Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Duh! Mi mwenyew napenda sana kuifanya hiyo biashara ya nafaka ila tatzo mtaji wang ni kdogo mno 600,000
 
Wakuu kama kuna mtu mwenye ujuzi wa biashara ya kununua mpunga then anakoboa na kuuza mchele naomba anisaidie kujibu maswali yafuatayo.

1. Nitajuaje mpunga ambao nikikoboa hautovunjika?

2. Gunia la debe 10/10 la mpunga nikikoboa nitatoa debe ngapi za mchele?

3. Kati ya Mbeya na Iringa wapi kuna mpunga mzuri?

4. Bei za kusafirisha mchele mikoa hiyo miwili?

5. Bei ya kukoboa mpunga kati ya mikoa hiyo miwili?

Naombeni mnisaidie japo najaribu kutafa hizo information huku mtaani, nisaidie nami kijana mwenzako nifanikiwe ili niwasaidie wengine.

Karibuni PM pia
 
ngoja mwenyewe nisubiri majibu ya haya maswali ili nijazilizie taarifa
 
utaniita w
Kwan ww unataarifa zipi mkuu
kaka taarifa zangu ni za kutoa mazao katavi(mpanda)
 
Pindi wakiwa wanavuna ndio muda mzur maana gunia la debe 6 linachezeaga kwenye 26-30 maana wanakua bado wana arosto la pesa.

Vitu vingne kama Ushuru na usafiri ni mamb madogo madogo tu.

MWENYEZI MUNGU akinijaalia huu msimu mwez wa tano nataka nianze na kimtaji changu kidogo.
 
Utanishtua msimu ukifika
 
Huyo anae hitaji mashine za kusaga na kukuboa tuwasiliane
 
Waungwana habari za jioni, kama kichwa cha habari kinavojieleza naomba kujua kutoka kwa mwenye uelewa wa biashara ya mchele kutoka morogoro he kwa sasa bidhaa hii inapatikana na he changamoto sake zikoje? Nataka kusafirisha kupeleka Zanzibar. Nitashukuru kama nitapata angalau taarifa ya bei kwa sasa ilivo.
 
Natamani kufanya biashara ya mazao ila sina uelewa nayo naomba MTU mwenye kuijua anipe muongozo natakiwa nianze na mtaji wa kiasi gani soko likoje mfano ndizi ,viazi,vitunguu nk
 


Mkuu wengine tuna uzoefu wa haya maswali yako lakini nashindwa kukupa majibu ya moja kwa moja kutokana na mikoa uliotaja hapo tofauti na mimi nilipokua nachukulia ,so naweza kukupa majibu yasijiotosheleza kulingana na hitaji lako.

Ila kama hutaitaji ufafanuzi wangu mimi ambae nilikua nachukulia mchele maeneo ya ifakara,mang'ula kilombero ntashare nawe uzoefu

Asante
 
Pindi nikiwa tayari nitakutafuta mkuu
 
Wadau Nauza mahindi yapo mbeya Mjini gunia la kg 100 ni 48,000 tu, mwenye kuhitaji Njoo PM tuyajengee!
 

1- Mpunga ambao hautavunjika wakati wa kukoboa utaujua kwa kupekecha kwenye viganja vyako sampuli ya mpunga unaotaka kukoboa km unakatika basi utaona umekatika karibia mpunga wote uliopekecha
2- Gunia la debe 10 unatoa kg 75-80 ambapo gunia ilo la mpunga linakua na kg 100-120
3- Mpunga mzuri unapatikana mbeya ambapo kamsamba kutoka chunya unashika namba moja,kufuatiwa mchele kutoka kyela na mwisho n mbalari katika mkoa wa mbeya ila mbarali ndio unapatikana mchele mwingi zaid takribana robo tatu ya mchele wote kutoka mbeya
4- Bei za kusafilishia mchele ni Tsh.7000/= kwa kila kg 100
5- Bei ya kukoboa mpunga ni Tsh5000 kwa kila gunia moja

Kama kunasehemu sijaeleweka nakaribisha maswali
 
Adam unafanya hii biashara? Samahani maana nataka nikutafute tuyajenge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…