,kwani ukiwa uswahilini unanunua karanga pakiti mia lakini kwanini sehemu zingine unanua mpaka mia 5 na kipimo ni kile kile,tumia akili na ukitaka kujifunza usibishane uliza,na usikariri biashara
 
Kweli mwenda wazimu yaani bila aibu unaongea kitu usicho kijua tena kwa kubisha!!...Ipo hivi hakuna Motor Grader,Excavator wala set ya mtambo wa barabara unao kodishwa kwa saa milioni moja.

Motor Grader kiwango cha juu kabisa ni 1.2mil VAT inclusive per day (8hrs) na mitambo mingine ni hivyo hivyo na huwa inashuka mpaka laki 7 kwa Dar (8hrs) kukodi Grader na Excavator.

Jamani kwa tusicho kijua tukubali kuwa wasikilizaji sio kudanganya uma eti kukodi Grader kwa saa milioni 1!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi najua hivi ulibosema. Motograder n.k inakodishwa laki nane kwa siku VAT Inclusive. Huyu anayesema M12 kwa siku sijui kapata wapi

Extend your hand in kindness and offer help to the most in need
 
Back
Top Bottom