Biashara ya Kununua magari yaliyopata Ajali

Mtoto Tajiri

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2014
Posts
300
Reaction score
173
Kwa wale wanaojua au ni wazoefu wa biashara hii ya kununua magari yaliyopata Ajali na yale mabovu naomba tu share Idea,Nataka kujua mtaji pia njinsi ya manunuzi ili upate faida hasa hasa gari ziwe Canter,Corrola na Toyota hiace,Natanguliza shukrani.
 
ndugu yangu biashara hiyo ukifanya inakutoa muda si mrefu.nakupatia namba za jamaa huyu alianza biashara hiyo miaka kama mitatu iliyopita lakini sasa ni tajiri.anaitwa bakari used autospare parts yupo dodoma, karibu na msikiti wa ghadafi,0754025923.yeye huwa ananua magari na kuanza kutoa spare tofauti tofauti
Kwa wale wanaojua au ni wazoefu wa biashara hii ya kununua magari yaliyopata Ajali na yale mabovu naomba tu share Idea,Nataka kujua mtaji pia njinsi ya manunuzi ili upate faida hasa hasa gari ziwe Canter,Corrola na Toyota hiace,Natanguliza shukrani.
 
Shukrani kwa mchango wako,ila nilikuwa nahitaji mchanganuo mzima wa Biashara,Natanguliza shukrani.
 
Wakuu hii si kama biashara ya kuuza majeneza vile?
Maana kama ajali hazipatikani basi unasikitika sana watu wapate ajali ili biashara ipatikane.
Utakapo ingia katika biashara hii fanya yafuatatayo
-Tafuta mtu anaetengeneza majeneza,ili mpange kwamba unanunua gari iliyopata ajalio na maiti wake.
-Tafuta wale wafanyakazi wa Mortuaries watakuambia kila ajali iliyotokea eneo husika,maana wao ndio wanaopokea maiti.Sasa hapo itakuwa kazi kwako wewe kuwahi kwenye tukio kuweka order ya gari husika na mwenye kutengeneza majeneza na yeye anaweka order hapo hapo.

Anyway,ni biashara nzuri sana ila lazima utafuta kijana mwenye uzoefu na masuala ya Ufundi magari ili awe anakufanyia uthaminisho wa bidhaa,maana yeye ndio atajua kwamba kwa bei husika inalipa au la,ila kama wewe huna uzoefu wa mambo hayo itakupa tabu sana,maana hata wauzaji wa gari za ajali huwa wanaangalia kama mhusika una idea ya masuala ya kiufundi na kujua uthamini wa muonekano wa gari na uharibifu wake.
 
Mkuu kwa kifupi nimekupata,Shukrani kwa mchango wako,kuhusu idea ya magari ninayo sababu nafanya biashara ya Daladala najua bei ya karibu spare Zote ila nilitaka nijikite na huu upande wa pili ndio maana nilikuwa naomba mchanganuo mzima kwa ujumla.
 
Kama una Idea ya mambo ya spare za magari basi hili ni bonge la mpango la biashara.
Natumai watakuja wataala wa maichanganuo ila wazo lako zuri
 
Shukrani zangu zote ziwaendee wale wote waliochangia na wale wataokuja baadae!,mchango wako ni muhimu sana kwangu.
 
Kwa wale wanaojua au ni wazoefu wa biashara hii ya kununua magari yaliyopata Ajali na yale mabovu naomba tu share Idea,Nataka kujua mtaji pia njinsi ya manunuzi ili upate faida hasa hasa gari ziwe Canter,Corrola na Toyota hiace,Natanguliza shukrani.

mimi ninayo Nissan Safari ya zamani hajiapata ajali ila naiuza maana imezeeka sana. haitembei ila ikiwekwa betri 2 inawaka na kutembea vema tu. niPm kama utahitaji au kama una mtu anayehitaji.
 
mimi ninayo Nissan Safari ya zamani hajiapata ajali ila naiuza maana imezeeka sana. haitembei ila ikiwekwa betri 2 inawaka na kutembea vema tu. niPm kama utahitaji au kama una mtu anayehitaji.
Bado hujakidhi vigezo na masharti ya mnunuzi,umeambiwa iwe imepata ajali,sasa wewe unauza nzima,vipi mkuu.
Kwa kukusaidia tu,tafuta teja mpe laki moja tu halafu umuwashie akaipige kwenye mti pwaa, halafu umpigie jamaa aje ainunue,maana ajali itakuwa tayari imepataikana.
 
Hahahaha!wakuu tuache utani tuzungumzie biashara!
 
Kwa kifupi natumaini mada yangu inaeleweka vizuri,Bado nahitaji uchambuzi wa Biashara hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…