Fanya vitu ivi kabla hujaamua kipi ufanye ama ushauri upi ufate;
1. Angalia eneo ulilopo kitu gani kina hitajika zaidi na kwa bei gani (analysis ya soko)
2. Anza na wa nyama kama utaona kuna demand na bei ni nzuri sokoni, utaweza kuwatoa ndani ya miezi miwili mpk minne, kutegemea na aina uliyopendezwa kuifuga... wapo wanaotoka mpk ndani ya wiki 4, ila sikushauri sana kuanza nao.
3. kama unaeneo kubwa la wazi unaweza fuga wa kienyeji... hawa wakipata open space unawalisha kidogo chakula kingine wanajitafutia... ila kuwafugia ndani wanachangamoto kidogo.
4. kwa issue ya wa mayai unaweza fuga chotara(sasso) ambapo utaanza kuwalisha chakula cha layers wakiwa na umri wa wiki 2, lakini fanya ivo kama eneo ulilopo mayai ya chotara yanauzwa kwa bei kubwa kama ya kienyeji... mfano niliko mimi trei ya mayai ya chotara 12,000 ila kama yanauzwa kama ya kisasa fuga layers pure kwa sababu idadi ya mayai yatakayotagwa na chotara ni tofauti na layers pure.
5. kama vyote vinademand sawa, tenga tu mabanda... fuga wote mean wa nyama unakuwa unawaleta na kuwatoa kila baada ya miezi 3 labda, ila wa mayai wanakuwepo na watataga mpk miaka 3 min.
Jitahidi sana ukianza kufuga kuandaa vizuri mazingira na kuwapa kuku wako chanjo muhimu, Magonjwa yanasababishia hasara wafugaji wengi mpk wengi wanakata tamaa.