Biashara ya kunenepesha ng’ombe,mbuzi na kondoo kisha kuwauza

Biashara ya kunenepesha ng’ombe,mbuzi na kondoo kisha kuwauza

mkoba mweupe

Senior Member
Joined
Feb 25, 2017
Posts
119
Reaction score
190
BIASHARA YA KUNENEPESHA NG’OMBE,MBUZI NA KONDOO KISHA KUWAUZA ( CATTLE AND GOAT FEEDLOTS

Habarini wana Jamvi naomba kushare hili jambo kidogo tupate elimu,ushauri na changamoto zake.

Kuna Hii biashara ya kunenepesha Mifugo hasa ng’ombe na Mbuzi Kisha kuwauza nasikia inalipa sana na inafaida sana Kama utakuwa uko serious na kufuata formula sahihi ya chakula na virutubisho sahihi kwa ajili ya kunenepesha mifugo .
Baada ya hapo unawapiga bei ndefu na yenye faida

Kuna mzee mmoja yupo Kilosa alikuwa rafiki yangu sana yeye alikuwa ananunua NG’OMBE waliokonda kipindi cha kiangaz anawatibu kisha anawipigisha msosi wa maana wakinenepa anawauza kwa faida.

Kwa anaeifahamu vizur hii biashara naomba atupe madini Mazee tumechoka kuajiriwa na kusubiri mwisho wa Mwezi 🤣🤣
 
Naifanya hii kazi, Kahama na Ikunzi Runzewe.

Faida ipo, sio kila siku utapata faida, kuna hasara pia. Mojawapo ya Hasara ni Migogoro ya Wakulima, Soko la ng'ombe wanaotoka pori kuanzia mwezi wa 11-12, alafu 4-6, changamoto nyingine uhaba wa pumba za alzeti, pamba. Changamoto nyingine baadhi ya ng'ombe kukataa kabisa kuyala mapumba haswa yale yaliyochanganywa na pumba za pamba, mchele, alzeti.

Mwenye mabasi ya Frester ameifanya sana hii biashara alikuwa ananunuaga zaidi ya ng'ombe 1000, mchagga mmoja ivi akili mingi.

Karibu chamani, usitegemee one source of income.
 
Kwanza kapate elimu kuhusu ufugaji io ni biashara nzuri tu japo inahitaji uangalizi mzuri
 
Mkuu kama huna eneo la kutosha usithubutu, cattle are heavy feeder. Badala ya kunenepesha utawakondesha zaidi.

Wenzetu hapo Kenya na South Africa wanatumia Eneo kidogo tu kufanya hii biashara Ila sasa gharama naona itakuwa kubwa Kama utawalisha Pumba tu na vyakula vya kununua bila Nyasi
Mm nakubaliana na ww kwenye Eneo ni sawa kabisa Ila sio kwenye ukuaji bali ni kupunguza gharama za malisho
 
Mkuu kama huna eneo la kutosha usithubutu, cattle are heavy feeder. Badala ya kunenepesha utawakondesha zaidi.
Ng'ombe ni mnyama mmoja uneconomical sijui binadamu kwanini alipendekeza aliwe commercially. Ng'ombe alifaa alimie tu na kufugwa nyumbani kishkaji sio kibiashara. Mwenzake kuku vilevile.

Nguruwe is far more economical. Sungura huyo ndio kazidi, kwanza nyama yake ina virutubisho vingi zaidi na ni salama zaidi kwa afya. Pili anazaliana hana mfano. Tatu anakula chakula kidogo, feed conversion rate yake ni kubwa sana.
 
Back
Top Bottom