Habarini wakuu, naombeni msaada kwa mwenye uzoefu, nataka nianze hii biashara ila sina baadhi ya taarifa hope wapo wenye uzoefu watanijuza, kama mlivoelezea juu hapo kuwa miezi ya mwanzo wa mwaka bei ya mahindi huwa inapanda kidogo, Taarifa kubwa ninayotaka kujua ni muda wa mavuno sababu mara nyingi bei ndio huwa inashuka, Naombeni mnijuze misimu ya mavuno au upatikanaji wa mahindi kulingana na mikoa kwa mfano kama sasa nikitaka mahindi nikachukue mkoa gani? maana nimejaribu kufuatilia bei wilaya kama ya sumbawanga naona wao mahindi yapo juu kidogo nadhani waliwahi kuvuna, nisaidieni kwenye hili jamani wenye uzoefu kwenye biashara hii. Yani kwa kifupi nataka nijue kwa kuanzia kama sahivi mkoa gani mahindi yanapatikana kwa wingi na mnijuze kila mkoa na miezi yake ya mavuno. Nitashukuru nikipata majibu ya hayo maswali yangu kwa haraka.
Natanguliza shukrani, Ahsanteni.