Biashara ya kununua na kuuza dola


Hiyo itakuwa biashara haramu ndugu. Tafuta vibali vinginevyo utafilisiwa na kujikuta polisi, mahakamani na mwisho magereza
 
napataje vibali mkuu! nipe uzoefu....

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukienda BOT watakupa maelekezo, ila kwa sasa sikushauri sana, kwani hii serikali haitabiriki. Kipindi cha nyuma kidogo BOT wakishirikiana wanajeshi walivamia maduka ya kubadilishia fedha, wakachukua fedha zote walizokuwa nazo, alafu wakayafunga maduka hayo, na mpaka sasa maduka hayo yamefungwa, na sijui wataruhusiwa kuyafungua tena.
 
Mimi kama tapeli wa forex nakushauri hivi.. Ni ngumu kupata faida unayoifikiria kwa haraka kwa kuwa kuna kitu inaitwa spread hii ni ile tofauti ya bei ya kubuy na kusell.. Mfano unaona kwenye bango wameandika Buy 2300 sell 2400

ina maana ukienda kununua Dollar hapo utalipa 2400 kwa dola 1..

Na ukitaka kuiuza wakati huo huo utapata hasara ya 100 coz utauza kwa 2300..

Ili upate faida inabidi usubiri sana hadi bei ipande kuzidi 2400 ambayo utasubiri sana bila mafanikio.

Sikushauri kifanya hicho kitu sababu hakina faida yeyote badala yake unaweza kufanya biashara zingine zenye tija.. Ni ushauri wangu tu kwako.. Japo ushauri mzuri sio rahisi kuupatta ila zingatia huo.

#tapeliwaforex [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Are you sure ulimbo?!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…