Biashara ya kununua maziwa Kibaha na kuuza Dar

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
1,527
Reaction score
3,811
Habari zenu wakuu,

Kuna wafugaji kadhaa wapo Kibaha nilianza mazungumzo nao ya kununua maziwa kwao na kuyaleta kuuza Dar na wapo tayari kwa hilo.

Wao wamesema wataniuzia kwa sh 1000 kwa lita namimi nina mpango wa kuuza sh 1800 kwa lita.

Kwa ujumla wana uwezo wa kuniuzia lita mia mbili kila siku.

Sasahivi nipo nafanya research ya masoko, nafikiria wateja wakuu watakuwa ni kina nani ambao wanaweza kununua minimum ya litre tano kwa siku.

Naomba ushauri wa kimasoko na ushauri mwingine wowote ule wa kunisaidia katika biashara hii.

Mbarikiwe.
 
Uzoefu mdogo nilionao kwa kuona, wanao uza maziwa kwa wingi wanapita mitaani na magari yao kama kwetu ni j3 na alhamis na bei ni shs1,500/=
 
jaribu kwenda ndani ndani vijijini zaidi upate kwa 800/= au 900/= kufidia garama za usafiri, SOKO NI KUZUNGUKA MTAANI NA KUULIZIA NA PITA SOKO NI UAMINIFU WAKO WA KUFIKISHA MAZIWA KILA SIKU
=> KWA BEI YA KUUZIA ANZA KWA BEI YA 1400/= ili uteke soko kwanza ndo uje kupandisha
=> bei ya maeneo mengi ni 1500/= kwa jumla
=> kwa wauzaji wa rejareja wanauza 1600,1700, 1800, 2000 inategemeana na eneo na ubora wa maziwa yenyewe MAANA WENGNE HUWEKA MAJI MPAKA INABAKI RANGI TU SIO MAZIWA TENA
 
Wazo zuri ila uwe mwaminifu. Nasikia uchakachuaji upo sana kuna wauzaji wasio waamninifu wanaongeza unga maji na mafuta ya kula kuleta cream ya janja janja na ujazo mwingi.
 
Wazo zuri ila uwe mwaminifu. Nasikia uchakachuaji upo sana kuna wauzaji wasio waamninifu wanaongeza unga maji na mafuta ya kula kuleta cream ya janja janja na ujazo mwingi.
Vipo vifaa vya kupima uchakachuaji wa maziwa
 
Mkamuaaji anaongeza maji ili baada ya kumuibia boss lita kadhaa, boss anaongeza maji ili maziwa yawe mengi, mchuuzi anaekuja kununua kwa boss nae anaongeza maji ili apate faida, mtaani nako tukisha nunua toka kwa mchuuzi tunaongeza maji ili chai iwe nyingi tutoshe kwenye familia maana tuko mtu 9,bora unywe chai ya rangi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaaa walai kwa mtindo huo bora chai ya rangi, unatia tangawiz na iriki mwendo mchibuyuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah kitu serial dilution [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahhahahahaa nimecheka saaaana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh Hongera sana kwa kuwa na family ya watu 9 usawa huu?
 
Uzoefu mdogo nilionao kwa kuona, wanao uza maziwa kwa wingi wanapita mitaani na magari yao kama kwetu ni j3 na alhamis na bei ni shs1,500/=
Hofu ni vichanganyiko humo ndani siku hizi wanaweka maji ......maziwa yanakuwa mepesi....wanaboa sana

SONY Xperia Z5 Premium
 
Ha ha ha ha ha ha kweli kabisa hiyo ni dhahiri

SONY Xperia Z5 Premium
 
Mkuu habari,samahani bado unafanya hii biashara? Mimi niko DSM natafuta wafugaji wa kuniuzia maziwa au wauzaji wa jumla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…